Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Mbowe anatapatapa tu,20 years in jail Ina mhusu huyu
Mzaha sio mzaha mara pap 20 years...makamanda hapa wataanzisha nyuzi refu kama reli ya kigoma siku ya tatu maisha yataendelea kama kawaida
Masikini mbowe anafungwa hivi hivi kutokana na ujinga wa Watanzania.kuwapigania watu wasiojielewa ni kazi sana.
 
Kengeza la gaidi DJ haliwezi kumtisha jaji mpaka akubali kujitoa, gaidi ajiandae kula mvua za kutosha!. 🤣
 
No retreat no surrender.... One step ahead..!!!

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Jaji amekosea sana kujitoa ktk kesi.
Maana yake ni kwamba tuhuma alizo zitoa Mbowe dhidi ya Jaji ni za kweli.
Kabla ya kujitoa hizo tuhuma lazima kwanza zithibitishwe maaana sio tu kwamba zina mchafua Jaji/Majaji bali zinauchafua Muhimili wa Mahakama.
 
Jaji amekosea sana kujitoa ktk kesi.
maana yake ni kwamba tuhuma alizo zitoa Mbowe dhidi ya Jaji ni za kweli.
kabla ya kujitoa hizo tuhuma lazima kwanza zithibitishwe maaana sio tu kwamba zina mchafua Jaji/Majaji bali zinauchafua Muhimili wa Mahakama.
 
Doh..... Lakini ukiona giza linaongezeka ujue panakaribia kukuchwa
 
Tulishasema tangu mapema kwamba hizi kesi za kutengeneza huwa zina mambo yake , kama binadamu wakati mwingine roho inakusuta .

Baada ya kuanikwa mitandaoni na Sauti Kubwa , hatimaye leo Jaji Luvanda amekubali kujitoa kwenye kesi ya Mbowe , baada ya kuombwa kufanya hivyo kutokana na kumstukia kwamba anatumika .

Huu ni ushindi wa kwanza .
 
Tuhuma alizozitoa Mbowe dhidi ya Jaji Luvanda sio tu zinamchafua yeye bali zinawachafua Majaji wote na Muhimili wa Mahakama.
Hivyo Mbowe na Mawikili wake walipaswa wathibitishe tuhuma hizo nzito.
 
Alisikika mzee wa kusini akitoa tahadhari kwa CCM na vyombo vyake - Ukimungunya nchale, Ukichimama nchale, ukichuchumaa nchale, ...
SWALI KUU KUHUSU MWENENDO WA KESI HII YA MBOWE NA WENZIE WATATU
Mheshimiwa Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuna swali zito sana toka kwa Askofu Bagonza anayejiuliza yafuatayo katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana imetendeka:

1.Serikali / Jamhuri ndivyo ilivyoshtaki.
2.Jaji E. B Luvanda kakubali mashtaka ya serikali yana kasoro
3.Jaji E.B Luvanda anaelekeza namna nzuri ya serikali kumshtaki Mbowe
4.Kwa hiyo
a) Jaji alipaswa amwachie Mbowe.
b) Mbowe hashtakiwi na Jaji anashtakiwa na serikali kupitia ofisi za mwendesha mashtaka DPP na Mawakili wa serikali, vipi jaji na yeye kujiunga upande wa Jamhuri kuwaelekeza kazi ifanywe vipi kisha wamletee halafu hapo haki kweli itatendeka?

Anawaza kwa sauti Askofu Bagonza.
Ni hakika umma wa waTanzania na hadhira ya wadau wengine unaoifuatilia kesi hii kwa makini nao pia fikara zao hazijaachana kwa mbali na anavyofikiri Baba Askofu.

Historia:

Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulibiwe. Akasema, Kwani? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulibiwe. Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe. Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu. Source : Bibilia Takatifu Mt 27: 11-25

Kesi imefikia patamu. Tunaamini kuwa haki itatendeka katika muhimili huu wa Mahakama hii huru ya Tanzania. Mahakama zetu ni huru tofauti na ile ambayo Nelson Mandela na wenziwe walisimama mbele ya Mahakama iliyokuwa chini ya utawala wa gandamizi ulioamini katika kubagua raia wa Afrika ya Kusini.

Mahakama zetu Tanzania haziangalii chama wala kubagua mtu kwa itikadi bali zinazingatia hali halisi ya mwenendo wa kesi ya jinai toka watuhiwa walivyokamatwa, njia zilizotumika ili 'ushahidi' upatikane na kisha DPP kuafiki mashtaka kuletwa mahakamani.

KESI IMEFIKA PATAMU, SASA DUNIA YOTE ILIYOKUWA HAIFAHAMU MATENDO YA CCM YA AWAMU YA 5 NA YA SASA YA AWAMU YA 6 YATAANIKWA NA KUFAHAMIKA KINAGA UBAGA

Kesi hii ya Mbowe itakuwa ktk vitabu kama kesi ya serikali ya makaburu dhidi ya Nelson Mandela. Kesi hii itasomwa ktk historia baada ya CCM kungolewa kutoka madarakani kwa kupitia uchaguzi huru kama kesi ya : Mpinzani Freeman Mbowe ndani ya 'mahakama' za CCM. ifahamike katika mabano neno 'mahakama' ni kuwa CCM inataka kuburuza Mahakama zitumike vibaya pamoja na mfumo wa kusimamia / kuchunguza za jinai (criminal justice system) nzima, lakini imani yetu bado ipo kuwa Mahakama hapa bila "mabano" ni mhimili huru na itatenda haki na kukataa mbinyo wa aina yoyote ile toka upande wowote.

Historia inasema makaburu waliokuwa ktk serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini iliona waAfrika raia wengine waliokuwa wanadai kuwa watu-uhuru, kutaka demokrasia shirikishi na Marndeleo ya watu wote walikuwa ni hatari na wangeweza kuchelewesha maendeleo ya vitu kama madaraja, reli, flyovers pamoja ni miradi mingine mikubwa iliyokuwa ya mfano barani Afrika. Madai hayo ya serikali ya kibaguzi ya wachache ya miaka hii yanarudiwa na CCM miaka hii ya 2015 - 2025. Na CCM pamoja na serikali yake kudai wapinzani ni watu hatari wasio na uzalendo na wasioitakia Tanzania maendeleo.

Soma utetezi wa Nelson Mandela alipofikishwa mbele ya korti na utetezi huo wa Nelson Mandela kuenziwa na watu wote duniani na taasisi kubwa za kimataifa na vyuo vikuu vijana kufunguliwa macho juu ya tawala kandamizi za kibaguzi, katili na vinazokandamiza utu wa watu na haki zao kwa kisingizio cha kujenga uchumi, madaraja, flyovers, mabwawa ya umeme n.k
 
Tuhuma alizozitoa Mbowe dhidi ya Jaji Luvanda sio tu zinamchafua yeye bali zinawachafua Majaji wote na Muhimili wa Mahakama.
Hivyo Mbowe na Mawikili wake walipaswa wathibitishe tuhuma hizo nzito.
 
Kwani Jaji ameshajitoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…