Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Huyu atakuwa Edward Ngoyai Lowassa
 
contempt of court ni chochote unachofanya kuashiria dharau kwa Mahakama na Mamlaka yake…hata kucheka kwa ishara ya dharau au kuongea na simu wakati mashauri ya kimahakama yanaendelea yanaweza kukupelekea huko

kwa muktadha ulioongelewa na Jaji ni kuwa PM hiyo alichana hukumu kuashiria kuidharau na kuipuuza
 
contempt of court ni chochote unachofanya kuashiria dharau kwa Mahakama na Mamlaka yake…hata kucheka kwa ishara ya dharau au kuongea na simu wakati mashauri ya kimahakama yanaendelea yanaweza kukupelekea huko
Hapo sasa !!
 
Nadhani kizazi cha 1990 kinaamini miaka 50 ni mingi sana ! πŸ˜….
 
Hakuna kazi wanayo weza kufanya maana miaka 65 ni Babu kwa hiyo ataenda kulala tu, ndio maana nimesema Majaji wanatakiwa kustaafu wakiwa ni umri wa miaka 50 ili wapate muda wa kufanya shughuli zao binafsi.

Mmnh!

Miaka 65 sio uzee wa kuchoka !

Wengine unawakuta vijana wa makamo tu.

Kama afya ikiwa njema wanakuwa fit bila kuchoka.
 
Nimejiuliza sana hili swala la kuchanwa kwa hukumu kama lilivyoongelewa na Jaji Mgeta mpaka nikapata hisia kwamba kuna kitu hakipo sawa upande wake.

Nilikua nafuatilia michango ya watu ni9ne kama kuna alifanya observation katika maelezo ya huyo Jaji lakini sikuona hadi nilipokutana na comment hii yaki.

Kuchanwa kwa huku na mtu ambaye tena hakuwepo ofisini bali mapumzikoni lina tija gani ikiwa hatua nyingine zote za utekelezwaji wa huku ile zilifanyika?

Kuchanwa kwa ile hukumu kuliathiri vipi hukumu yenyewe au hadhi ya Mahakama?
Katika hili huyu Jaji ameleta cheap talk bila kupima athari zinazoweza kuletwa na hoja zake nyepesi kwa mtu wa nafasi yake.

Aina hii ya Majaji ni wale wenye mafungamano na wanasiasa wakitarajia kuoshi kwa huruma na favours za wanasiasa. Hawa ndiyo wanaoudhoofisha Mhimili wa Mahakama na kuufanya utukanike na uonekane usio huru.
 
Si angemoiga tu contempt of court, siku 7 ndani zingetosha ukichukulia haina right to be heard wala rufaa.
 
Majaji wengi nyoko sana, labda hujakutana nao in vis-a-vis meeting, wanajiona Miungu watu yaani, wanakera mno, pumbaf sana [emoji35]

Halafu hawa jamaa bana!

Yaani kwa miaka mingi wana jipendelea sana kimaslahi huenda kuliko watumishi wengine wote wa Umma.

Wakistaafu pension zao ni sawa na 80% ya Jaji wa cheo chake alichostafia.

Imagine! [emoji848][emoji848]
 
Mkuu, naungana nawe. Jaji aliyetoa taarifa inawezekana mlengo wake ulikuwa ni kuonesha muingiliano wa mihimili au kutoheshimiwa kwa muhimili wa mahakama dhidi ya mihimili mingine. Ila alichokizungumza kimeshindwa kuonesha hicho alichokuwa amekitarajia kukionesha.

Mikanganyiko kama hii haileti tija kwa jamii zaidi ya kupotosha. Mfano hapo, kwa alichokizungumza, ameua mara 100 imani ya wananchi kwa Mahakama kuliko angeisema habari hiyo kwa kuibeba mahakama, mfano angesema, "Nilichekeshwa na kitendo cha waziri mstaafu kuchana nakala ya hukumu niliyoandika kwa sababu tu haikumfurahisha. Sisi Mahakama hatupo kuwafurahisha watu, tupo kwa ajili ya kusaidia utoaji wa haki kwa wananchi. Na ndio maana hukumu ile iliyochanwa na waziri bado ilitekelezwa vilevile kama nilivyoitoa bila kujali kama inamuudhi au kumfurahisha mheshimiwa waziri". Maneno kama haya ndio yanayojenga imani ya wananchi na ndio ukweli /uhalisia.
 
Angeisema kwa namna ulivyoipendekeza hakika angeijengea Mahakama confidence kubwa sana ma wananchi wangeona namna Mahakama ilivyo huru na imara. Lakini yeye ameidunisha mbele ya wananchi halafu watu wanasifia tu.
 
Anasema anashukuru serikali ilisimama na kutekeleza hukumu ile, ni kama anasema kuwa hata utekelezaji wa hukumu unafanywa kama favour. Jaji ameidunisha sana mahakama. Pascal Mayalla
 
Anasema anashukuru serikali ilisimama na kutekeleza hukumu ile, ni kama anasema kuwa hata utekelezaji wa hukumu unafanywa kama favour. Jaji ameidunisha sana mahakama. Pascal Mayalla
Aina hii ya Judges ni useless pia ni tatizo kubwa sana kwa heshima, ustawi na nguvu ya mhimili wa Mahakama.
Anaishukuru serikali kutekeleza hukumu. Yaani ni sawa na kumshukuru mhukumiwa kwa kukubali kuhukumiwa. Angeweza hata kumshukuru jambazi kwa kukubali kutumikia hukumu ya kifungo.
Yeye haoni kuwa ule ulikuwa ni wajibu wa serikali bali ni hisani tu.

Huyu could be among the worse Judges down the history lane.
 
Anasema anashukuru serikali ilisimama na kutekeleza hukumu ile, ni kama anasema kuwa hata utekelezaji wa hukumu unafanywa kama favour. Jaji ameidunisha sana mahakama. Pascal Mayalla
Kwamba anashukuru kwa favour aliyoipata πŸ˜…πŸ˜… ! Lakini huenda hakuwa na maana hiyo ila ni tabia zetu wabongo unyenyekevu kwa kila kitu hata mtu akienda dukani kununua kitu huwa anasema Mangi naomba vocha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…