Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Dunstan Ndunguru imekataa ombi la mshtakiwa Tundu Lissu la kuwaita baadhi ya mashahidi wa utetezi katika Kesi ya Uhaini Na. 19605/2025, ikieleza kuwa ushahidi wao hauna umuhimu kwani wajibu wa kuthibitisha kosa ni wa Jamhuri.
Hata hivyo, Jaji Ndunguru ameagiza kutolewa kwa wito rasmi (summons) kwa Mkuu wa Majeshi (CDF), Mkuu wa Polisi (IGP) na DCI ili wafike Mahakamani kutoa ushahidi upande wa utetezi. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 11, 2026
Fuatilia mwenendo wa Kesi ya Uhaini ya Lissu>> Heche: Nilikamatwa na Kusomewa Shtaka la Ugaidi la Kuchoma Vituo vya Mwendokasi Kimara hadi Magomeni
Uamuzi wa Mahakama Kuu
Jaji Ndunguru anaendelea kusoma uamuzi, anasema Mahakama imejiuliza endapo pingamizi ni la msingi.
Kifungu cha 281 cha CPA kinaeleza kuwa msajili atatoa summons kwa mashahidi waliotajwa wakati wa committal na tumeangalia ni kweli kwenye proceedings hakuna orodha ya mashahidi. Kutoorodheshwa mashahidi hakuwezi kutibiwa wakati wa usikilizwaji wa hoja za awali.
Tunakubaliana na upande wa mashtaka kwamba kutowataja mashahidi wakati wa committal hakutibiwi na kuwataja wakati wa usikilizwaji wa hoja za awali.
Kwa mujibu wa kifungu cha 314 cha CPA kinaipa Mahakama hiari ya kuruhusu mashahidi kuitwa kwa kuangalia umuhimu wa mashahidi hao.
Wakati mshtakiwa anasema anawataka hao mashahidi alisema anawataka waje waeleze kama walitishika au vinginevyo.
Katika kesi za jinai upande wa mashtaka ndio una wajibu wa kuthibitisha jinai na sio upande wa utetezi kuthibitisha utakatifu wake (innocence yake) hivyo Jamhuri ndio walikuwa na wajibu wa kuwaleta wao hao mashahidi kuja kuthibitisha na sio upande wa Jamhuri.
Mahakama inaona kwamba hakuna haja ya kuwaita mashahidi hao na ushahidi wao sio relevant katika kesi hii kwa upande wa utetezi.
Kuhusu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa aliyetoa ushahidi katika kesi ya Khatibu Ghandi aliitwa na Jamhuri na sio upande wa utetezi na ni msimamo wa kisheria kwamba kila kesi huamuliwa kutokana na mazingira yake.
Katika kesi ya Khatibu Ghandi Sheria hii ya sasa ya Usalama wa Taifa haikuwepo.
Mashahidi ambao hatujawagusa ni DCI, CDF na IGP wao tumeona ushahidi wao ni relevant, hivyo summons zitolewe ili waje kutoa ushahidi upande wa utetezi.