Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Huyu kigogo atakuwa nani?,hebu wajuzi ingieni chimbo mtujuze.

Tusisubiri kutafuniwa kila kitu, jaji mstaafu ametoa hint ni kigogo wa serikali .

Tanzania toka tupate uhuru imeongozwa na vigogo wa serikali ya CCM na mawaziri wakuu wastaafu wanahesabika na pia wote ni wanasiasa wa chama CCM.

Mahakama ina database ya wazi ya hukumu zake dhidi ya Kigogo wa serikali / waziri mkuu.

TanzLII ni tovuti ya Mahakama ya Tanzania inayochapisha maamuzi:
 
Hayo maswali yote uliyo yauliza hayana maana kwa wakati huu.

Yalikuwa maswali ya msingi wakati tukio lilipo tokea tu sio sasa.

Jaji alikuwa na malaka ya kisheria ya kuchukua hatua lkn akashindwa kuyatumia!! na kuachilia uhuru wake kuingiliwa na kudharauliwa kama ni kweli!!!! Hii ni stori ya kipuuzi kabisa na inalengo la kumdhalilisha kiongozi aliye tuhumiwa.

Kama alishindwa kuchukua hatua kipindi kile basi ni Bora angeendelea kukaa kimya kuliko alivyo onyesha udhaifu wake leo hii!!!!
Kosa haliachi kuwa kosa kwa kuwa limetendeka muda mrefu uliopita. Ni kweli kwa sasa masimlizi ya jaji ni stori tu yaweza semwa haina maana.

Lakini kama jamii hatupati lolote la kujifunza kupitia stori hiyo kwa maoni yako isiyo maana ?

Ni wazi kuwa kama kweli tukio lilitokea, huyo Waziri Mkuu alichana akijua jaji hana cha kumfanya maana katiba imeipa serikai kuu na viongozi wake mamlaka ya karibiana na Mungu.. sasa wakati jamii ikitaka kubadiri/ kurekebisha katiba yake,hili haliwezi kuwa funzo kuwa mihilimili hii ina nguvu zinazopishana kwa umbali sanaa kiasi kwamba wanadharauriana?

Badala ya kuendelea kutukuza viongozi wa juu kama wanatuhumiwa,ipo haja ya kujua kama ni kweli tukio lilitokea? Na linarekebishwaje? Labda kama ni furaha yako kuona viongozi wa serikali wanakuwa kama miungu watu wasihojika

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Sisi humu JamiiForums kama wadau wa kulinda utawala wa sheria tunapiga kelele mahakama na majaji kutishiwa na kudharauliwa na wanasiasa waliolewa madaraka je wadau wengine kama Bunge, Vyama vya Wanasheria / Mawakili, NGOs za kuhakikisha utawala bora n.k wana kauli gani ?

04 May 2023

MDAU WA UTAWALA WA SHERIA, RAIS WA TLS (Tanganyika Law Society) ANA MAONI GANI JUU YA TUKIO HILI

Na Mary Gwera, Mahakama

Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani ameongoza sherehe ya kuwaaga kitaaluma Majaji watatu wastaafu wa Mahakama hiyo ambapo amesema kwamba, Mhimili huo utaendelea kusimamia haki katika utendaji kazi na kuwaomba wananchi kuendelea kuwa na imani na chombo hicho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 04 Mei, 2023 mara baada ya kuhitimisha zoezi la kuongoza sherehe hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, Mhe. Siyani amesema kuwa ni wajibu wa Majaji na watumishi wote wa Mahakama kuhakikisha kwamba wanaendelea kujenga imani ya wananchi dhidi ya Mahakama.

“Wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi na Mahakama, hivyo niwakumbushe wananchi kuendelea kutumia Mahakama zote kuanzia ngazi ya Mahakama za Mwanzo hadi Mahakama ya Rufani kwakuwa ndipo haki inapopatikana,” amesema Jaji Kiongozi.

Mhe. Siyani amesema kwamba, wananchi wanapokosa imani kwa Mahakama maana yake hawatatumia chombo hicho na hivyo kutakuwa na ongezeko la vitendo vya uhalifu vitakavyohatarisha amani ya nchi.

