The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Inaonesha wazi hili limewakuta katika namna ya kuwashangaza kidogo, au siyo mkubwa...?Kimsingi sheria haizuii hati ya mashitaka kufanyiwa marekebisho muda wowote ule wakati kesi ikiendelea, lkn pia Jaji hazuiwi kutoa maelekezo ya kufanya marekebisho kama alivyo fanya Jaji Luvanda, ameona kasoro na amewaelekeza upande wa Jamuhuri wazirebishe ili tu haki iweze kutendeka.
hakuna kosa lolote la kisheria hapo.
Jaji ametumia busara ameona ni bora aelekeze marekebisho yafanyike kuliko kuliondoa shitaka.
Hata kama angeliondoa shitaka dhidi ya Mbowe bado Mbowe asingekuwa huru lazima angeendelea kubaki kizuizini wakati Jamuhuri ikifanyia marekebisho hati ya mashitaka, hivyo alicho kifanya Jaji ni kutumia busara tu maana hakuna ambacho kingebadilika.
kasoro zilizopo ktk hati ya mashitaki hazipelekei kesi kufutwa, ktk sheria kuna tofauti kati ya "kufutwa" na "kuondolewa"
kuondoa shitaka hakumalizi kesi, kesi bado ipo kwa kuwa Jamuhuri bado inania ya kumshitaki mbowe.
tulieni acheni papara tuone utamu wa sheria.
By the way hivi hiki ukiandikacho ya kuwa "sheria inaruhusu kubadilisha hati ya mashitaka kwa kuondoa shitaka X na kuanzisha shitaka jipya Y" ni kwa mujibu wa sheria gani na kifungu gani cha sheria hiyo...?
Au unasukumwa na mihemko na matamanio yako tu mkubwa kisha unaandika hapa...?.