PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Jaribu uwe na akili angalau hata zile za kukumbuka kujisafisha baada ya kujisaidia au hata za kuuliza ili kujua bei za vitu kabla ya kutaka kununua au hata anhalau za kuvukia barabara.Ni kawaida katika nchi zote duniani baada ya chaguzi zo zote za kisiasa upande ulioshindwa kulalamika kufanyiwa ndivyo sivyo.
Kushindwa kura kunauma, na walioshindwa ni haki yao kulalamika kuwa uchaguzi haukuwa fare and transparent na hivyo ni batili. Kwamba kura ziliibiwa, kulikuwa na kura fake, ujumlishaji wa kura haukuwa sahihi, wagombea walienguliwa kinyume na sheria etc etc
Utaratibu kote duniani pamoja na hapa kwetu (isipokuwa kwa uchaguzi wa raisi), malalamiko kama hayo huwataka walalamikaji kuyafikisha mahakamani wakiwa na ushahidi. Upande wa walalamikiwa (serikali, tume ya uchaguzi etc) hupewa nafasi ya kujitetea na kutoa ushahidi kabla ya mahakama kutoa maamuzi aka hukumu.
Haya yote unayajua vizuri kuliko sisi kwani wewe ni mwanasheria mbobezi uliyepitia mengi. Hata wewe Mzee Wasira alipokushinda kwenye ubunge wa jimbo la Bunda miaka ile ulimburuza mahakamani, kilichotokea kule unakifahamu.
Sasa kwa nini huwashauri hao wanaolalamika kwenye huu uchaguzi wa s/mitaa kuyapeleka malalamiko yao mahqkamani ili mbichi na mbivu zikajulikane huko? Ikajulikane kama ni kweli polisi au hao wasimamizi wa uchaguzi kweli walihusika na wizi wa kura aka kura fake na mengineyo hususani yale ya kuengua wagombea kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Unapoongelea Mahakama, unaongelea Mahakama zipi? Hii ambayo Upinzani walipeleka dai la kuimamishwa kwa uchaguzi sababu una 4thenda kukiuka sheria ya uchaguzi?
Na unapotaja habari za Mahakama, elewa nchi haipaswi kuendeshwa Kimahakama bali kwa mseto wa utawala bora. Watu wafanye upumbavu hadharani kabisa halafu ubaki kutegemea mahakama ambako pia wamejazana makada tupu?