Akizungumzia kustaafu kwa Majaji hao ambao ni Mhe. Beatrice Rhoda Mutungi, Mhe. Sekela Cyril Moshi na Mhe. John Mgetta, Jaji Kiongozi amesema kuwa watakumbukwa kwa uzoefu na umahiri wao katika kuendesha gurudumu la utoaji haki nchini.

“Kustaafu kwa Majaji hawa waliokuwa na uzoefu wa kutosha ni dhahiri kuwa kumeacha pengo, hivyo nitoe rai kwa Majaji wanaobaki kuchukua mazuri yote ambayo yameachwa na Majaji hawa ili kuendelea kuwahudumia vema wananchi,” ameeleza Mhe. Siyani.

Wakizungumza katika sherehe hiyo ya kitaaluma, Majaji wastaafu walioagwa wametoa rai kwa watumishi wa Mahakama kuimarisha ushirikiano katika kazi, kutokuwa na upendeleo, kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza matumizi ya TEHAMA.

Katika sherehe hiyo maalum ya kitaaluma Jaji Kiongozi aliongoza jopo lenye jumla ya Majaji 28 wa Mahakama Kuu na vilevile imehudhuriwa na pia baadhi ya watumishi na Viongozi wa Mahakama ambao ni pamoja na Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Martin Chuma. Kadhalika imehudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa Majaji wastaafu.

Wadau waliohudhuria katika sherehe hiyo ni pamoja na Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).

Zoezi la kuwaaga kitaaluma Majaji wastaafu linafanyika kwa mujibu wa Waraka Na. 1 wa Mwaka 2006 wa Jaji Mkuu.
Source : https://www.judiciary.go.tz/web/index.php?r=posts/webview&id=2260
 
Kitendo cha Jaji kuchaniwa hukumu na kutulia nalo moyoni hadi leo...

Inaonesha bado kuna tatizo mahali...
 
Jaji Kiongozi anaongea kuhusu uhuru wa mahakama lakini nadhiri inamsuta kuwa anaongea uongo

MAJAJI WATATU WA MAHAKAMA KUU WALIOAGWA WATOA USHAURI MUHIMU

04-05-2023 0

Na Magreth Kinabo- Mahakama
Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo tarehe 4 Mei, 2023 wameaagwa kitaaluma baada ya kustaafu utumishi wa Umma kwa kujibu wa sheria, huku wakisisitiza watumishi wa Mahakama kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano, weledi, uadilifu na upendo ili kuweza kutekeleza jukumu la utoaji haki na kulinda uhuru wa Mahakama.

Majaji hao ambao wamestaafu waliotoa kauli hizo kwa nyakati tofauti ni Mhe. Beatrice Mutungi, Mhe. John Mgeta na Mhe. Sekela Moshi.

Kwa pamoja wameishukuru Mahakama kwa ushirikiano walioupata katika utumishi wao na kuiacha Mahakama katika mikono salama.

Aidha, Majaji hao waliasa kwamba jukumu la utoaji haki linahitaji uvumilifu na muda wa kujitolea kwa kiwango cha juu.

Kwa upande wake, Jaji Mutungi, ambaye amekuwa mtumishi kwa Mahakama kwa miaka 33 amehudumu katika ngazi mbalimbali, ikiwemo Hakimu Mkazi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika Kanda tofauti, zikiwemo Songea, Moshi na Dar es Salaaam.

Alisema mbali na kufanya kazi kwa kuzingatia mambo mbalimbali, uwezo wa kutoa hukumu na maamuzi mbalimbali umechangiwa na kuwa chini ya viongozi waelekezi na kupata mafunzo ya kitaaluma ndani na nje ya nchi.

“Haki isitendeke tu bali ionekane wazi na bila shaka inatendeka. Maana ya msemo huu ilinipasa kusikiliza kwa umakini ushahidi wote ulioletwa na pande zote katika mashauri, kusoma na kufanya utafiti ili niweze kufikia maamuzi yasiyokuwa na upendeleo. Rai yangu kulingana na ukuaji wa sayansi na teknolojia mambo mengi yanabadilika. Hapa nalenga kuwaasa kuwa Mahakama Mtandao ipewe kipaumbele,” alisema na kusisitiza watumishi kupatiwa semina na mafunzo.

