Jaji Mkuu: Hakuna mtu yeyote anatakiwa kumwingilia au kumpigia simu Hakimu ambaye kesi fulani ipo mbele yake

Swali: Ni nani humpigia hakimu simu?
simu nyingi huwa zinatoka juu, utasikia agizo kutoka juu
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema hakuna mtu yeyote anatakiwa kumwingilia au kumpigia simu Hakimu ambaye suala au kesi fulani ipo mbele yake akisisitiza, "Ukiona anakupigia simu ya aina hiyo mpeleke mbele ya Tume ya Utumishi wa Mahakama"

Ameeleza hayo katika Hafla ya kuapishwa Mahakimu Wakazi Wateule Jijini Dar es Salaam, na kuwataka walioapishwa kuepuka mitego ya kuzungumzia masuala ya Mahakama kwenye makundi ya WhatsApp
Vipi akipigiwa kutoka magogoni asitoe zamana itakuwaje?
 
Yeye mwenyewe mteuliwa tu hapoo,muulizeni kwanza akipigiwa na aliyemteua afanye mafekecheo flaniii na ni nje ya sheria,atagomaa?!

Mwambie akae tu kimyaa,hii nchi inaliwa wa wenye nchi.
Hapo sasa na hilo swali akikujibu naomba nishtue.
 
Bora hata kupigiwa simu,Wale jamaa ukiwa judge na wakaona unataka kutenda Haki hawakupigii hata simu,Bali unapandishwa cheo tu ghafla.

Majaji wa nchi ya Cuba Ni noma.

In most cases, kupandishwa cheo hakumaanishi kwamba kesi zote ambazo kwa wakati huo ziko mbele yako unaachana nazo. Kuna baadhi ya kesi utalazimika kuzimalizia katika wadhifa wako wa zamani. Kama ulikuwa hakimu (say, PRM) na sasa umekuwa judge, zile kesi itabidi uzimalizie kwa kofia ya PRM.
 
Huku Cuba nilipo, utaratibu Ni tofauti.
 
Tanzania haijawahi kupata Jaji Mkuu wa hovyo kabisa kama Prof. Ibrahim Juma ambaye alikuwa mwalimu wangu pale UDSM na kwa namna alivyokuwa mtu wa staha na mpole na mcheshi kiasi sikutarajia kumbe ana uwezo mdogo wa uongozi wa Mahakama kiasi hiki.

Toka ameteuliwa hii nafasi hajawahi kuitendea haki Kama majaji wakuu wengine waliopita kama Samatta, nk ukiacha majaji wa Mahakama za juu kama marehemu Mwalusanya J, Lugakingira J as he then was.

Ameishia kuwa Jaji Mkuu wa matamko tu Kama mwanasiasa. Ameharibu sana muundo wa seniority kwenye Mahakama na staff ikiwemo muundo wa mawakili, practice, seniority, uchaguzi wa TLS, namna ya ushiriki nk.

Ameishushia Mahakama hadhi yake kwa kuruhusu kuendeshwa kwa kesi zenye utata wa kisheria na kiutendaji pia kesi za uhujumi uchumi ambazo zilikataza dhamana kwa watuhumiwa ingali anafahamu kabisa kwamba right to bail ni haki ya msingi katika utekelezaji wa haki ya mtu binafsi na dhana nzima ya innocence before the court.

Hajawahi kukemea na kuzitamka Sheria kandamini kwamba zipo kinyume na Katiba ya nchi. Amezipokea Sheria kama ya vyombo vya habari, Sheria ya mitandao, Sheria ya uhujumu uchumi, Sheria ya terrorism, na Sheria nyingine nyingi ambazo zipo kinyume na Katiba yetu.

Magufuli alimteua akijua kabisa huyu hajakulipa kwenye judiciary alikuwa lecturer tu hana ethics za uhakimu au judiciary.

