Jaji Rwegasira: Nimeagizwa na ngazi ya juu kuulinda mkataba wa LUGUMI

Jaji Rwegasira: Nimeagizwa na ngazi ya juu kuulinda mkataba wa LUGUMI

Kwahiyo PAC Wanatafuta Umaarufu. Kwahiyo Mh Magu anapotumbua majipu anatafuta umaarufu. Tafakari Fikirisha Kichwa Chako.
Huo uwezo wa kutafakari hana ndio maana amepost kitu kama hicho,kinacho muongoza ni kujaza tumbo tu
 
Nadhan mkataba unajulikana, " umesainiwa 2011 kusambasa vifaa vya alama za vidole katika vituo vya polis zaid ya 100, kwa jumla tsh billion 37"

Kama hataki uonyeshwe, basi ajibu maswali ya matumizi mabaya ya kodi za wananchi, kwanin zimeshatumika billion 34 kwa vituo 14 pekee..?!
We mgogo,tulia andika vizuri ndio upost siyo KUSAMBASA!!!! ni KUSAMBAZA
 
Mkuu, mimi kwa sasa nimeanza kujiuliza sana kuhusu hili suala.

Kuna uwezekano mkubwa tukawa tunacheza ngoma za watu bila kufahamu ajenda zake.
Kwa maana yako hutaki watu wachangie kwenye hii issue?
 
Safi kabisa katibu mkuu....kiukweli masuala ya jeshi hayafai kuanikwa .....ikumbukwe masuala ya jeshi si kama taasisi zingine za Mkonge....



polisi nalo ni jeshi wale ni RAIA WAKAKAMAVU.
 
Ni ile ile,wapuuzi endeleeni kupiga makofi!
Jk yupo ametulia anasikilizia tu,kweli kwa uozo kama huu wasinge kubali rasimu ya warioba ipitishwe hata kwa kutumia vifaru na wabunge wa ccm wakaingizwa chaka bila kujijua
 
We mgogo,tulia andika vizuri ndio upost siyo KUSAMBASA!!!! ni KUSAMBAZA
Duuh kweli babu ni KUSAMBAZA, Lakin na wewe siku nyingine utulie pia na uunganishe kiswahil chako vizur hapo " TULIA UANDIKE VIZURI sio TULIA ANDIKA VIZURI
 
Kipimo kizuri Sana kwa awamu ya tano.
Wakifunika kikombe Mwana haram apite then ntaichukulia serikali hii ya ki bongo movie sana,wala hata haijafikia serikali yenye kiwango cha maigizo Kama holly wood .
 
Huo ndio utaratibu issue za kiusalama sio kila mtu anapaswa kuziangalia na kujitafutia umaarufu kama hawa wajumbe wa PAC
Ina maana kamati ya PAC iliyokuwa inang'ang'ania ipewe mkataba huo haizijui taratibu hizi za ni kamati gani iliyopaswa kuuona?
 
Kwenye eneo la majeshi ni ngumu sana kutumbua majipu ndiyo maana hata CAG huwa hakagui sana kwenye eneo hilo na hasa JWTZ

Sawa lakini masuala ya Kampuni ya Lugumi hayana uhusiano wowote wa manunuzi ya silaha au mambo mengine nyeti ya kijeshi, ni project ya kawaida tu hakuna mambo ya usiri au nini sijui.

Wasitake kuficha maovu kwa kisingizio chochote kile vifaa vya biometric, cctv cameras na servers zake nk havina unyeti wowote na haviwezi kuchukua zaidi ya miaka mitano kukamika kufungwa na kuanza kutumika, kuna kitu kimekaa ndio sivyo pale, we kampuni inawezaje kulipwa asilimia 90% wakati kazi ilivyo fanyika so far haizidi asilimia ishirini 20% hii inaingia akilini kweli? Na wala siamini kama Jaji Rwegasira anaweza kutoa kauli tajwa - watu watakua wamemzulia tu.
 
Kama mleta uzi kasema uongo basi mkuu tunakuomba wewe mwenye ukweli tuwekee hapa ili tujuwe kuliko kutuwacha hewani
Kakuwekea link hapo yenye habari ya ukweli bado unataka ukweli upi?
 
Tatizo mnaingiza uwongo mwingi na udaku kwenye suala hili mpaka linakosa hata maana nzima au watu wengine wenye fikra pana wanaanza kujiuliza na kuangalia kilichoko nyuma ya suala zima.

Ninaamini habari umeitoa hapa halafu ukaiongezea uwongo na udaku kwa faida ya ajenda zako;

Hivi huwa mnapata faida gani mnapoleta thread zenye hoja za uwongo au udaku?
NA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO NAONA SIKU HIZI HAIFANYI KAZI.NYUMBU NI JANGA KUU.
 
Kulikuwa hakuna haja ya Saidi Lugumi kutoroka,mbona kisha shinda hii kesi kama mambo yenyewe yako hivi.
 
Kulikuwa hakuna haja ya Saidi Lugumi kutoroka,mbona kisha shinda hii kesi kama mambo yenyewe yako hivi.

Hajatoroka mkuu wangu ebu ona hii hapa
 

Attachments

  • 1460714803030.jpg
    1460714803030.jpg
    57 KB · Views: 35
Nadhan mkataba unajulikana, " umesainiwa 2011 kusambasa vifaa vya alama za vidole katika vituo vya polis zaid ya 100, kwa jumla tsh billion 37"

Kama hataki uonyeshwe, basi ajibu maswali ya matumizi mabaya ya kodi za wananchi, kwanin zimeshatumika billion 34 kwa vituo 14 pekee..?!
we kwel mgogo,huna akili kama wagogo wenzako,kichwan peupe peee,kwahyo ukiambiwa mkataba ndo unajua ni hzo details? Paka kwel wewe,kama unatetea ugal wako jitahd kuwa deep kdogo angalau
 
Ndio maana JPM analalama kwamba kazi ya uraisi ni ngumu kama angejua tokea mwanzo asingegombea.
Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.

Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.

Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.
 
mhhhhh... hii itazimwa na itapita bila kufanyiwa lolote la maana kama ambavyo yalivyopita maufisadi mengine YOOOOTE kwenye hili taifa.

...iiiif i could turn, turn "foward" the hands of time, then my darling tanzania you 'will' still be ???!!?!!?!?...
 
Back
Top Bottom