GE2025 Jaji Hamidu Mwanga akataa kujitoa kwenye kesi ya CHADEMA

GE2025 Jaji Hamidu Mwanga akataa kujitoa kwenye kesi ya CHADEMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwani kukaa pembeni shilingi ngapi?...
Huyu jamaa vipi?....kwani judge yupo peke yake?...
Anakomaa kwa manufaa ya nani?...
 
ni kukata rufaa..............................INGAWA HII NI INTERLOCUTORY MATTER THAT DOES NOT DETERMINE THE FINALITY OF THE CASE
How does it not determine the final ruling? Clash of interests ni serious matter kwa nature ya kesi. Pia inakuaje maombi ya jaji kuondolewa kwenye kesi apelekewe jaji mwenyewe? Kwani hakuna tume ya majaji au whatever ili maombi yapelekwe huko?

Au justice system is a scam
 
Mimi sielewi vizuri mambo ya sheria bali concern yangu iko hapa, hii alishindwa nini kukataa kujitoa siku ile ile ya kwanza mpaka ahahirishe maamuzi hadi baada ya week mbili!?
Ina maana akili/Kicchwa alichyokuwa nayo siku ile ni tofauti na leo!?
Na kama ni yeye basi alikuwa anaenda kushauriana na nani, si angesema tu siku ile ile kuwa sijitoi!?

Turidhani hii elimu ya mzungu ingetubadilisha walau na sisi tukawa binadamu na kupunguza kuwaza wanawake/wanaume na chakula tu, ila watu wamesoma hadi vyuo vikuu ajabu akili zao zimerudi miaka 1500 nyuma huku waliotuletea hii elimu wakiwaza kinachoendelea, sio kwenye sayari ya Mars bali galaxies zingine.
Mkuu, ukiona hivyo ujue kuna masilahi binafsi anatetea si bure
 
Jaji Hamidu Mwanga, anayesikiliza hoja za ombi la kutaka ajitoe kwenye Kesi Namba 8323/2025, iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Said Issa Mohammed, dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho, amesema kwamba anakataa kujitoa kama ilivyoombwa, kwa kuwa hakuna sababu za msingi zilizowasilishwa.

Akisoma uamuzi wa Mahakama, Jaji Mwanga amekataa hoja zote zilizowasilishwa na CHADEMA zikitaka ajitoe kwenye kesi hiyo.

Katika hoja ya kwanza, kuhusu uamuzi uliotolewa Juni 10, 2025 wa kuweka zuio la muda kwa CHADEMA kufanya shughuli za kiutendaji (siasa), jambo ambalo CHADEMA walipinga, Jaji amesema kuwa uamuzi wa Jaji katika shauri hauwezi kuwa sababu ya kumlazimu kujitoa. Ameeleza kuwa upo utaratibu mwingine wa kisheria iwapo kuna kutokubaliana na uamuzi wa Mahakama.

Kuhusu hoja inayomhusu Wakili Edison Kiratu, ambaye alidaiwa kuandika barua kwa niaba ya mmoja wa walalamikaji katika kesi hiyo ili ajitoe, pamoja na madai kuwa hakupata nafasi ya kusikilizwa na kwamba Jaji alitoa haki kwa upande mmoja, Jaji amesema kuwa hoja hiyo haina mashiko. Ameeleza kuwa Wakili Kiratu hajawahi kufika Mahakamani na hayupo kwenye rekodi za Mahakama katika shauri hilo. Aidha, ameongeza kuwa inaonekana alileta nyaraka na ‘kuziacha’ Mahakamani kisha kutoweka, jambo ambalo amesema halikubaliki kisheria.

Katika hoja nyingine iliyowasilishwa na CHADEMA, ambayo ilidai kuwa Jaji Mwanga aliwahi kuwa mtendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC, ambayo sasa ni INEC), hivyo hawezi kutoa uamuzi kutokana na rekodi za karibuni kati ya CHADEMA na Tume hiyo, Jaji amekataa hoja hiyo akieleza kuwa hilo haliwezi kuwa sababu ya msingi ya yeye kujitoa. Amesema kuwa NEC si sehemu ya shauri lililopo Mahakamani, na kwamba historia ya ajira katika Tume hiyo haiwezi kutumika kama msingi wa kujitoa kwake katika kesi hiyo.

Aidha, kuhusu hoja nyingine iliyowasilishwa na CHADEMA kwamba wamewasilisha malalamiko dhidi ya Jaji huyo kwenye Tume ya Maadili kutokana na mienendo yake katika shauri hilo, Jaji amesema kuwa hajapokea taarifa yoyote kuhusu malalamiko hayo, wala hajui kilichoandikwa katika malalamiko hayo. Hivyo, amesema hawezi kujitoa kwa msingi huo.

Mheshimiwa Jaji Hamidu Mwanga amesema kuwa zipo sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya Jaji ajitoe kwenye kesi, ikiwemo kama itabainika ana chuki binafsi na upande wowote katika kesi husika, au ana uhusiano wa karibu na upande wowote kwenye shauri hilo. Hata hivyo, amesema kuwa ingawa Jaji anaweza kuamua kujitoa kwa hiari hata kama hakuna sababu za msingi, yeye binafsi ameamua kutokujitoa katika kesi hii.
Mimi kama muislam zamani nishajitoa, maana ninapoenda baada ya kufa ni pagumu zaidi kuliko kitu chochote hapa duniani
 
Mkuu, ukiona hivyo ujue kuna masilahi binafsi anatetea si bure
Ni sawa, lakini hayo maslahi kweli yanapita hadhi ya mtu kufikia level ya ujaji!?
Ni heshima kubwa sana kimaadili kuwa judge, let us hope kwamba maslahi hayo ni ya kimaadili na si vyeo, nyumba, gari, mashamba, wanawake nk ambavyo hata ukiiweka kwenye malengo mwisho wake they all perish.
Angallia watu waliokuwa na nyumba Upanga, Ada Estate au Kapripoint miaka ya 80s, leo hii si wanaona 'wajanja' wanaamia Mbweni na kwingineko!? Je, kama ulinyang'anya haki ya mtu wakati huo na umejaaliwa kuishi hadi leo ukiiona jamii ya mtu huyo uliyempoteza unajisikiaje!?
 
Hii habari imenikumbsha mbali sana.
back then.. ndiyo nimeanza maisha ya ghetto,Kuna demu(mtu wa singida) mmoja kitaa nikawa ninafinya kishikaji.
one day nikamfuma eneo la hatari na mshikaji,akaniona nikamuona...nikaziua as if hakuna mbaya..mida flan narudi ghetto yule Malaya huyu hapa.. akaingia moja kwa moja Ngwea.
nikamwambia ajichenge..yule Malaya akasema"huwezi nifukuza hapa kwa kosa dogo kama ili".
zilipita sekunde kadhaa singer chochote baada ya jibu lile.
 
Chaumma haiwezi kuwa Chadema. Ila inawezekana kuwa kuna wanachama wa Chadema wanaweza kutimkia Chaumma ili wapate nafasi ya kugombea.

Mbowe hawezi kuhamia Chaumma kwa sababu itasababisha mgongano wa madaraka. Kinachoweza kutokea ni uongozi wa sasa kujiuzulu na hivyo kumpa nafasi ya kugombea uenyekiti. Ila sidhani kama atafanya hivyo maana kuna wanachama wengi wa Chadema watakaomkataa kwa imani kuwa ndie aliyesababisha uongozi ujiuzulu.

Amandla...
Hashim ameshasema Mbowe atakaporipoti tu Chaumma anamwachia Uenyekiti 😀
 
Back
Top Bottom