GE2025 Jaji Jacobs amesema Sheria 2 mpya zimeketa mabadiliko. Ila naona bado hazijakaa sawa

GE2025 Jaji Jacobs amesema Sheria 2 mpya zimeketa mabadiliko. Ila naona bado hazijakaa sawa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
IMG_8712.jpeg

​

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, amesema sheria mpya mbili za uchaguzi zimeanzisha mabadiliko muhimu, yakiwemo kuruhusu wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura ya Rais nje ya vituo vyao vya kawaida, pamoja na kuweka utaratibu wa uchaguzi katika maeneo yenye mgombea mmoja na magerezani.​

Akizungumza leo wakati wa kufunga mafunzo kwa waratibu, wasimamizi na wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo pamoja na maafisa manunuzi, Jaji Mwambegele amesema sheria hizo-Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani

Na. 1 ya 2024, na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya 2024-zinaleta mageuzi yasiyokuwepo hapo awali.

"Masuala haya mapya hayakuwapo katika sheria za zamani, hivyo hakuna mwenye uzoefu nayo. Ni jukumu lenu kuhakikisha mnaleta uelewa sahihi kwa vitendo," alisema Jaji Mwambegele.

Alisisitiza kuwa wahitimu hao sasa wana jukumu la kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa weledi na kuhakikisha uelewa wa sheria hizo mpya ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu yao ya usimamizi wa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom