Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Hilo tatizo wamejitengenezea wenyewe hao majaji, ni wao kwenye huo mhimili wenye tabia ya kufanya kazi ili kuwafurahisha wanasiasa, sasa inapotokea umetoa hukumu kinyume na matarajio ya boss wako unategemea kitu gani? akupongeze wewe servant wake?!
 
Kumbuka aliyefanya hivyo alikuwa kigogo wa serikali[emoji848]aliwaza mafao yake na penshen yake ya uzeen akaamua kutumia busara kuliacha lipite[emoji1787]he knows the court system is somehow fu.ck.e.d up[emoji1733]
Kaingiliwa uhuru wake badala ya kuchukua hatua wakati ule kuonyesha kuchukuzwa na jambo Hilo badala yake anakuja kutueleza Leo hii anapo staafu!!!!
Huu ni uoga na unafiki ambao haupaswi kuigwa.

Unafiki mtupu
 
Miaka 65!!!
nadhani wengi wao hawatambui umri wao wa kuzaliwa, ukiwatizama kwa sura zao wengi Wana umri mkubwa!!!
Nawashauri wangeomba kustaafu kwa hiari ili wapate muda wa kufanya kazi zao za kifamilia.
Miaka 55, 60, 65 ni umri mkubwa sana , ni vyema wakastaafu wakiwa na miaka 50.
Ukiwa na miaka 65 unaenda kufanya shughuli gani ya kifamilia?
 
Ukiwa na miaka 65 unaenda kufanya shughuli gani ya kifamilia?
Hakuna kazi wanayo weza kufanya maana miaka 65 ni Babu kwa hiyo ataenda kulala tu, ndio maana nimesema Majaji wanatakiwa kustaafu wakiwa ni umri wa miaka 50 ili wapate muda wa kufanya shughuli zao binafsi.
 
Hakuna kazi wanayo weza kufanya maana miaka 65 ni Babu kwa hiyo ataenda kulala tu, ndio maana nimesema Majaji wanatakiwa kustaafu wakiwa ni umri wa miaka 50 ili wapate muda wa kufanya shughuli zao binafsi.
Kwani mtu anapokua jaji hana shughuli binafsi? Wana heka heka nyingi tu na michepuko kama watu wengine
 
Huo upande
Jaji aliyemaliza muda wake wa kuitumikia Mahakama, Jaji John Mgeta amesema katika kazi yake ya utumishi kama Jaji hatasahau namna ambavyo kigogo wa Serikali alichana hukumu mbele yake.

Jaji Mgeta ameyasema hayo leo Mei 4, 2023 muda mfupi baada ya hafla ya kuagwa yeye na majaji wengine wawili iliyofanyika Mahakama Kuu Kanda Masjala ya Dar es Salaam.

Jaji Mgeta amelitaja tukio hilo kama moja hya changamoto kubwa aliyowahi kukutana nayo katika utendaji wake.

“Miongoni mwa changamoto nilizokutana nazo ni kusimamia kesi ya aliyekuwa kigogo wa Serikali na kushindwa kesi kwa kigogo huyo. Katika shauri hilo kigogo wa serikali alishindwa kesi lakini nilipopeleka maamuzi ya mahakama aliyadharau na kuamua kuchana karatasi ya hukumu, kitendo hiki kiliniumiza sana na nilikosa furaha, lakini nashukuru baadae serikali ilisimama na kutekeleza kile kilichoagizwa na mahakama,”amesema Jaji Mgeta.

Awali, akizungumza katika hafla ya kuwaaga majaji hao, Jaji Kiongozi Mustapha Siyani amesema wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi na mahakama kwani ni huru na inatoa haki.

Jaji Siyani amewataja majaji hao waliomaliza muda wao wa utumishi kuwa ni Jaji Sekela Moshi, Jaji Beatrice Mtungi na Jaji John Mgeta ambapo amesema kuwa kipindi chote cha kazi kwa majaji hao walikuwa wanafanya kazi kwa weledi.

Amesema mbali na kuchapa kazi pia waliomaliza muda wao na wenye utii kwa kila mtu na kwamba kuondoka kwao ni pengo.

“Wananchi wakikosa imani na mahakama kila mtu atachukua sheria mkononi, na nchi yoyote duniani lazima iwe na mahakama, hivyo tuna mahakama nchi nzima zipo kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi,” amesema Jaji Siyani.

Amesema kitendo cha kumaliza muda wao wa kazi kisheria ni alama tosha ya kuweza kuigwa kwa watumishi ili kuleta ufanisi katika kazi yao.

