Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Kimsingi sheria haizuii hati ya mashitaka kufanyiwa marekebisho muda wowote ule wakati kesi ikiendelea, lkn pia Jaji hazuiwi kutoa maelekezo ya kufanya marekebisho kama alivyo fanya Jaji Luvanda, ameona kasoro na amewaelekeza upande wa Jamuhuri wazirebishe ili tu haki iweze kutendeka.
hakuna kosa lolote la kisheria hapo.
Jaji ametumia busara ameona ni bora aelekeze marekebisho yafanyike kuliko kuliondoa shitaka.
Hata kama angeliondoa shitaka dhidi ya Mbowe bado Mbowe asingekuwa huru lazima angeendelea kubaki kizuizini wakati Jamuhuri ikifanyia marekebisho hati ya mashitaka, hivyo alicho kifanya Jaji ni kutumia busara tu maana hakuna ambacho kingebadilika.
kasoro zilizopo ktk hati ya mashitaki hazipelekei kesi kufutwa, ktk sheria kuna tofauti kati ya "kufutwa" na "kuondolewa"
kuondoa shitaka hakumalizi kesi, kesi bado ipo kwa kuwa Jamuhuri bado inania ya kumshitaki mbowe.
tulieni acheni papara tuone utamu wa sheria.
Inaonesha wazi hili limewakuta katika namna ya kuwashangaza kidogo, au siyo mkubwa...?

By the way hivi hiki ukiandikacho ya kuwa "sheria inaruhusu kubadilisha hati ya mashitaka kwa kuondoa shitaka X na kuanzisha shitaka jipya Y" ni kwa mujibu wa sheria gani na kifungu gani cha sheria hiyo...?

Au unasukumwa na mihemko na matamanio yako tu mkubwa kisha unaandika hapa...?.
 
Ujinga tu wa CCM na serekali yake....
-Kwamba anakabiliwa na mashtaka mazitooo!.
- kisha ataandaliwa mashtaka mazitooo! ambayo ni magumu kuyapangua!......
Ha ha haaa. Only in Tanzania. Sasa wakiandaa kinyume na hati hii yakwanza si ndo itakula kwao mazima. Waache wajichanganye tu
 
Naamini umesoma na kuelewa mashitaka yanayomkabili na pingamizi za jopo (13) la Mawakili wake, ambazo baadhi zimekubaliwa na Jaji. Pia unatambua kiwango cha hisia za watu wa ndani na nje.

Mawili hayo yanaweka ulazima wa mashtaka kuandaliwa upya kulingana na uzito wa ushahidi walionao ili isije kujitokeza kuwa ni kesi ya "kubambika".

Laiti Mawakili wangeendelea na mashtaka yenye mapungufu, Serikali isingepata nafasi ya kuandaa mashtaka upya
Wengi tunajadili hili jambo blindly tu kwa kusukumwa na misukumo binafsi inayosukumwa na itikadi za kisiasa bila kujiuliza maswali muhimu ya msingi ya kisheria....

Labda kwa kujengeana ufahamu wa mambo haya ya kisheria, hebu tusaidie kujibu haya;

1. Hati ya mshtaka kwa mujibu wa Criminal Prosecution Act [CPA] ni nini...?

2. Kisheria, hii hati ya mashtaka;

å Kazi yake hasa ni nini...?

å Inaandaliwa na nani...?

å Wakati gani inapaswa kuandaliwa..?

å Ni hatua gani za kisheria zinapaswa kufuatwa wakati wa kuindaa...?

å Ikitokea imekosewa kuandaliwa sheria inasemaje....?

NB: Ni bora wanasheria wakafunga mjadala huu kwa kutoa ufafanuzi wa kisheria..
 
Naamini umesoma na kuelewa mashitaka yanayomkabili na pingamizi za jopo (13) la Mawakili wake, ambazo baadhi zimekubaliwa na Jaji. Pia unatambua kiwango cha hisia za watu wa ndani na nje.

Mawili hayo yanaweka ulazima wa mashtaka kuandaliwa upya kulingana na uzito wa ushahidi walionao ili isije kujitokeza kuwa ni kesi ya "kubambika".

Laiti Mawakili wangeendelea na mashtaka yenye mapungufu, Serikali isingepata nafasi ya kuandaa mashtaka upya.
Kwamba mashitaka "mazito zaidi" yatatokana na tuhuma zile zile au kuna tuhuma mpya?.... ( Kumbuka CCM na serekali yake hugawa tuhuma kwa wale wawapendao)
 
Hii kesi CCM wasipokuwa makini itawaacha uchi...waachane nayo mapema!!

Jaji katoka mnyonge maskini...sijawahi kushuhudia Jaji anawashauri waleta mashitaka wakarekebishe shitaka wakati wao hata hawajaiomba mahakama..aisee.
Kuna vitu haijalishi, inafikka unaona ujinga, wakati hufika maji yanatoka nshingo , hii wale hawakujipanga
 
Wapambe wake Mbowe wanasukumwa na hisia kuliko mashtaka dhidi yake ambayo ni mazito kiasi cha kuvuta wawakilishi wa Balozi za nje.

