Uchambuzi kamili toka gazeti la MWANAHALISI wa nini DPP amepanga kufanya kujaribu kuchelewesha maamuzi ya kesi ya Tundu Lissu
Kiuhalisia, DPP kwa makusudi kabisa anakiuka sheria ili kujaribu kuishawishi mahakama ipindishe sheria ili kumnyima haki ya uhuru Tundu Lissu
DPP ameamua kupitia mlango wa nyuma kwa kumwandikia barua Jaji mkuu aitishe faili la mwenendo wa kesi ya TL ili apitie upya (revision) maamuzi ya mambo mawili yaliyofanywa na mahakama kuu chini ya jopo la majaji wa3 wakiongozwa na Jaji Ndunguru:
MADAI YA DPP YA KUOMBA MAREJEO YA MAAMUZI YA HIGH COURT
1. Eti DPP haridhiki na kukataliwa kwa kielelezo cha ushahidi mkuu wa kesi hii (video yenye neno "tutakinukisha") toka JamboTV kwa kuwa kiliingizwa kinyume cha utaratibu wa kisheria
====DPP ANATAKA NINI?
====Anataka kielelezo hiki kirudishwe na kitumike kama ushahidi hata kama hakikidhi sifa za kisheria
2. Eti DPP anaishutumu na kuilalamikia mahakama kwa nini ikatae nyongeza ya ushahidi wa matukio ya 29/10 kutumika kama ushahidi dhidi ya kesi iliyoanza kusikikizwa miezi 6 au 7 nyuma.
Kumbukeni shahidi huyu Amini Mahamba alishawasilisha ushahidi wake wote huko ktk mahakama ya committal (Kisutu Resident Magistrate Court).
Sasa huyu Mahamba inasemekana kapata nyongeza ya ushahidi mpya ni ule wa matukio ya mauaji ya 29/10 na siku zilizofuata. Haieleweki wanataka yaingie ingie vipi kwenye shauri hili
Hata kama wewe si mwanasheria unaweza kung'amua mara moja kuwa haiwezekani ulete ushahidi wa tukio lililotokea baada ya mtuhumiwa kukamatwa na kufunguliwa mashitaka na kesi kuanza kusikilizwa huku mshitakiwa huyo akiwa under court custody!
====DPP ANATAKA NINI KWENYE HILI?
====Anataka mahakama ikiuke sheria, imruhusu Amini Mahamba aongeze ushahidi wake kinyume cha sheria inavyotaka!!
USHAURI WANGU KWA DPP NA SAMIA SULUHU HASSAN
1. Jaji mkuu Mh Masaju na majaji wako, tunzeni reputation yenu. Maisha ni mafupi mno. Wakiwalazimisha kupindisha sheria, jitoeni kusikiliza kesi, waachieni wengine watakaowaleta wao. Ndipo tutajua nini cha kufanya
2. Kubalini ukweli kuwa 29/10 na siku zilizofuata serikali kupitia vyombo vyake vya dola polisi, TISS, KIMKM nk ndizo zilizoua watu kwa amri ya Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vyote - Samia S. Hassan
3. Kubalini kuwa hesabu zenu za kuutengeneza uongo wa kesi hii ulikuwa mbovu na hovyo kwelikweli.
======Hebu jaribu kufikiri, eti serikali inatumia neno "tutakinukisha" lililotamkwa na mtu kuua wananchi maelfu kwa maelfu. Leo inapeleka hoja hiyo mahakamani kuwa tuliua kwa sababu huyu mtu alisema "tutakinukisha" na neno lake limetimia, HUYU NI MHAINI KWELIKWELI🤔🤔🤔🤔🫣🫣🫣🫣
4. Mkiukubali UKWELI huu kuwa nyie ni wajinga, hatua inayofuata TUBUNI pengine Mungu Muumba akawahurumia na kupunguza hukumu ya adhabu yenu. Out of that, you can't escape the karma..!
5. Hamna kesi hapo. Mnatumia mamlaka yenu vibaya (abuse of powers) kuonea na kutesa mtu wa HAKI, mtu asiye na hatia Tundu Lissu kwa makosa yenu. Hili halikubaliki na God of Heaven will never spare you!