Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs C. Mwambegele, kwa masikitiko makubwa ametangaza kifo cha Mjumbe wa Tume hiyo, Mhe. Jaji Rufani Mwanaisha A. Kwariko, kilichotokea tarehe 27 Desemba, 2024, nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Tume, mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nchini kwa maandalizi ya mazishi, ambayo yamepangwa kufanyika kijijini kwao Bicha, wilayani Kondoa, mkoani Dodoma, tarehe 30 Desemba, 2024.