Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele anafafanua kuhusu Kura ya Mapema wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kusema:
“Sheria ya Uchaguzi Zanzibar inaeleza kuwa kuna Watu wanaruhusiwa kupiga kura mapema siku moja kabla ya Uchaguzi, wanaoruhusiwa kupiga kura ni wale ambao watakuwa na shughuli zinazohusu Uchaguzi siku ya Uchaguzi, mfano Askari, Watumishi wa Vyombo vya Usalama, Watumishi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, madaktari n.k.
“Upande wa Tanzania Bara Sheria hiyo haipo, hivyo suala hilo ni mahitaji ya Sheria na inatekelezwa.”
Jaji Mwambegele amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni kuhusu Uchaguzi Mkuu 2025, leo Agosti 3, 2025 kwenye Ukumbi wa Mkutano Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Kama sheria ingekuwa ni mtu huyu hapa ni Kinyesi chake. Mbona wanyakyusa ni watu makini sana hii takataka na Tulia zilitoka mapori gani mbona hamna kitu kichwani kabisa? Jitu limezubaa kama hili linakuwaje jaji sasa?