Majaji wakuu waliokulia kwenye judiciary Wana sifa ya kutoendeshwa na serikali kuu (executive). Wamekuwa wakikemea sheria mbovu zinazotungwa bungeni na wamekuwa wakizikataa kuzitumia Mahakamani kwa kuwa zilikuwa kinyume na Katiba Ila huyu aliyepo yeye ni matamko ya jukwaani na sio akiwa functus officio.

Ndio maana judiciary imekuwa jalala la lawama za ukandamizaji wa haki ingali mwarobaini wake anaufahamu huyu Shemeji yake Mzee Shimbo.
Ni takataka tupu, nadhani amehitimu madrasat Quba
 
Sijui huyu Jaji ana maana gani!
Sijui yeye ni mara ngapi ameona haya yakitendeka na alikaa kimya!
Kwanini anasema sasa wakati huko nyuma alikaa kimya na huenda alitumika!
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema hakuna mtu yeyote anatakiwa kumwingilia au kumpigia simu Hakimu ambaye suala au kesi fulani ipo mbele yake akisisitiza, "Ukiona anakupigia simu ya aina hiyo mpeleke mbele ya Tume ya Utumishi wa Mahakama"

Ameeleza hayo katika Hafla ya kuapishwa Mahakimu Wakazi Wateule Jijini Dar es Salaam, na kuwataka walioapishwa kuepuka mitego ya kuzungumzia masuala ya Mahakama kwenye makundi ya WhatsApp
muwawekee na ulinzi hasa majumbani.
 
Tanzania haijawahi kupata Jaji Mkuu wa hovyo kabisa kama Prof. Ibrahim Juma ambaye alikuwa mwalimu wangu pale UDSM na kwa namna alivyokuwa mtu wa staha na mpole na mcheshi kiasi sikutarajia kumbe ana uwezo mdogo wa uongozi wa Mahakama kiasi hiki.

Toka ameteuliwa hii nafasi hajawahi kuitendea haki Kama majaji wakuu wengine waliopita kama Samatta, nk ukiacha majaji wa Mahakama za juu kama marehemu Mwalusanya J, Lugakingira J as he then was.

Ameishia kuwa Jaji Mkuu wa matamko tu Kama mwanasiasa. Ameharibu sana muundo wa seniority kwenye Mahakama na staff ikiwemo muundo wa mawakili, practice, seniority, uchaguzi wa TLS, namna ya ushiriki nk.

Ameishushia Mahakama hadhi yake kwa kuruhusu kuendeshwa kwa kesi zenye utata wa kisheria na kiutendaji pia kesi za uhujumi uchumi ambazo zilikataza dhamana kwa watuhumiwa ingali anafahamu kabisa kwamba right to bail ni haki ya msingi katika utekelezaji wa haki ya mtu binafsi na dhana nzima ya innocence before the court.

Hajawahi kukemea na kuzitamka Sheria kandamini kwamba zipo kinyume na Katiba ya nchi. Amezipokea Sheria kama ya vyombo vya habari, Sheria ya mitandao, Sheria ya uhujumu uchumi, Sheria ya terrorism, na Sheria nyingine nyingi ambazo zipo kinyume na Katiba yetu.

Magufuli alimteua akijua kabisa huyu hajakulipa kwenye judiciary alikuwa lecturer tu hana ethics za uhakimu au judiciary.

Majaji wakuu waliokulia kwenye judiciary Wana sifa ya kutoendeshwa na serikali kuu (executive). Wamekuwa wakikemea sheria mbovu zinazotungwa bungeni na wamekuwa wakizikataa kuzitumia Mahakamani kwa kuwa zilikuwa kinyume na Katiba Ila huyu aliyepo yeye ni matamko ya jukwaani na sio akiwa functus officio.

Ndio maana judiciary imekuwa jalala la lawama za ukandamizaji wa haki ingali mwarobaini wake anaufahamu huyu Shemeji yake Mzee Shimbo.
Stone alikuwa anatafuta watu wa dizaini hii.
 
Back
Top Bottom