Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema ufuatiliaji wa masuala ya Mahakama unaofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan haumaanishi kuingilia uhuru wa mhimili huo, bali unaonesha dhamira ya kushirikiana kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa haki nchini.
Pia, Soma: Spika Dkt. Tulia ashangazwa na wanaosherehekea uamuzi wa Mahakama viongozi kushtakiwa
Profesa Juma amesema hayo leo Jumapili, Juni 15, 2025 katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji George Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, iliyofanyika Ikulu jijini Dodoma.
"Sijawahi hata siku moja kukaa na Mheshimiwa Rais, Spika au Waziri Mkuu na kuzungumzia kesi hata siku moja. Kwanza sina hata majalada hapa. Tunazungumza mambo ya masilahi mapana ya Taifa," amesema Profesa Juma.