Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 22,981
- 47,826
Kaisari ni kiboko miaka hiyo ana hela ina picha yake..Pilato alitaka kujitoa wayahudi wakamtisha “ ukijitoa hautakuwa RAFIKI wa Kaisari”
Ilikuwa mwaka 0001 AC 😂 sasa ni 2025 AC

ataangamia yeye! na kuiacha CDMHuyo ana maagizo mahsusi toka kwa mamlaka ya uteuzi kuiangamiza Chadema hivyo hawezi kujitoa anaogopa kwenda kinyume na mamlaka ya uteuzi. Hapo Mbowe roho yake kwatuuuu !!View attachment 3421874
Unakuwa mbabaishaji kama Samia.Nazungumzia mambo hayo yalianza mwanzoni mwa kalenda
Ningetaka kuweka tarehe ya hukumu ingesomeka 0033 AC 😄✔️🇮🇱
Kweli labda ungekua na hiden cameraNi Risk Mkuu.
Mkubwa, it's year 1 AD (or as you call it 0001) and 2025 AD. Wewe hiyo AC umeitoa wapi?Kuijua 0001 ni lazima kwanza ujue unabii wa kuzaliwa Masihi wa Mungu wa mbinguni uliotolewa miaka 400 kabla 😄
History Form Two 😂😂🇹🇿Mkubwa, it's year 1 AD (or as you call it 0001) and 2025 AD. Wewe hiyo AC umeitoa wapi?
chadema huwa hawatumii akili ila mihemko na maguvu, na sometimes unaweza fikiri wanafanya makusudi au wanatumika. na it is very possible wanatumika kwa expense ya raia. kwa sababu, haiji akilini edison kilatu na mawakili mpo hapo, halafu anakuja mtu anasema hamidu mwanga aliwahi kuwa tume ya uchaguzi zanzibar; edson kilatu alikuwa mwaka mmoja nyuma ya hamidu mwanga pale udsm sheria, na mawakili wote wanajua hamidu kabla hajaenda tume ya uchaguzi hapa bongo alikuwa wakili wa serikali pale kwa DPP, kaendesha kesi kibao. unakuja leo unasema hamidu alikuwa zanzibar, hata research kidogo tu kuuliza mawakili wenzenu kwenye jopo hilohilo waliosoma naye na wengine wapo hadi kwenye magroup, majaji hao wengi tupo nao whatsapp huko mwanasheria yeyote akiteuliwa tunajua ametoka wapi na alikuwa wapi, tunao. kweli leo mtu aibuke kusema hamidu mwanga, huyo mpare wa same alikuwa zanzibar? really?Jaji Hamidu Mwanga, anayesikiliza hoja za ombi la kutaka ajitoe kwenye Kesi Namba 8323/2025, iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Said Issa Mohammed, dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho, amesema kwamba anakataa kujitoa kama ilivyoombwa, kwa kuwa hakuna sababu za msingi zilizowasilishwa.
Akisoma uamuzi wa Mahakama, Jaji Mwanga amekataa hoja zote zilizowasilishwa na CHADEMA zikitaka ajitoe kwenye kesi hiyo.
Katika hoja ya kwanza, kuhusu uamuzi uliotolewa Juni 10, 2025 wa kuweka zuio la muda kwa CHADEMA kufanya shughuli za kiutendaji (siasa), jambo ambalo CHADEMA walipinga, Jaji amesema kuwa uamuzi wa Jaji katika shauri hauwezi kuwa sababu ya kumlazimu kujitoa. Ameeleza kuwa upo utaratibu mwingine wa kisheria iwapo kuna kutokubaliana na uamuzi wa Mahakama.
Kuhusu hoja inayomhusu Wakili Edison Kiratu, ambaye alidaiwa kuandika barua kwa niaba ya mmoja wa walalamikaji katika kesi hiyo ili ajitoe, pamoja na madai kuwa hakupata nafasi ya kusikilizwa na kwamba Jaji alitoa haki kwa upande mmoja, Jaji amesema kuwa hoja hiyo haina mashiko. Ameeleza kuwa Wakili Kiratu hajawahi kufika Mahakamani na hayupo kwenye rekodi za Mahakama katika shauri hilo. Aidha, ameongeza kuwa inaonekana alileta nyaraka na ‘kuziacha’ Mahakamani kisha kutoweka, jambo ambalo amesema halikubaliki kisheria.
Katika hoja nyingine iliyowasilishwa na CHADEMA, ambayo ilidai kuwa Jaji Mwanga aliwahi kuwa mtendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC, ambayo sasa ni INEC), hivyo hawezi kutoa uamuzi kutokana na rekodi za karibuni kati ya CHADEMA na Tume hiyo, Jaji amekataa hoja hiyo akieleza kuwa hilo haliwezi kuwa sababu ya msingi ya yeye kujitoa. Amesema kuwa NEC si sehemu ya shauri lililopo Mahakamani, na kwamba historia ya ajira katika Tume hiyo haiwezi kutumika kama msingi wa kujitoa kwake katika kesi hiyo.
