Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Jaji wa aina hii inaonekana hata hukumu zake hazikuwa za Haki, mashaka matupu kama kweli alikuwa anatoa hukumu za haki!!!
Uzuri Hukumu zake zipo documented, unaweza kufungua hii link; Home | Tanzlii

Kasome hukumu zake halafu njoo hapa utuambie ni ngapi zilikatiwa RUFAA na matokeo yalikuwaje baada ya rufaa hizo
 
Ulitaka aseme wakati wa Magufuli halafu unajuwa kingefuata nini? Angeweza kutekwa, angeweza kufunguliwa kesi ya utakatishaji fedha au angeweza hata kuuliwa.

Naunga mkono msimamo wa Jaji Mgeta
Waziri Mkuu Lowassa alikuwa wakati wa Rais Magufuli!!? Naona una hasira na Magufuli sana mpaka unawashwa na mkund wako!!
 
Hukumu ya mahakama kuu inaendaje Baraza la ardhi la wilaya?kesi zikishindikana kwenye mabaraza ya Ardhi ya wilaya na kata ndo zinaenda mahakamani,sasa hii yako mbona imekuwa vise versa [emoji848]Tena Kuna kiwango Cha thamani ya kiwanja/jengo ikizid hayo mabaraza yanakuwa hayana uwezo wa kushughulikia kesi ya namna hiyo[emoji120]
Kesi ilianzia Baraza kabla haijafika Mahakama Kuu!
 
Nauliza, Je Jaji mstaafu Mugeta kumtuhumu Waziri Mkuu mstaafu kwa kuchana hukumu mbele yake Je maneno hayo dhidi ya kiongozi Mkuu ni ukosefu wa maadili au Nini hiki?

Tuangalie vizuri mienendo ya Majaji kwa maoni yangu sio busara kumtuhumu kiongozi wa juu kama waziri Mkuu!!!

Tukiachia tabia hii kesho utasikia anatuhumiwa Makamu wa Rais siku nyingine Rais, huu ni utovu wa nidhamu ulio jificha kwenye mwamvuli wa kustaafu.

Unafiki na uzandiki ndio umewatawala vichwani mwao.
Mzee acha kuabudu binadamu wezako hata kama kula yako inategemea uwepo wao
 
Hata simba, siyo jaji yule. Fikiria afisa wa TISSS anapokuwa msajili.wa mahakama. Yeye ndiye anayepanga kesi gani isikilizwe na jaji gani.
Anayepanga majaji wa kusikiliza kesi ni jaji mfawidhi wa mahakama husika, msajili kazi yake ni kuzipokea kesi na kuzisajili.
 
contempt of court ingemhusu
Hapana mkuu. Kuchana nakala ya hukumu sio kosa, maana haibatilishi hukumu. Nakala ya hukumu ni haki ya kila upande kwenye kesi, ukishapewa unaweza kuifanya chochote utakacho , hata kufungia maandazi au kuitumia chooni. Haitabadilisha chochote kilichoamuliwa na wala haitatengeneza kosa la jinai.
 
Ulitaka aseme wakati wa Magufuli halafu unajuwa kingefuata nini? Angeweza kutekwa, angeweza kufunguliwa kesi ya utakatishaji fedha au angeweza hata kuuliwa.

Naunga mkono msimamo wa Jaji Mgeta
Wewe ni mpuuzi,jaji anasema ilichanwa na waziri mkuu mstaafu wewe unawaza Magufuli au unamimba ya Magufuli

USSR
 
JPM waziri mkuu alikuwa Kassim. Huyu siyo mtu wa hivyo. Itakuwa ni zile enzi za JK au Mkapa. Ndo kipindi tulikuwa na PMs wenye 'Nyodo.'
Ndio jaji kasema waziri mkuu mstaafu, nashangaa wajinga humu wanamuandama Kassim majaliwa,wawe wanasoma

USSR
 
Jambo la pili tujiulize,kama ni kweli alichana hiyo hukumu,ni jambo sahihi kwa kiongozi yoyote wa serikali kuchana hukumu kama hizo?

Jambo la tatu ni tujiulize,kuchana hiyo hukumu,kiongozi huyo aliidharau Mahakama kama mhimili au alimdharau Jaji husika? ( Maana tunaona aliyeumia ni jaji binafsi na wala siyo mahakama)
Mahakamani watu huwa wana nafasi mbili, kuwa mdai au kuwa mdaiwa. Nafasi hizo hazihusishi chochote kwenye kazi zao au vyeo vyao kisiasa serikalini. Hata Jaji mkuu anaweza kuwa mdaiwa na akatakiwa kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Upokeaji wa hukumu kwa wanaoshindwa kesi hutofautiana kwa kila mtu. Wengine hulia, wengine hukaa kimya bila kuongea chochote, wengine huondoka bila hata kumaliza mwisho wa hukumu nk Kuchana nakala ya hukumu ni aina mojawapo ya mapokeo ya hukumu, kila binadamu ana aina yake ya mapokeo. Mfano, huyo aliyeshindwa kesi mapokeo yake ni kuchana nakala ya hukumu, Na kuchanwa kwa nakala ya hukumu, mapokeo ya jaji ni kuona amedharauliwa.

Hata hivyo Jaji husoma hukumu na sio mtoa nakala za hukumu. Nakala za hukumu hutolewa masjala na makarani wa mahakama kwa kuwa huwa kuna rejista mdai/mdaiwa anapotakiwa kusaini kuonesha amechukua hukumu. Sijui Jaji aliona wapi hilo tukio la nakala kuchanwa.

Hata hivyo nakala inayozingatiwa ni ile halisi iliyopo kwenye faili la mahakama au tovuti. Kilichochanwa ni nakala ya hukumu, sio hukumu.
 
Majaji wengi nyoko sana, labda hujakutana nao in vis-a-vis meeting, wanajiona Miungu watu yaani, wanakera mno, pumbaf sana 😡
Hawajui kuwa wao ni kama wauza bidhaa dukani (wauza duka), wamekaa kusubiri wateja. Mteja anapokuja unamhudumia kama mfalme..ajabu wao wamejigeuza kuwa wafalme na sasa wanahubiri wananchi wawe na imani na mahakama. Imani ambayo wao wenyewe (majaji) wameivunja kwa wananchi.
 
Nauliza, Je Jaji mstaafu Mugeta kumtuhumu Waziri Mkuu mstaafu kwa kuchana hukumu mbele yake Je maneno hayo dhidi ya kiongozi Mkuu ni ukosefu wa maadili au Nini hiki?

Tuangalie vizuri mienendo ya Majaji kwa maoni yangu sio busara kumtuhumu kiongozi wa juu kama waziri Mkuu!!!

Tukiachia tabia hii kesho utasikia anatuhumiwa Makamu wa Rais siku nyingine Rais, huu ni utovu wa nidhamu ulio jificha kwenye mwamvuli wa kustaafu.

Unafiki na uzandiki ndio umewatawala vichwani mwao.
Kweli wewe hujielewi
 
Back
Top Bottom