Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Inaonesha wazi hili limewakuta katika namna ya kuwashangaza kidogo, au siyo mkubwa...?

By the way hivi hiki ukiandikacho ya kuwa "sheria inaruhusu kubadilisha hati ya mashitaka kwa kuondoa shitaka X na kuanzisha shitaka jipya Y" ni kwa mujibu wa sheria gani na kifungu gani cha sheria hiyo...?

Au unasukumwa na mihemko na matamanio yako tu mkubwa kisha unaandika hapa...?.
 
Ujinga tu wa CCM na serekali yake....
-Kwamba anakabiliwa na mashtaka mazitooo!.
- kisha ataandaliwa mashtaka mazitooo! ambayo ni magumu kuyapangua!......
Ha ha haaa. Only in Tanzania. Sasa wakiandaa kinyume na hati hii yakwanza si ndo itakula kwao mazima. Waache wajichanganye tu
 
Wengi tunajadili hili jambo blindly tu kwa kusukumwa na misukumo binafsi inayosukumwa na itikadi za kisiasa bila kujiuliza maswali muhimu ya msingi ya kisheria....

Labda kwa kujengeana ufahamu wa mambo haya ya kisheria, hebu tusaidie kujibu haya;

1. Hati ya mshtaka kwa mujibu wa Criminal Prosecution Act [CPA] ni nini...?

2. Kisheria, hii hati ya mashtaka;

å Kazi yake hasa ni nini...?

å Inaandaliwa na nani...?

å Wakati gani inapaswa kuandaliwa..?

å Ni hatua gani za kisheria zinapaswa kufuatwa wakati wa kuindaa...?

å Ikitokea imekosewa kuandaliwa sheria inasemaje....?

NB: Ni bora wanasheria wakafunga mjadala huu kwa kutoa ufafanuzi wa kisheria..
 
Kwamba mashitaka "mazito zaidi" yatatokana na tuhuma zile zile au kuna tuhuma mpya?.... ( Kumbuka CCM na serekali yake hugawa tuhuma kwa wale wawapendao)
 
Hii kesi CCM wasipokuwa makini itawaacha uchi...waachane nayo mapema!!

Jaji katoka mnyonge maskini...sijawahi kushuhudia Jaji anawashauri waleta mashitaka wakarekebishe shitaka wakati wao hata hawajaiomba mahakama..aisee.
Kuna vitu haijalishi, inafikka unaona ujinga, wakati hufika maji yanatoka nshingo , hii wale hawakujipanga
 
Mashitaka gani Nje ya kesi ya msingi?? Upande wa Jamhuri umeonyesha udhaifu mkubwa hasa ktk kesi hii. Hawakujiandaa na ndiyo maana Jaji akaona sihitaji kuwekwa kwenye rekodi na baadae yatumike kuwaumiza wengine.

Walikurupuka kutengeneza kesi isiyokuwa na dhamana wakidhani wanamkomoa Mbowe. Matokeo yake ni kuwabebesha Mahakama mzigo unao onekana wazi kuwaelemea.
 
Niamini kuwa wewe pia ni Mwanasheria, la hoja yako yaweza kuwa umekurupuka, kwa kuwa hujaeleza mapungufu yake
 
Sahau, Mbowe hatakaa afungwe
Wajifanya shindana na Mungu ,so watajua hawajui, huwa nasema na nitasema, wasiojua wakapitie post ZANGU tangu 2019, na modi awakumbushe mchango nilisema 2020 mungu anaenda tenda maajabu.
2021, nilisema mwaka mgum twaenda limia meno na kucha, tafadhali mods tafuta post hizi na ziwe wazi, mengine hua ni magum ukiyataja wazi wazi waweza itwa gaidi , mungu katupa uwezo huo basi tu
 
Haja kataa ila vifungu viko wazi, anakikiri vifungu au shitaka halijakidhi vigezo then ,anakwambia upande wa mashitaka wabadilishe kesi,nchi ngani hii ni, haibu juu ya aibu,thanks mh mbowe
Mkuu, ndo kukataa kwenyewe ....
 
Kwani ulikuwa hujui!
 
Nina maombi yangu binafsi kuanzia usiku huu nataka nimuone mungu wangu Alie up to date , na nipate majibu ,niongee nae KWa wole WOTE hawatendi haki kisa danganywa na nyama,anasa za kidunia , halikubaliki ,na mungu amekataaa
Sasa 9 na dakika 47 nitaanza ongea na mungu wangu ulipo mda huo, sema tu Mungu mkubwa, usiamuke maana huu ni WITO sio WOTE waweza, ila hata ukiwa umeshutuka KWa Alam sema tu Mungu mkubwa ,saa 9 na dakika 47 Kama utaweza
 
kisheria charge sheet ndio inayomwezesha mtuhumiwa kuweza kujitetea......sasa kama kuna fabricated offenses (if any) inakuwa ngumu kwa accussed kujitetea; ndio maana Mawakili wa utetezi wameweka nguvu nyingi kwenye PO =Preliminary Objections.

Hapo umepigilia msumari katika kesi hii. Shukrani kwa somo ambalo tutafaidika nalo wanaJF na umma mpana wa wasomaji wa mtandao namba moja wa waswahili duniani kote.
 
Unafikiri Mbowe hajui hayo yote?? Kuingia kwenye Hayo mapambano alijua kwamba siyo jela tu, anaweza kufa! Anachokipigania Mbowe, kitakua hata wakimkata kichwa, Kwa hiyo kuendelea kusota ni kumwongezea chura mwendo kwa kumpiga teke!
 
Jaji Luvanda keshaiharibu kesi kiujumla. Ameonesha Mahakama ina upande,jambo ambalo hakupaswa kuruhusu lionekane!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…