Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
“Sheria ya Uchaguzi Zanzibar inaeleza kuwa kuna Watu wanaruhusiwa kupiga kura mapema siku moja kabla ya Uchaguzi, wanaoruhusiwa kupiga kura ni wale ambao watakuwa na shughuli zinazohusu Uchaguzi siku ya Uchaguzi, mfano Askari, Watumishi wa Vyombo vya Usalama, Watumishi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, madaktari n.k.
“Upande wa Tanzania Bara Sheria hiyo haipo, hivyo suala hilo ni mahitaji ya Sheria na inatekelezwa.”
Jaji Mwambegele amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni kuhusu Uchaguzi Mkuu 2025, leo Agosti 3, 2025 kwenye Ukumbi wa Mkutano Mlimani City Jijini Dar es Salaam.