Aidha, kuhusu hoja nyingine iliyowasilishwa na CHADEMA kwamba wamewasilisha malalamiko dhidi ya Jaji huyo kwenye Tume ya Maadili kutokana na mienendo yake katika shauri hilo, Jaji amesema kuwa hajapokea taarifa yoyote kuhusu malalamiko hayo, wala hajui kilichoandikwa katika malalamiko hayo. Hivyo, amesema hawezi kujitoa kwa msingi huo.
Mheshimiwa Jaji Hamidu Mwanga amesema kuwa zipo sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya Jaji ajitoe kwenye kesi, ikiwemo kama itabainika ana chuki binafsi na upande wowote katika kesi husika, au ana uhusiano wa karibu na upande wowote kwenye shauri hilo. Hata hivyo, amesema kuwa ingawa Jaji anaweza kuamua kujitoa kwa hiari hata kama hakuna sababu za msingi, yeye binafsi ameamua kutokujitoa katika kesi hii.
Jaji Hamidu Mwanga, anayesikiliza hoja za ombi la kutaka ajitoe kwenye Kesi Namba 8323/2025, iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Said Issa Mohammed, dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho, amesema kwamba anakataa kujitoa kama ilivyoombwa, kwa kuwa hakuna sababu za msingi zilizowasilishwa.
Akisoma uamuzi wa Mahakama, Jaji Mwanga amekataa hoja zote zilizowasilishwa na CHADEMA zikitaka ajitoe kwenye kesi hiyo.
Katika hoja ya kwanza, kuhusu uamuzi uliotolewa Juni 10, 2025 wa kuweka zuio la muda kwa CHADEMA kufanya shughuli za kiutendaji (siasa), jambo ambalo CHADEMA walipinga, Jaji amesema kuwa uamuzi wa Jaji katika shauri hauwezi kuwa sababu ya kumlazimu kujitoa. Ameeleza kuwa upo utaratibu mwingine wa kisheria iwapo kuna kutokubaliana na uamuzi wa Mahakama.
Kuhusu hoja inayomhusu Wakili Edison Kiratu, ambaye alidaiwa kuandika barua kwa niaba ya mmoja wa walalamikaji katika kesi hiyo ili ajitoe, pamoja na madai kuwa hakupata nafasi ya kusikilizwa na kwamba Jaji alitoa haki kwa upande mmoja, Jaji amesema kuwa hoja hiyo haina mashiko. Ameeleza kuwa Wakili Kiratu hajawahi kufika Mahakamani na hayupo kwenye rekodi za Mahakama katika shauri hilo. Aidha, ameongeza kuwa inaonekana alileta nyaraka na ‘kuziacha’ Mahakamani kisha kutoweka, jambo ambalo amesema halikubaliki kisheria.
Katika hoja nyingine iliyowasilishwa na CHADEMA, ambayo ilidai kuwa Jaji Mwanga aliwahi kuwa mtendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC, ambayo sasa ni INEC), hivyo hawezi kutoa uamuzi kutokana na rekodi za karibuni kati ya CHADEMA na Tume hiyo, Jaji amekataa hoja hiyo akieleza kuwa hilo haliwezi kuwa sababu ya msingi ya yeye kujitoa. Amesema kuwa NEC si sehemu ya shauri lililopo Mahakamani, na kwamba historia ya ajira katika Tume hiyo haiwezi kutumika kama msingi wa kujitoa kwake katika kesi hiyo.
Aidha, kuhusu hoja nyingine iliyowasilishwa na CHADEMA kwamba wamewasilisha malalamiko dhidi ya Jaji huyo kwenye Tume ya Maadili kutokana na mienendo yake katika shauri hilo, Jaji amesema kuwa hajapokea taarifa yoyote kuhusu malalamiko hayo, wala hajui kilichoandikwa katika malalamiko hayo. Hivyo, amesema hawezi kujitoa kwa msingi huo.
Mheshimiwa Jaji Hamidu Mwanga amesema kuwa zipo sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya Jaji ajitoe kwenye kesi, ikiwemo kama itabainika ana chuki binafsi na upande wowote katika kesi husika, au ana uhusiano wa karibu na upande wowote kwenye shauri hilo. Hata hivyo, amesema kuwa ingawa Jaji anaweza kuamua kujitoa kwa hiari hata kama hakuna sababu za msingi, yeye binafsi ameamua kutokujitoa katika kesi hii.
15 April 2026
Dodoma, Tanzania
Mahakama ya Rufani Yarejesha Shughuli za Kisiasa za Chadema
![]()
Picha maktaba
Mahakama ya Rufani Kanda ya Dodoma, Aprili 15, 2026 imetengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyokizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya shughuli za Siasa nchini, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar), Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya chama hicho.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema taarifa zaidi kuhusu hatua hiyo itatolewa baadaye Saa 9:00 Alasiri