LGE2024 Jaji Warioba kabla kutoa hukumu yako hususani ya Uchaguzi wa S/Mitaa, uwe umsikiliza pande zote na ushahidi ulionao

LGE2024 Jaji Warioba kabla kutoa hukumu yako hususani ya Uchaguzi wa S/Mitaa, uwe umsikiliza pande zote na ushahidi ulionao

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sasa mtu amekosa vigezo vya kuwa mgombea atachaguliwa vipi?
Wewe kiazi mtu mzima yeyote ambaye sio mhalifu na ni raia wa Tanzania anatosha kuwa mwenyekiti au mjumbe wa kijiji, mtaa na kitongoji. Hayo mengine yote ni porojo za kihuni tu.
 
Ni kawaida katika nchi zote duniani baada ya chaguzi zo zote za kisiasa upande ulioshindwa kulalamika kufanyiwa ndivyo sivyo.

Kushindwa kura kunauma, na walioshindwa ni haki yao kulalamika kuwa uchaguzi haukuwa fare and transparent na hivyo ni batili. Kwamba kura ziliibiwa, kulikuwa na kura fake, ujumlishaji wa kura haukuwa sahihi, wagombea walienguliwa kinyume na sheria etc etc

Utaratibu kote duniani pamoja na hapa kwetu (isipokuwa kwa uchaguzi wa raisi), malalamiko kama hayo huwataka walalamikaji kuyafikisha mahakamani wakiwa na ushahidi. Upande wa walalamikiwa (serikali, tume ya uchaguzi etc) hupewa nafasi ya kujitetea na kutoa ushahidi kabla ya mahakama kutoa maamuzi aka hukumu.

Haya yote unayajua vizuri kuliko sisi kwani wewe ni mwanasheria mbobezi uliyepitia mengi. Hata wewe Mzee Wasira alipokushinda kwenye ubunge wa jimbo la Bunda miaka ile ulimburuza mahakamani, kilichotokea kule unakifahamu.

Sasa kwa nini huwashauri hao wanaolalamika kwenye huu uchaguzi wa s/mitaa kuyapeleka malalamiko yao mahqkamani ili mbichi na mbivu zikajulikane huko? Ikajulikane kama ni kweli polisi au hao wasimamizi wa uchaguzi kweli walihusika na wizi wa kura aka kura fake na mengineyo hususani yale ya kuengua wagombea kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kesi ya mbuzi kwenda kwa fisi,ni ama mawili fisi apate kitoweo ama amraruerarue tu mbuzi bila hata ya sababu kwani hata kumla hamli kwa kuwa anashibe.
 
Yaan kati ya kitu ambacho wapinzan walijichanganya ni kuingia kwenye huu uchaguz wakijua fika mwamuz wa matokeo ni CCM,kwanza wagombea wa upinzani walienguliwa mbaya Zaid CCM ikajitangazia ushindi wa mezani,Hawa wapinzan wasije wakathubutu kuingia tena kwenye uchaguz wa namna hii,nafikiri hata mwakani yatatokea haya haya halafu wataanza kulalamika bila kuchukua hatua,Warioba anastahili tuzo amegusa penyewe na ni mzalendo
Wangewezaji kuitambulisha aibu yenu,hapo wamewaacheni bila nguo,basi angalao mngechutama,ila wapi?
 
Back
Top Bottom