PreGE2025 Jaji Mutungi: Lissu na "no Reforms no Elections" hawajafanya kosa lolote kisheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Maneno mazito yake Jaji Mutungi Msajili wa vyama vya siasa ni mwiba mwingine kwa waliojibatiza utawala badala ya uongozi:

IMG_20250411_203954.jpg

---
Msajili wa vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi amesema kauli ya ‘No reform, no Election’ bado haijavunja sheria ya vyama vya siasa, huku akisisitiza kuwa uchaguzi mkuu 2025 uko palepale.

Jaji, Mutungi amesema wakati anazungumza na waandishi wa habari baada ya kushiriki warsha ya wadau wa kujadili namna ya kuzuia na kupambana na rushwa katika uchaguzi mkuu 2025.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi wa ndani, CHADEMA wamekuwa wakieleza kuwa, bila mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi hakutakuwa na uchaguzi mkuu mwaka 2025 na kwamba watauzuia kwa kuandamana nchi nzima kauli ambayo inapingwa na vyama vingine vya siasa ikiwemo CCM.

Msajili huyo amesema hakuna anayeweza kuzuia uchaguzi wa mwaka huu, kwakuwa kinachosemwa ni matamshi ya wanasiasa majukwaani ambayo kila chama kinaweza kuwa na maana yake.

“Hakuna awezaye kuzuia uchaguzi kwa kutamka tu kwenye majukwaa, CHADEMA hawajavunja sheria na nilipokutana nao hivi karibuni walisema hawatakuwa tayari kuvunja sheria za uchaguzi,” amesema Jaji Mutungi.

Aidha, amesema chombo kinachoweza kuzuia uchaguzi ni mahakama na hadi sasa hakuna aliyekwenda huko isipokuwa kinachoendelea ni matamshi ya midomoni mwa wanasiasa.

Amesema hajasikia kuwa CHADEMA wamekwenda mahakamani kupinga uchaguzi licha ya kuwa wanao wanasheria wanaojua utaratibu mzima wa nini kifanyike hivyo kinachoonekana ni kama wanafanya propaganda za kisiasa ambazo haziwezi kuwatia hatiani isipokuwa kama kutakuwa na maneno mengine ndani ya kauli zao.

“Mimi nitatafuta muda wa kuwaiteni kuzungumza kirefu zaidi kuhusu mambo haya, lakini kama ulivyosema mimi ndiye baba wa vyama vya siasa ni kweli, na kila chama kina haki ya kusikilizwa lakini siyo kuvunja sheria, sisi hatutegemei kama wanaweza kuvunja sheria,” amesema.

---

Pamoja na haya ya Jaji Mutungi, jingine la kujiuliza ni kuwa:

"hivi zile kesi za uhaini zikiwakabili kina Mwabukusi, Dk. Slaa, Mdude au Mwamba; ziliishia wapi?"

Kabla ya ule mwisho wenye lao jambo mbona, "ni kama bado wangali hawajasema?"

Ama hakika na watasema tu!

Source: Mwananchi.
 
Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza anena haya;

RESILIENCE ni USTAHIMILIVU

Kwenye 4R za Rais wetu, “R” moja inahusu USTAHIMILIVU yaani kwa Kijaluo, RESILIENCE. Kwa sasa marubani wetu wa nchi, niwasihi zimeni “R” zote, bakizeni RESILIENCE (Ustahimilivu).

Naelewa, msalani hatuendi na njaa bado inauma! Naelewa, ngedere wapo wanaocheka msitu ukiteketea na hivi punde giza litaingia hawatapata mahali pa kulala.

Bila USTAHIMILIVU tutakosea kama bado hatujakosea:

1. Yule pale kasingizia kuna Ebola na M-pox, akavumiliwa kwa sababu magonjwa hayo hayapo. Aliamka vibaya siku hiyo au alisahau kumeza dawa.

2. Huyu kakurupuka, “tutakinukisha na mashindano ya kujaza fomu hayatafanyika”. Mvumilie naye mlivyomvumilia yule. Kwani mashindano ya kujaza fomu yameishakwama? iAu mnahukumu nia? Wahukumuni wote basi.

