TANZIA Jaji Mwanaisha Kwariko, Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, afariki dunia

TANZIA Jaji Mwanaisha Kwariko, Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, afariki dunia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs C. Mwambegele, kwa masikitiko makubwa ametangaza kifo cha Mjumbe wa Tume hiyo, Mhe. Jaji Rufani Mwanaisha A. Kwariko, kilichotokea tarehe 27 Desemba, 2024, nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Tume, mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nchini kwa maandalizi ya mazishi, ambayo yamepangwa kufanyika kijijini kwao Bicha, wilayani Kondoa, mkoani Dodoma, tarehe 30 Desemba, 2024.
IMG_2073.jpeg
 
Apumzike kwa amani her honorable Judge Mwanaisha. Nyuma yake mbele yetu. Duniani ni mapito tu; mwendo kaumaliza ole ni wetu!
 
Mtu ambaye hajawahi kunitendea ubaya wowote, akifa huwa ninahuzunika sana.

R.I.P
 
Such is life, Kuna hatua na siku basi vyote viwili vikifika unakufa tu, sometimes si kwasababu ya uzee lah bali ni hivyo vitu viwili. Unakwenda kufukiwa ardhini, baada ya siku au wiki watu washasahau wanaendelea na mambo Yao kama kawaida.
 
Back
Top Bottom