“Tunawakumbuka kwa bidii yenu ya kazi lakini na namna bora ya uongozi kwa kutatua kesi mbalimbali bila kujali ukubwa wake,” ameongeza Jaji Siyani.

Aidha, amesoma wasifu wa viongozi hao ambapo amesema wote walikuwa wamejaaliwa ujuzi katika kuandika hukumu pamoja hekima wanapokuwa na watu.

Chanzo: Mtanzania
HUo upande mmoja wa shilingi lakini kuna upande wake wa pili.

Huyo jaji alikuwa anamsaidia kiichinichini jamaa mmoja katika kesi yake na jamaa huyo katika kulipa fadhila akamteua mtoto wake wa kike kuingia katika bodi fulani kama mwakilishi wa hiyo taasisi binafsi hiyo taadisi ilikuwa inatakiwa kupendekeza jina moja lla mfanyabiahara ambaye ni memba wao. ili aingie katoka bodi ya taadisi ya serikali) Huyo binti yake hakuwa mfanyabiashara wala memba wa hiyo taasisi binafsi lakini aliingia katika bodi ya taasisi ya serikali kwa mgongo wa hiyo taasisi binafsi na kwa kupendekezwa na huyo swahiba aliyekuwa Rais wa hiyo taasisi binafsi.
 
Hivi vitu vinatokea Africa tu. Nchi zilizoendelea hata Rais au Waziri Mkuu akifanya hivyo atawajibishwa.
Tungepata na mifano ya nchi zingine Afrika. Vilevile ingekuwa vizuri sana Au hata mifano ya nchi zilizoendelea- ilipotokea Raisi au Waziri Mkuu kuchana hukumu halafu akawajibishwa! Kali sana hii
 
Jaji aliyemaliza muda wake wa kuitumikia Mahakama, Jaji John Mgeta amesema katika kazi yake ya utumishi kama Jaji hatasahau namna ambavyo kigogo wa Serikali alichana hukumu mbele yake...
Wacha wadharaulie tu sababu wao pia hawatendi haki kwa wananchi wa kawaida,pia hao ndo wanaokwamisha hata juhudi za kupata katiba mpya.

Tukiwaambia katika ndo tiba ya mambo yote hayo lkn wao huwa wanaiegemea mamlaka(serikali).
 
Kutokana na kauli ya Jaji huyu najifunza kitu kimoja kuwa kuna baadhi ya majaji sio waadilifu ndio maana Leo hii tunamshudia huyu Jaji mugeta akimtuhumu kiongozi wa juu kabisaa kwa dharau.

Hii inaonyesha kuna Majaji wengi hawana maadili na kuwatusi na kuwatuhumu viongozi wa juu bila hata aibu!!!!

Leo anatuhumiwa waziri Mkuu kesho watamtuhumu kwa dharau Rais!!!! Tuwe makini na baadhi ya Majaji ni Vimeo, hawafai.
 
Nauliza, Je Jaji mstaafu Mugeta kumtuhumu Waziri Mkuu mstaafu kwa kuchana hukumu mbele yake Je maneno hayo dhidi ya kiongozi Mkuu ni ukosefu wa maadili au Nini hiki?

Tuangalie vizuri mienendo ya Majaji kwa maoni yangu sio busara kumtuhumu kiongozi wa juu kama waziri Mkuu!!!

Tukiachia tabia hii kesho utasikia anatuhumiwa Makamu wa Rais siku nyingine Rais, huu ni utovu wa nidhamu ulio jificha kwenye mwamvuli wa kustaafu.

Unafiki na uzandiki ndio umewatawala vichwani mwao.
 
Hakuna kazi wanayo weza kufanya maana miaka 65 ni Babu kwa hiyo ataenda kulala tu, ndio maana nimesema Majaji wanatakiwa kustaafu wakiwa ni umri wa miaka 50 ili wapate muda wa kufanya shughuli zao binafsi.
Screenshot_20230505-084335_Google.jpg


Huyo hapo, ana miaka 86 and still in the office.
 
Jaji Mgeta ni mkwe wa mchungaji Rwakatare rip

Kwa sasa mkewe ndiye Askofu wa Mikocheni Assemblesy of God

Jamaa kapitia magumu mengi sana!

Magumu yake hayatuhusu, hakuna binadamu dunia hii hapitii magumu, hii ni lugha dhaifu na mtu dhaifu ndio hutaja taja magumu yake to public, hata Yesu kapitia magumu kuliko mwanadamu yeyote.

Magumu ni kwa kila binadamu, hatutaki mtu atutangazie magumu yake, akae nayo sbb kila mmoja ana magumu yake, tukianza kutangaziana hatutamaliza.
 
Back
Top Bottom