3. Nimewasikia watu wanalaani uanaharakati. Wanautumia uanaharakati kulaani uanaharakati. Tukikosa ustahimilivu tutakosea. Kwa nini?

a. Huyu kadai reforms za kuondoa polisi katika shughuli za kisiasa. Polisi wamemkamata katika shughuli za kisiasa. Je kakosea? Polisi hawajampa point 3 za bure?

b. Anasema bila reforms hakuna uchaguzi. Wenzake (G55) wanasema twende kwenye uchaguzi. Kama polisi wameingilia kampeini, wataacha kuingilia uchaguzi?!

c. Wana Ijumaa walimaliza mfungo wao juzi ile. Wavaa majoho wakaonywa waache kihelehele, watulie wale sadaka zao kimya kimya. Wana Jumapili watafungua mfungo wiki ijayo. Hawa wavaa majoho wataacha kuwashwawashwa? Polisi wanayo magunzi ya kutosha kuwakuna wanapowashwa kufurahia “gaidi” aliyeuawa na polisi akafufuka siku ya tatu?!

4. Tuache kuchezea neno “uhaini”. Maneno yanaumba. Tusilizoee maana halizoeleki. Tafsiri zake zinatisha:

a. Kupindua serikali ni uhaini lakini tuna wahaini wengiii wanaongoza serikali Afrika na wanalaani uhaini.

b. Kuiba kura ni uhaini kwa sababu unapindua madaraka ya wananchi. Tunazo serikali nyingiiii barani Afrika zilizoiba kura na zinalaani wizi wa kura.

c. Kukalia kimya wizi wa kura, kuwezesha wizi wa kura, kukubali matokeo ya wizi wa kura ni uhaini. Uwiiiii, hata mimi ni mhaini maana nami nimo humu.

Jamani eh! Huu msimu na mwaka wa siasa. Tuvumiliane. Linaloshindikana, RUDI MEZANI. Kupigana mabomu ya kodi zetu wakati leo nimeenda hospitali nikakosa bandeji ya kufunga kidonda nilichopata jana nikikimbia mabomu, Siyo sawa.

“Bwana akawajibu, akasema, hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele” (siyo mabomu)
Luka 19:40.
 
Maneno mazito yake Jaji Mutungi Msajili wa vyama vya siasa ni mwiba mwingine kwa waliojibatiza utawala badala ya uongozi:

View attachment 3299737

Ndio maana nasema CCM wote na police wote hawanaga akili kabisa aiseeee. Trust me, hawa Jamaa ni mashetani
 
Maneno mazito yake Jaji Mutungi Msajili wa vyama vya siasa ni mwiba mwingine kwa waliojibatiza utawala badala ya uongozi:

View attachment 3299737

Pamoja na haya ya Jaji Mutungi, jingine la kujiuliza ni kuwa:

"hivi zile kesi za uhaini zikiwakabili kina Mwabukusi, Dk. Slaa, Mdude au Mwamba; ziliishia wapi?"

Kabla ya ule mwisho wenye lao jambo mbona, "ni kama bado wangali hawajasema?"

Ama hakika na watasema tu!

Source: Mwananchi.
Hajawahi kuwa na nia njema kwa Chadema na upinzani hivyo maneno yake huenda lengo ni kisema uchaguzi utafanyika hata kama kelele ni nyingi ama?
 
Hukumsikia Samia alivyoeleza matokeo ya alichokiita maridhiano
 
Hajawahi kuwa na nia njema kwa Chadema na upinzani hivyo maneno yake huenda lengo ni kisema uchaguzi utafanyika hata kama kelele ni nyingi ama?

Kutokuwa na nia njema ni kitu gani ndugu?

1744224725751.png

Vipi machadema miguuni pale, unadhani wao wanayo thamani ipi wapi kulinganisha na ukweli huu wa Mutungi?

Kwamba hata Pilato hakuwa na nia njema, so what ndugu?

Kulikoni kuwa na adui wa kudumu?
 