Akimzungumzia Jaji Mutungi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, Mhe. Juliana Masabo alisema anastahili kuigwa kwa uongozi wake mahiri, kuimarisha maadili ya watumishi na kuwasaidia watumishi na wadau katika kutatua malalamiko.

Kwa upande wake, Jaji Moshi ambaye amehudumu katika Mahakama kwa muda wa miaka 33 aliwasisitiza Mawakili wa Serikali na wale wa kujtegemea kuzingatia shajara zao ili kuepusha mashauri mengi kwa wakati mmoja.

Kadhalika, aliwaasa Mahakimu na Majaji kufanya ukaguzi katika masjala za Mahakama. Aliongeza kuwa kazi ya ujaji ni ngumu inahitaji muda wa ziada ya saa za kazi.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masajala Kuu, Mhe. Leila Mgonya, akimzungumzia Jaji Moshi alisema atakumbukwa kwa uongozi mahiri na mwepesi wa kuchukua hatua, usimamizi wa rasilimali watu, maono na ubunifu.

Naye Jaji Mgetta ambaye amehudumu katika Mahakama kwa kipindi cha miaka 32 ameshika nafasi mbalimbali kutoka Hakimu Mkazi na kuendelea kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu. Alipata kozi mbalimbali fupi ndani na nje ya nchi ambazo zilimsaidia kupata uzoefu, ikiwemo kuongeza thamani katika kazi yake.

“Ni muhimu kuzingatia utawala wa sheria na wakati huo huo unasimamia haki za wananchi kwa mantiki hiyo kunahitajika uharaka katika kutoa maamuzi na umakini wa ziada katika maudhui ya maamuzi hayo kwa kuhakikisha yanakuwa sahihi,” alisema.

Jaji Mgetta alisema mabadiliko ya sayansi na teknolojia yatumike vizuri ili kuhakikisha muda wa kusikiliza mashauri unapungua na imani ya wananchi juu ya Mahakama inaongezeka.

Akimzunguzia Jaji Mgetta, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Moses Mzuna alisena ni jasiri, alilinda taswira ya taaluma, mwanadiplomasia, mkweli, myenyenyekevu na mwenye bidii.

Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. Mark Mulambo alisema Majaji hao wana mchango mkubwa katika tasnia ya sheria kutokana na maamuzi waliyoyatoa.

Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Gloria Kalabamu aliwapongeza Majaji hao na kuahidi kuwa TLS itaendelea kushiriana nao katika kupata ushauri, usaidizi katika tafiti na uzoefu.
Source : https://www.judiciary.go.tz/web/index.php?r=posts/webview&id=2262
 
Itasaidia Nini kwa sasa?!
alitakiwa asema jambo hilo wakati uleule angeonekana jasiri na mwenye msimamo madhubuti kuliko kusema sasa.

alionyesha udhaifu mkubwa sana kwa kutokuchukua hatua kipindi like na akabaki na maumivu Hadi Leo!!!!!!

anawafumdisha nidhamu ya uoga, kwamba ukifanyiwa jambo baya usiseme usubirie Hadi siku ya kustaafu ndipo uelezee kama stori!!!!!!!

Tukisema mahakama haziko huru huwa mnatokwa na mishipa kuwa ziko huru. Sasa kama hukumu imechanwa na hakuna lolote kafanywa aliyeichana, huwa mnataka wapinzani waende mahakamani kufuata nini? Hata hii kesi ya Covid 19 ni muendelezo huohuo wa udhaifu wa mahakama.
 
Kaingiliwa uhuru wake badala ya kuchukua hatua wakati ule kuonyesha kuchukuzwa na jambo Hilo badala yake anakuja kutueleza Leo hii anapo staafu!!!!
Huu ni uoga na unafiki ambao haupaswi kuigwa.

Unafiki mtupu
Mi kuna Mwenyekiti wa Baraza la aridhi na Nyumba la Wilaya alizarau hukumu ya Mahakama Kuu,nimemchapa na barua ya malalamiko kwa Msajili,bado nasubiria majibu!!
 