Kama zilivyo hoja zako, Mawakili wa utetezi hawamtendei haki mteja wao. Kwa kuwa hati ya mashtaka ilikuwa na mapungufu wangeendelea na kesi ili watumie mapungufu hayo kujenga hoja za kumnusuru mteja wao. Kitachotokea yataandaliwa mashtaka mazito ambayo watakuwa na kazi kuyapangua
Mashitaka gani Nje ya kesi ya msingi?? Upande wa Jamhuri umeonyesha udhaifu mkubwa hasa ktk kesi hii. Hawakujiandaa na ndiyo maana Jaji akaona sihitaji kuwekwa kwenye rekodi na baadae yatumike kuwaumiza wengine.

Walikurupuka kutengeneza kesi isiyokuwa na dhamana wakidhani wanamkomoa Mbowe. Matokeo yake ni kuwabebesha Mahakama mzigo unao onekana wazi kuwaelemea.
 
Mashitaka gani Nje ya kesi ya msingi?? Upande wa Jamhuri umeonyesha udhaifu mkubwa hasa ktk kesi hii. Hawakujiandaa na ndiyo maana Jaji akaona sihitaji kuwekwa kwenye rekodi na baadae yatumike kuwaumiza wengine.

Walikurupuka kutengeneza kesi isiyokuwa na dhamana wakidhani wanamkomoa Mbowe. Matokeo yake ni kuwabebesha Mahakama mzigo unao onekana wazi kuwaelemea.
Niamini kuwa wewe pia ni Mwanasheria, la hoja yako yaweza kuwa umekurupuka, kwa kuwa hujaeleza mapungufu yake
 
Sahau, Mbowe hatakaa afungwe
Wajifanya shindana na Mungu ,so watajua hawajui, huwa nasema na nitasema, wasiojua wakapitie post ZANGU tangu 2019, na modi awakumbushe mchango nilisema 2020 mungu anaenda tenda maajabu.
2021, nilisema mwaka mgum twaenda limia meno na kucha, tafadhali mods tafuta post hizi na ziwe wazi, mengine hua ni magum ukiyataja wazi wazi waweza itwa gaidi , mungu katupa uwezo huo basi tu
 
Haja kataa ila vifungu viko wazi, anakikiri vifungu au shitaka halijakidhi vigezo then ,anakwambia upande wa mashitaka wabadilishe kesi,nchi ngani hii ni, haibu juu ya aibu,thanks mh mbowe
Mkuu, ndo kukataa kwenyewe ....
 
Jaji amekosea sana kujitoa ktk kesi.
Maana yake ni kwamba tuhuma alizo zitoa Mbowe dhidi ya Jaji ni za kweli.
Kabla ya kujitoa hizo tuhuma lazima kwanza zithibitishwe maaana sio tu kwamba zina mchafua Jaji/Majaji bali zinauchafua Muhimili wa Mahakama.
Kwani ulikuwa hujui!
 
Nina maombi yangu binafsi kuanzia usiku huu nataka nimuone mungu wangu Alie up to date , na nipate majibu ,niongee nae KWa wole WOTE hawatendi haki kisa danganywa na nyama,anasa za kidunia , halikubaliki ,na mungu amekataaa
Sasa 9 na dakika 47 nitaanza ongea na mungu wangu ulipo mda huo, sema tu Mungu mkubwa, usiamuke maana huu ni WITO sio WOTE waweza, ila hata ukiwa umeshutuka KWa Alam sema tu Mungu mkubwa ,saa 9 na dakika 47 Kama utaweza
 
kisheria charge sheet ndio inayomwezesha mtuhumiwa kuweza kujitetea......sasa kama kuna fabricated offenses (if any) inakuwa ngumu kwa accussed kujitetea; ndio maana Mawakili wa utetezi wameweka nguvu nyingi kwenye PO =Preliminary Objections.

Hapo umepigilia msumari katika kesi hii. Shukrani kwa somo ambalo tutafaidika nalo wanaJF na umma mpana wa wasomaji wa mtandao namba moja wa waswahili duniani kote.
 
Nami naomba iwe hivyo (kesi nyepesi).

Ukweli unabaki Mawakili wake hawauoni huo wepesi, kama uonavyo wewe. Ingekuwa nyepesi, kihivyo, wangeendelea na kesi iishe haraka. Pingamizi zinaongeza muda wa mteja kuendelea kusota mahabusu.

NB: Mashitaka ya sasa yakifutwa atakamatwa na mchakato unaanza upya. Yawezekana jopo la Mawakili wake wakaanza pingamizi upya.
Unafikiri Mbowe hajui hayo yote?? Kuingia kwenye Hayo mapambano alijua kwamba siyo jela tu, anaweza kufa! Anachokipigania Mbowe, kitakua hata wakimkata kichwa, Kwa hiyo kuendelea kusota ni kumwongezea chura mwendo kwa kumpiga teke!
 
Jaji Luvanda keshaiharibu kesi kiujumla. Ameonesha Mahakama ina upande,jambo ambalo hakupaswa kuruhusu lionekane!
 
Back
Top Bottom