Maneno mazito yake Jaji Mutungi Msajili wa vyama vya siasa ni mwiba mwingine kwa waliojibatiza utawala badala ya uongozi:

View attachment 3299737

Pamoja na haya ya Jaji Mutungi, jingine la kujiuliza ni kuwa:

"hivi zile kesi za uhaini zikiwakabili kina Mwabukusi, Dk. Slaa, Mdude au Mwamba; ziliishia wapi?"

Kabla ya ule mwisho wenye lao jambo mbona, "ni kama bado wangali hawajasema?"

Ama hakika na watasema tu!

Source: Mwananchi (Gazeti la jana).
Nimeamua kuachana na mke wangu Ili niwe na soma mabandiko Yako mkuu bila buguza yyte
 
Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza anena haya;

RESILIENCE ni USTAHIMILIVU

Kwenye 4R za Rais wetu, “R” moja inahusu USTAHIMILIVU yaani kwa Kijaluo, RESILIENCE. Kwa sasa marubani wetu wa nchi, niwasihi zimeni “R” zote, bakizeni RESILIENCE (Ustahimilivu).

Naelewa, msalani hatuendi na njaa bado inauma! Naelewa, ngedere wapo wanaocheka msitu ukiteketea na hivi punde giza litaingia hawatapata mahali pa kulala.

Bila USTAHIMILIVU tutakosea kama bado hatujakosea:

1. Yule pale kasingizia kuna Ebola na M-pox, akavumiliwa kwa sababu magonjwa hayo hayapo. Aliamka vibaya siku hiyo au alisahau kumeza dawa.

2. Huyu kakurupuka, “tutakinukisha na mashindano ya kujaza fomu hayatafanyika”. Mvumilie naye mlivyomvumilia yule. Kwani mashindano ya kujaza fomu yameishakwama? iAu mnahukumu nia? Wahukumuni wote basi.

3. Nimewasikia watu wanalaani uanaharakati. Wanautumia uanaharakati kulaani uanaharakati. Tukikosa ustahimilivu tutakosea. Kwa nini?

a. Huyu kadai reforms za kuondoa polisi katika shughuli za kisiasa. Polisi wamemkamata katika shughuli za kisiasa. Je kakosea? Polisi hawajampa point 3 za bure?

b. Anasema bila reforms hakuna uchaguzi. Wenzake (G55) wanasema twende kwenye uchaguzi. Kama polisi wameingilia kampeini, wataacha kuingilia uchaguzi?!

c. Wana Ijumaa walimaliza mfungo wao juzi ile. Wavaa majoho wakaonywa waache kihelehele, watulie wale sadaka zao kimya kimya. Wana Jumapili watafungua mfungo wiki ijayo. Hawa wavaa majoho wataacha kuwashwawashwa? Polisi wanayo magunzi ya kutosha kuwakuna wanapowashwa kufurahia “gaidi” aliyeuawa na polisi akafufuka siku ya tatu?!

4. Tuache kuchezea neno “uhaini”. Maneno yanaumba. Tusilizoee maana halizoeleki. Tafsiri zake zinatisha:

a. Kupindua serikali ni uhaini lakini tuna wahaini wengiii wanaongoza serikali Afrika na wanalaani uhaini.

b. Kuiba kura ni uhaini kwa sababu unapindua madaraka ya wananchi. Tunazo serikali nyingiiii barani Afrika zilizoiba kura na zinalaani wizi wa kura.

c. Kukalia kimya wizi wa kura, kuwezesha wizi wa kura, kukubali matokeo ya wizi wa kura ni uhaini. Uwiiiii, hata mimi ni mhaini maana nami nimo humu.

Jamani eh! Huu msimu na mwaka wa siasa. Tuvumiliane. Linaloshindikana, RUDI MEZANI. Kupigana mabomu ya kodi zetu wakati leo nimeenda hospitali nikakosa bandeji ya kufunga kidonda nilichopata jana nikikimbia mabomu, Siyo sawa.

“Bwana akawajibu, akasema, hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele” (siyo mabomu)
Luka 19:40.

Uzuri ni kuwa Kila Figisu kwa Lissu au upinzani ni Fursa adhimu kwetu.

