Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Kisheria siyo kila makosa kwenye hati ya mashtaka yanaletea mashtaka yote kufutwa. Kuna makosa yanarekebishwa na kesi inaendelea. Hata wewe ukijaza sehemu fulani vibaya kwenye form, haimaanishi kwamba jambo hilo sasa lifutwe. Mfano ufutwe chuo, ufutwe kazini, ufutiwe mkopo wa elimu n.k. Haki ni kupima uzito wa makosa. Anayepima uzito huo ni Jaji na siyo mwingine.
Haya ni Mambo ya kisheria ndugu sio sawa na mawazo yako.
Kisheria alipaswa aifute hio kesi na kuwachia watuhumiwa. Miongozo ya kesi zote za mahakama kuu na mahakama za Rufani zinaelekeza namna hiyo. Kitendo cha Mhe. Luvanda kukiri kuwa charge sheet ina makosa ilipaswa afafanue kama charge sheet ni curable au ni defective ili kuweka misingi ya haki kwa pande zote.
Kwa kuwa amekiri kuwa charge sheet ni defective it means haiwezi kurekebishika hivyo hivyo alipaswa aamue kwa kumfavor mtuhumiwa.
 

Attachments

Ni swali fikirishi tu na pengine ujasiri wa mtu aitwa mheshimiwa Jaji.
Kituko cha kisheria leo Jaji Luvanda kuombwa kujitoa katika kesi ya ufafanuzi pingamizi la kesi ya ugaidi inayomkabili Mbowe, imeinua macho ya wengi.

Miaka kadhaa iliyopita Jaji Jasiri, tena mwanamke , Jaji Atuganile Ngwala, aliwafurumusha serikali kwa kutosimamia haki katika suala la wasimamizi wa uchaguzi.

Jaji Attu Ngwala sliinyesha ujasiri mkubwa kwa kusisimamia sheria ,haki na ukweli.

Nina uhakika kukataliwa Jaji Luvanda, leo ni kama naye hatapata usingizi na yuko lock up ya kisheria.
The precedence has been made.
 
Aibu kubwa sana kwa mahakama zetu Tanzania, hatuna uhuru wa mahakama kabisa bora zifungwe majengo yageuzwe ofisi ndogo za CCM.

Mpaka kufikia hapa serikali imeshacheza vibaya karata zake, namna nzuri ya kujificha kwenye hii aibu watafute namna waifute hiyo kesi, hii michezo ya watu wa TISS kutumika kuamua haki za wapinzani ni ujinga.
 
Dada labda uje nikupakue mb za kutosha,inaonekana mumeo anakupa mb chache sana,njoo nkupakue na mafuta ya mnara utaona faida yake ...mimba utapata mapacha
Hizi hasira zako kuzionesha hapa ni kupoteza muda!

Nenda kazioneshee pale kisutu kwa gaidi wako!
 
Sasa hivi atakuwa anapiga mvinyo wa presidential kutoka Dodoma. Hii kesi ingemtia najisi ya mwaka. Baada ya kuona Mbowe kashukiwa na Roho Mtakatifu kwa kumtaka ajitoe akaona hapohapo ndo pakuponea. Akanawa mikono akashukuru akasema "Damu ya hawa watu na iwe juu yenu na juu ya watoto wenu" Akasepa zake.
 
Atapewa ujaji mkuu. Subiri uone, hii ndio Tanzania
 
SWALI KUU KUHUSU MWENENDO WA KESI HII YA MBOWE NA WENZIE WATATU
Mheshimiwa Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuna swali zito sana toka kwa Askofu Bagonza anayejiuliza yafuatayo katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana imetendeka:

1.Serikali / Jamhuri ndivyo ilivyoshtaki.
2.Jaji E. B Luvanda kakubali mashtaka ya serikali yana kasoro
3.Jaji E.B Luvanda anaelekeza namna nzuri ya serikali kumshtaki Mbowe
4.Kwa hiyo
a) Jaji alipaswa amwachie Mbowe.
b) Mbowe hashtakiwi na Jaji anashtakiwa na serikali kupitia ofisi za mwendesha mashtaka DPP na Mawakili wa serikali, vipi jaji na yeye kujiunga upande wa Jamhuri kuwaelekeza kazi ifanywe vipi kisha wamletee halafu hapo haki kweli itatendeka?

Anawaza kwa sauti Askofu Bagonza.
 
Jaji mbona anaonyesha weaknesses, Jaji hawezi yumbishwa na akina Mbowe.
Kaah😡
 
Ni heri angeifuta na kumuachia kisha Polisi wakamkamata na kumshitaki kama pilato alivyo elekeza...
 