MAJAJI WATATU WA MAHAKAMA KUU WALIOAGWA WATOA USHAURI MUHIMU

04-05-2023 0

Na Magreth Kinabo- Mahakama
Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo tarehe 4 Mei, 2023 wameaagwa kitaaluma baada ya kustaafu utumishi wa Umma kwa kujibu wa sheria, huku wakisisitiza watumishi wa Mahakama kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano, weledi, uadilifu na upendo ili kuweza kutekeleza jukumu la utoaji haki na kulinda uhuru wa Mahakama.

Majaji hao ambao wamestaafu waliotoa kauli hizo kwa nyakati tofauti ni Mhe. Beatrice Mutungi, Mhe. John Mgeta na Mhe. Sekela Moshi.

Kwa pamoja wameishukuru Mahakama kwa ushirikiano walioupata katika utumishi wao na kuiacha Mahakama katika mikono salama.

Aidha, Majaji hao waliasa kwamba jukumu la utoaji haki linahitaji uvumilifu na muda wa kujitolea kwa kiwango cha juu.

Kwa upande wake, Jaji Mutungi, ambaye amekuwa mtumishi kwa Mahakama kwa miaka 33 amehudumu katika ngazi mbalimbali, ikiwemo Hakimu Mkazi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika Kanda tofauti, zikiwemo Songea, Moshi na Dar es Salaaam.

Alisema mbali na kufanya kazi kwa kuzingatia mambo mbalimbali, uwezo wa kutoa hukumu na maamuzi mbalimbali umechangiwa na kuwa chini ya viongozi waelekezi na kupata mafunzo ya kitaaluma ndani na nje ya nchi.

“Haki isitendeke tu bali ionekane wazi na bila shaka inatendeka. Maana ya msemo huu ilinipasa kusikiliza kwa umakini ushahidi wote ulioletwa na pande zote katika mashauri, kusoma na kufanya utafiti ili niweze kufikia maamuzi yasiyokuwa na upendeleo. Rai yangu kulingana na ukuaji wa sayansi na teknolojia mambo mengi yanabadilika. Hapa nalenga kuwaasa kuwa Mahakama Mtandao ipewe kipaumbele,” alisema na kusisitiza watumishi kupatiwa semina na mafunzo.

Akimzungumzia Jaji Mutungi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, Mhe. Juliana Masabo alisema anastahili kuigwa kwa uongozi wake mahiri, kuimarisha maadili ya watumishi na kuwasaidia watumishi na wadau katika kutatua malalamiko.

Kwa upande wake, Jaji Moshi ambaye amehudumu katika Mahakama kwa muda wa miaka 33 aliwasisitiza Mawakili wa Serikali na wale wa kujtegemea kuzingatia shajara zao ili kuepusha mashauri mengi kwa wakati mmoja.

Kadhalika, aliwaasa Mahakimu na Majaji kufanya ukaguzi katika masjala za Mahakama. Aliongeza kuwa kazi ya ujaji ni ngumu inahitaji muda wa ziada ya saa za kazi.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masajala Kuu, Mhe. Leila Mgonya, akimzungumzia Jaji Moshi alisema atakumbukwa kwa uongozi mahiri na mwepesi wa kuchukua hatua, usimamizi wa rasilimali watu, maono na ubunifu.

Naye Jaji Mgetta ambaye amehudumu katika Mahakama kwa kipindi cha miaka 32 ameshika nafasi mbalimbali kutoka Hakimu Mkazi na kuendelea kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu. Alipata kozi mbalimbali fupi ndani na nje ya nchi ambazo zilimsaidia kupata uzoefu, ikiwemo kuongeza thamani katika kazi yake.

“Ni muhimu kuzingatia utawala wa sheria na wakati huo huo unasimamia haki za wananchi kwa mantiki hiyo kunahitajika uharaka katika kutoa maamuzi na umakini wa ziada katika maudhui ya maamuzi hayo kwa kuhakikisha yanakuwa sahihi,” alisema.

Jaji Mgetta alisema mabadiliko ya sayansi na teknolojia yatumike vizuri ili kuhakikisha muda wa kusikiliza mashauri unapungua na imani ya wananchi juu ya Mahakama inaongezeka.