Kabla ya chakula kuwiva huchemka barabara kwanza!
 
Sa100 mabango kila sehemu nchini lakini bado hasomeki kudadek!

Mara bao la mama, champion wa komedi, sijui samia marathon...samia pikipiki, samia radio, kofia, vitenge, tshirt na ujinga mwingine kedekede

Kuna na Madaktari wa mama, msaada wa Sheria na wanasheria wa mama ..

Na yale mengine haya hapa yenye kububujikwa na machozi: Lucas Mwashambwa, Tlaatlaah Kwa lolote.

Bure kabisa!
 
Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza anena haya;

RESILIENCE ni USTAHIMILIVU

Kwenye 4R za Rais wetu, “R” moja inahusu USTAHIMILIVU yaani kwa Kijaluo, RESILIENCE. Kwa sasa marubani wetu wa nchi, niwasihi zimeni “R” zote, bakizeni RESILIENCE (Ustahimilivu).

Naelewa, msalani hatuendi na njaa bado inauma! Naelewa, ngedere wapo wanaocheka msitu ukiteketea na hivi punde giza litaingia hawatapata mahali pa kulala.

Bila USTAHIMILIVU tutakosea kama bado hatujakosea:

1. Yule pale kasingizia kuna Ebola na M-pox, akavumiliwa kwa sababu magonjwa hayo hayapo. Aliamka vibaya siku hiyo au alisahau kumeza dawa.

2. Huyu kakurupuka, “tutakinukisha na mashindano ya kujaza fomu hayatafanyika”. Mvumilie naye mlivyomvumilia yule. Kwani mashindano ya kujaza fomu yameishakwama? iAu mnahukumu nia? Wahukumuni wote basi.

3. Nimewasikia watu wanalaani uanaharakati. Wanautumia uanaharakati kulaani uanaharakati. Tukikosa ustahimilivu tutakosea. Kwa nini?

a. Huyu kadai reforms za kuondoa polisi katika shughuli za kisiasa. Polisi wamemkamata katika shughuli za kisiasa. Je kakosea? Polisi hawajampa point 3 za bure?

b. Anasema bila reforms hakuna uchaguzi. Wenzake (G55) wanasema twende kwenye uchaguzi. Kama polisi wameingilia kampeini, wataacha kuingilia uchaguzi?!

c. Wana Ijumaa walimaliza mfungo wao juzi ile. Wavaa majoho wakaonywa waache kihelehele, watulie wale sadaka zao kimya kimya. Wana Jumapili watafungua mfungo wiki ijayo. Hawa wavaa majoho wataacha kuwashwawashwa? Polisi wanayo magunzi ya kutosha kuwakuna wanapowashwa kufurahia “gaidi” aliyeuawa na polisi akafufuka siku ya tatu?!

4. Tuache kuchezea neno “uhaini”. Maneno yanaumba. Tusilizoee maana halizoeleki. Tafsiri zake zinatisha:

a. Kupindua serikali ni uhaini lakini tuna wahaini wengiii wanaongoza serikali Afrika na wanalaani uhaini.

b. Kuiba kura ni uhaini kwa sababu unapindua madaraka ya wananchi. Tunazo serikali nyingiiii barani Afrika zilizoiba kura na zinalaani wizi wa kura.

c. Kukalia kimya wizi wa kura, kuwezesha wizi wa kura, kukubali matokeo ya wizi wa kura ni uhaini. Uwiiiii, hata mimi ni mhaini maana nami nimo humu.

Jamani eh! Huu msimu na mwaka wa siasa. Tuvumiliane. Linaloshindikana, RUDI MEZANI. Kupigana mabomu ya kodi zetu wakati leo nimeenda hospitali nikakosa bandeji ya kufunga kidonda nilichopata jana nikikimbia mabomu, Siyo sawa.

“Bwana akawajibu, akasema, hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele” (siyo mabomu)
Luka 19:40.

"Au mnahukumu nia?"

Maneno mwiba sana haya kwa mkoloni mweusi.

imhotep au nasema uongo?
 
Back
Top Bottom