GE2025 Jaji Hamidu Mwanga akataa kujitoa kwenye kesi ya CHADEMA

GE2025 Jaji Hamidu Mwanga akataa kujitoa kwenye kesi ya CHADEMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
photo_2025-07-28_10-01-32.jpg
Jaji Hamidu Mwanga, anayesikiliza hoja za ombi la kutaka ajitoe kwenye Kesi Namba 8323/2025, iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Said Issa Mohammed, dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho, amesema kwamba anakataa kujitoa kama ilivyoombwa, kwa kuwa hakuna sababu za msingi zilizowasilishwa.

Akisoma uamuzi wa Mahakama, Jaji Mwanga amekataa hoja zote zilizowasilishwa na CHADEMA zikitaka ajitoe kwenye kesi hiyo.

Katika hoja ya kwanza, kuhusu uamuzi uliotolewa Juni 10, 2025 wa kuweka zuio la muda kwa CHADEMA kufanya shughuli za kiutendaji (siasa), jambo ambalo CHADEMA walipinga, Jaji amesema kuwa uamuzi wa Jaji katika shauri hauwezi kuwa sababu ya kumlazimu kujitoa. Ameeleza kuwa upo utaratibu mwingine wa kisheria iwapo kuna kutokubaliana na uamuzi wa Mahakama.

Kuhusu hoja inayomhusu Wakili Edison Kiratu, ambaye alidaiwa kuandika barua kwa niaba ya mmoja wa walalamikaji katika kesi hiyo ili ajitoe, pamoja na madai kuwa hakupata nafasi ya kusikilizwa na kwamba Jaji alitoa haki kwa upande mmoja, Jaji amesema kuwa hoja hiyo haina mashiko. Ameeleza kuwa Wakili Kiratu hajawahi kufika Mahakamani na hayupo kwenye rekodi za Mahakama katika shauri hilo. Aidha, ameongeza kuwa inaonekana alileta nyaraka na ‘kuziacha’ Mahakamani kisha kutoweka, jambo ambalo amesema halikubaliki kisheria.

Katika hoja nyingine iliyowasilishwa na CHADEMA, ambayo ilidai kuwa Jaji Mwanga aliwahi kuwa mtendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC, ambayo sasa ni INEC), hivyo hawezi kutoa uamuzi kutokana na rekodi za karibuni kati ya CHADEMA na Tume hiyo, Jaji amekataa hoja hiyo akieleza kuwa hilo haliwezi kuwa sababu ya msingi ya yeye kujitoa. Amesema kuwa NEC si sehemu ya shauri lililopo Mahakamani, na kwamba historia ya ajira katika Tume hiyo haiwezi kutumika kama msingi wa kujitoa kwake katika kesi hiyo.

Aidha, kuhusu hoja nyingine iliyowasilishwa na CHADEMA kwamba wamewasilisha malalamiko dhidi ya Jaji huyo kwenye Tume ya Maadili kutokana na mienendo yake katika shauri hilo, Jaji amesema kuwa hajapokea taarifa yoyote kuhusu malalamiko hayo, wala hajui kilichoandikwa katika malalamiko hayo. Hivyo, amesema hawezi kujitoa kwa msingi huo.

Mheshimiwa Jaji Hamidu Mwanga amesema kuwa zipo sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya Jaji ajitoe kwenye kesi, ikiwemo kama itabainika ana chuki binafsi na upande wowote katika kesi husika, au ana uhusiano wa karibu na upande wowote kwenye shauri hilo. Hata hivyo, amesema kuwa ingawa Jaji anaweza kuamua kujitoa kwa hiari hata kama hakuna sababu za msingi, yeye binafsi ameamua kutokujitoa katika kesi hii.
 
Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza hoja za ombi la kutaka ajitoe kwenye Kesi Namba 8323/2025 iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Zanzibar Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu amesema kwamba anakataa kujitoa kama ombi lilivyowasilishwa kwa kuwa hakuna sababu za msingi.

Taarifa zaidi zinafuata...
Yaani haaminiki ila yeye ndio anaamua ajitoe ama la?
 
Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza hoja za ombi la kutaka ajitoe kwenye Kesi Namba 8323/2025 iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Zanzibar Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu amesema kwamba anakataa kujitoa kama ombi lilivyowasilishwa kwa kuwa hakuna sababu za msingi.

Taarifa zaidi zinafuata...
ni kukata rufaa..............................INGAWA HII NI INTERLOCUTORY MATTER THAT DOES NOT DETERMINE THE FINALITY OF THE CASE
 

Attachments

Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza hoja za ombi la kutaka ajitoe kwenye Kesi Namba 8323/2025 iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Zanzibar Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu amesema kwamba anakataa kujitoa kama ombi lilivyowasilishwa kwa kuwa hakuna sababu za msingi.

Taarifa zaidi zinafuata...
Nature itaamua uondoke au vinginevyo! Mungu ni mkuu!
 
Yaani haaminiki ila yeye ndio anaamua ajitoe ama la?
Huyu Hamudu ni kati ya mashetani yaliyotumbukizwa kwenye mifumo mbalimbali ya kutoa haki huku yenyewe yakiwa ndiyo madhulumaji makuu ya haki.

Ni jambo lililotarajiwa. Kwa sababu hili jitu lilipelekwa NEC kwenye kudhulumu haki kwenye mchakato wa uchaguzi, sasa limepelekwa mahakamani kwenda kudhulumu haki za kimahakama. Na lenyewe linaona limefanikiwa sana, lakini halijui kesho yake. Haya madhulumaji haki siku zote huwa na miisho mibaya sana.

Mungu wa haki, mkono wako wa ukuu umfikie huyu mdhulumaji wa haki aliyeamua kumtumikia shetani kwa nguvu zake zote.
 
Bahati nzuri Malipo ni hapa hapa duniani.. Atalipia tu kwa namna moja au nyingine
Mimi sielewi vizuri mambo ya sheria bali concern yangu iko hapa, hivi alishindwa nini kukataa kujitoa siku ile ile ya kwanza mpaka ahahirishe maamuzi hadi baada ya week mbili!?
Ina maana akili/Kichwa alichyokuwa nayo siku ile ni tofauti na leo!?
Na kama ni yeye basi alikuwa anaenda kushauriana na nani, si angesema tu siku ile ile kuwa sijitoi!?

Tulidhani hii elimu ya mzungu ingetubadilisha walau na sisi tukawa binadamu na kupunguza kuwaza wanawake/wanaume na chakula tu, ila watu wamesoma hadi vyuo vikuu ajabu akili zao zimerudi miaka 1500 nyuma huku waliotuletea hii elimu wakiwaza kinachoendelea, sio kwenye sayari ya Mars bali galaxies zingine.
 
Back
Top Bottom