Akimzunguzia Jaji Mgetta, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Moses Mzuna alisena ni jasiri, alilinda taswira ya taaluma, mwanadiplomasia, mkweli, myenyenyekevu na mwenye bidii.

Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. Mark Mulambo alisema Majaji hao wana mchango mkubwa katika tasnia ya sheria kutokana na maamuzi waliyoyatoa.

Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Gloria Kalabamu aliwapongeza Majaji hao na kuahidi kuwa TLS itaendelea kushiriana nao katika kupata ushauri, usaidizi katika tafiti na uzoefu.
Source : https://www.judiciary.go.tz/web/index.php?r=posts/webview&id=2262

Hizi porojo za kuhakikisha mashtaka yanasikilizwa kwa wakati ni porojo za miaka yote, na hakuna lolote linatekelezwa.
 
Si ajabu PM mwenyewe akawa mstaafu ndiyo maana kaweza kuliongea hili.

BTW:Watumishi wa mahakama hasa Hao majaji wakishavaa hayo magauni yao wanajiona "superhumans".

Huyo PM angemzaba hata vibao ni sawa tu.

Kuna karani wa mahakama aliatamia hundi yangu ya malipo kidogo imalize muda wake hadi nikatumia nguvu ya ziada.
 
Mi kuna Mwenyekiti wa Baraza la aridhi na Nyumba la Wilaya alizarau hukumu ya Mahakama Kuu,nimemchapa na barua ya malalamiko kwa Msajili,bado nasubiria majibu!!

Utapoteza muda tu kwa utaratibu huo, ni aidha uachane naye, au mtafutie jobless wammwagie tindikali.
 
Nauliza, Je Jaji mstaafu Mugeta kumtuhumu Waziri Mkuu mstaafu kwa kuchana hukumu mbele yake Je maneno hayo dhidi ya kiongozi Mkuu ni ukosefu wa maadili au Nini hiki?

Tuangalie vizuri mienendo ya Majaji kwa maoni yangu sio busara kumtuhumu kiongozi wa juu kama waziri Mkuu!!!

Tukiachia tabia hii kesho utasikia anatuhumiwa Makamu wa Rais siku nyingine Rais, huu ni utovu wa nidhamu ulio jificha kwenye mwamvuli wa kustaafu.

Unafiki na uzandiki ndio umewatawala vichwani mwao.
Umeandika Nini hebu soma Tena?
Unamaanisha kwamba Kama Hilo liliwahi kumtokea hakupaswa kulisema kwa kuwa Ni Waziri Mkuu aliyefanya hayo?

Kwanini usiseme kwamba Waziri Mkuu husika alikosa heshima juu ya mhimili wa Mahakama na tuwe na mfumo wa kuwapata viongozi waadilifu wanaoheshimu Mahakama pamoja na mihimili mingine ikiwemo Bunge?

Kwamba kuwa makamu wa Rais au Pm au Rais kunampa uhalali wa kudharau Mahakama?
 
Usiwe mgumu kuelewa,
Kwanini Jaji anatoa tuhuma hizi Leo hii akiwa anastaafu?! Kwanini anasema wakati huu kama kweli anayajua mamlaka yake?!!

Tuhuma anazo zitoa Leo hii zinapaswa zichukuliwe kama uzushi na zenye lengo la kuvunja heshima ya huyo aliye mtuhumu ambaye kwa sasa hawezi kujitetea.
Huu ni ukosefu wa maadili kwa Jaji
 
Mi kuna Mwenyekiti wa Baraza la aridhi na Nyumba la Wilaya alizarau hukumu ya Mahakama Kuu,nimemchapa na barua ya malalamiko kwa Msajili,bado nasubiria majibu!!
Hukumu ya mahakama kuu inaendaje Baraza la ardhi la wilaya?kesi zikishindikana kwenye mabaraza ya Ardhi ya wilaya na kata ndo zinaenda mahakamani,sasa hii yako mbona imekuwa vise versa 🤔Tena Kuna kiwango Cha thamani ya kiwanja/jengo ikizid hayo mabaraza yanakuwa hayana uwezo wa kushughulikia kesi ya namna hiyo🙏
 
Back
Top Bottom