Luvanda amethibitisha bila chenga kuwa ni mtu wa serikali na anapokea maagizo kutoka serikalini! Kwa kesi hii aliingizwa cha kike?
Inawezekana ni UWT pia maana wamejazana kila kona.
 
Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake
Sasa ni sawa. Huyu jaji ni kati ya majaji hopeless.. Haja wahi kufuata sheria kwenye maamuzi.

Yuko kama yule Mutungi. Na hakimu mmoja anaitwa Simba. We need justice kwa Mbowe.

Haya ndiyo matokeo ya vyeo vya kuhongwa. Sasahii inakwenda kuwa rejea mahakama kuu.
 
Huyu ndiye anaenda kumreplace Jaji Luvanda
1630927519551.png
 
Nafahamu kuwa Jaji yeyote anaweza kujitoa kusikiliza kesi yoyote ile endapo tu tuhuma hizo zitathibitika kuwa ni za kweli na zitapelekea haki kutokutendeka.

Sasa tuhuma alizo zitoa Mbowe na Mawakili wake dhidi ya Jaji Luvabda eti kuwa amepewa maelekezo kutoka juu kuwa amfunge Mbowe, tuhuma hizi zilipaswa zithibitishwe kwanza kabla ya Jaji kujitoa kusikiliza kesi hiyo.
nasema hivyo kwa sababu zifuatazo;

1. Tuhuma zilizo tolewa dhidi ya Jaji ni tuhuma nzito ambazo sio tu kwamba zinamchafua yeye Jaji Luvanda bali zinawachafua Majaji wote wa Tanzania bara na Muhimili wa Mahakama kwa ujumla wake kuwa hawatendi haki.

Tuhuma hizo zilipaswa zithibitishwe kwanza, huko ni kuichafua Mahakama, na wananchi wa kawaida watapoteza IMANI na MAHAKAMA.
Kwa kitendo cha Jaji kuamua kujitoa bila hata tuhuma hizo kuthibitishwa kumewaabisha Majaji wote pamoja na Muhimili kuwa huwa hawatendi haki.
 
Hii ni aibu kwa mamlaka ya nchi, kuanzia mahakama mpaka serikalini, kutaka kumfunga Mbowe kijanja halafu baadae aje kuachiwa na Rais ili aonekane ana huruma kwa Chadema ni ujinga.

Tabia ya kuchezea haki za watu kwa lengo la kutafuta mtaji wa kisiasa itasababisha chuki itawale kati ya wananchi na vyombo vya utoaji haki vinavyoibeba CCM havitaaminiwa tena na wengi, watu wataanza kujichukulia sheria mkononi.
 
6 Sept 2021
Mahakama Kuu
Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
Dar es Salaam, Tanzania

Wakili Peter Kibatala azungumza baada ya Jaji Luvanda kujiengua



Habari kubwa iliyojitokeza Leo ni Jaji Luvanda ajitoa kesi ya Mbowe na wenzake.

Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya Ugaidi, amejitoa kusikikiza kesi hiyo.

Sababu ya kujitoa katika kesi hiyo ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuieleza mahakama hiyo kuwa yeye na washtakiwa wenzake watatu hawana imani na Jaji huyo katika kutenda haki dhidi ya kesi yao.

Kesi imehairishwa mpaka jaji mwingine atakapopatikana. Pia awali Jaji Elinaza Benjamin Luvanda alikataa kutoa uamuzi wake leo juu ya mapingamizi ya upande wa utetetezi mpaka atapopata hansard / kumbukumbu za majadiliano ya Bunge kuhusu sheria ya ugaidi.

Wote walikubaliana kuwa kesi hii ina masilahi mapana kwa umma wote waliopo ndani ya Mahakama na nje.

Hoja 3 za upande za upande wa utetezi zilikuwa zinashambulia madhaifu na kasoro ya hati ya mashtaka. Hoja ya kwanza ilikubaliwa na jaji wakati hoja ya pili ilikubaliwa kwa nusu yake na jaji wakati hoja ya tatu ya kutupiliwa mbali au kufutwa kesi, jaji aliikataa.

Na kwa msingi huo mtuhumiwa Freeman Mbowe kwa niaba ya wenzake akasimama na kusema hawana imani na Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuendelea kusikiliza kesi hiyo, na mheshimiwa Jaji E.B Luvanda akaafiki ombi hilo na kujiengua kusikiliza kesi hii.
Source : Mwananchi Digital
 
Back
Top Bottom