04 October 2024
Oysterbay, Dar es Salaam
Tanzania
View: https://m.youtube.com/watch?v=Y5z3HSDrAP4
Jaji Joseph Sinde Warioba anazungumzia uchaguzi unaokuja wa November 2024 TAMISEMI na ule uchaguzi mkuu 2025
Jaji Warioba uchaguzi wa 2019 na 2020 ulikuwa wa kipekee kwa kuwa ulipangwa uwe na dosari nchini nzima tena dosari kubwa za makusudi tofauti na miaka ya 2015 kwenda nyuma hadi 1995 ambapo kulikuwa na dosari ndogo ndogo sehemu chache za nchi.
Baada ya kusema hayo (Jaji Warioba) nataka sasa tuangazie uchaguzi wa serikali za mitaa November 2024 naona kuna taarifa za makusudi kuwakanganya wananchi wasiweze kushiriki kikamilifu uchaguzi wa November 2024.
Elimu inayosemekana inatolewa kwa mpiga kura ni potofu, inachanganya ... mfano serikali ndiyo inasimamia kupitia TAMISEMI uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji ambapo wananchi hawapewi elimu kuwa ili uweze kupiga kura November kuna daftari la mtaani ukajiandikishe ama sivyo hutaweza kushiriki November 2024 kuchagua au kuchaguliwa... hii ni kazi ya Serikali siyo Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa INEC
Tuna wasiwasi yale ya 2019 kuhusu wapiga kura, wagombea na mawakala kuenguliwa, kutoruhusiwa kuingia vituoni, kutoshirikishwa kuhesabu kura pia kushindwa kushirikishwa wakati wa kutangaza matokeo ..
Sheria ya kuwakamata na kuwatia ndani watu, inatumiwa vibaya na wakuu wa wilaya, nakumbuka waziri wa mambo ya ndani ya nchi jenerali Kimaro alipata pressure alitaka kuwatia ndani kina mchungaji Christopher Mtikila waliokuwa wanatofautiana na serikali wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.
Sisi tulikataa na kupiga kelele. Sheria ya DC kutia watu ndani, sheria hiyo bado ipo na watu wanaitafuata sana wanataka waitumie, sasa tunaelekea ktk uchaguzi sheria hiyo kandamizi bado ipo ...
Mtindo wa DC kuongozana na viongozi wa majeshi yote hayo kwa kisingizio cha kuwa mkuu wa Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya, ni kujaribu kuliigiza jeshi la polisi na majeshi mengine mengi ya Tanzania. Pia ni kuwapotezea muda wakuu wa Polisi wa wilaya kushindwa kufanya majukumu yao kwa kuwa wanalazimishwa kuambataba na maDC kila mahali.
Nchi ina majeshi mengi kuanzia Polisi, Misitu, TAKUKURU, UHAMIAJI, MAGERAZA, TISS n.k , Tume ya Haki Jinai imependekeza nchi iwe na jeshi moja tu yaani TPDF / JWTZ na majeshi mengi yavunjwe badala yake yawe Taasisi za Huduma.
Sasa hivi majeshi haya yasiyo TPDF yanakamata, kufunga, kutesa kutokana na muundo wao kuwa wa kijeshi jeshi na kutumika vibaya ... watuhumiwa wakikamatwa hawajulikani wapo wapi na nani kawakamata ...
Utawala bora yaani mfumo wazi unaoeleweka wa haki na mifumo ya usalama ndiyo huzaa demokrasia, bila utawala bora wa kujua nani anafanya nini, mamlaka yake ni yepi na anawajibika kwa nani basi demokrasia inakuwa haipo ...