Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

Ushahidi upi wa Makonda ambao wewe umeutoa hapa au ni chuki zako tu? Ofcourse dogo ana hela na ni don sasa kinakuuma nini badala upambane na maisha unakalia majungu tu
 
Wewe mwenye akili hakikisha una utajiri kumzidi yeye acha ushamba
 
Ipo wazi kwamba kila binaadamu ana mabaya yake na mazuri yake, sasa likitokea kundi linamfanya binaadamu mwenzao kuwa hana mazuri ana mabaya tu na kundi lengine linamfanya binaadamu mwenzao hana mabaya ana mema tu basi hapo linapokuja tatizo.
Ni kweli, tatizo linakuja hapo, si kwamba jamaa hakufanya mazuri, kuna mazuri mengi alifanya! Ishu ni pale yakizungumzwa madhaifu ya awamu yake, wapambe wake wanakuja juu kama Mbogo, mara katukanwa n.k.! But the same time mazuri/mabaya ya awamu zingine zote yanazungumzwa vizuri tu, watu wanayajadili na maisha yanasonga! Sasa huu udikteta wa kupangiana cha kuzungumza kuhusu awamu ya 5 sijui umetoka wapi!
 
Ushahidi upi wa Makonda ambao wewe umeutoa hapa au ni chuki zako tu? Ofcourse dogo ana hela na ni don sasa kinakuuma nini badala upambane na maisha unakalia majungu tu
Hahaha! Utajiri ambao mtaji ni ukuu wa mkoa? Wewe jamaa wa hovyo sana! Arudishe mali alizokwapua kutumia jina la Jiwe sasa, aache kulialia
 
Hahaha! Utajiri ambao mtaji ni ukuu wa mkoa? Wewe jamaa wa hovyo sana! Arudishe mali alizokwapua kutumia jina la Jiwe sasa, aache kulialia
Huo uchoko kwani mkuu wa mkoa hawezi kuanzisha miradi binafsi? Mbona unakuwa zwazwa sana
 

..hata Magufuli alikosea kuweka picha ktk fomu yake lakini Tume ikamhurumia.

..Juma Duni Haji ambaye amegombea chaguzi nyingi alienguliwa ktk uchaguzi wa 2020.

NB:

..Mwaka 2020 Tume ya uchaguzi iliengua wagombea wengi wa upinzani kuliko ilivyofanya mwaka 1995.

Cc WALOLA VUNZYA , Nguruvi3
 
Mzee Warioba aliwahi kusema kazi ya tume si kuengua wagombea, kukosea kujaza fomu si sababu ya kumuengua mgombea, akauliza sheria hiyo ipo wapi?
Tume inapata wapi muongozo huo?

Pili, kuna matatizo mengi.
Wakurugenzi kukimbia ofisi mgombea achelewe kurudisha Fomu . Wanaochelewa ni Wapinzani tu

Tatu, kuna uhuni wa watu kunyang'anywa fomu na ni Wapinzani tu, haijawahi kutokea Polisi ikakamata watu hao ambao kisheria ni wahalifu kama wahalifu wa uporaji tu

Ukimsikiliza Mahera lazima tumbo litakukata, tuna watu wa ajabu sana
Mahera anasema kama kuna kuenguliwa tume haihusiki kwasababu haifiki huko vijijini.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzani Dr Mahera anadhani tume ipo makao makuu tu ikisubiri kujumlisha matokeo. Huyu ni Dr hajui wigo wa Tume, unabaki kujiuliza sana!

Ni kama niliyosikia Dr Kitila akisema kwanini Wapinzani hawakwenda Mahakamani.

Mkumbo anajua Jaji mkuu aliambiwa kuna mhimili uliojichimbia tangu hapo tukaanza kumuona kila hafla ya kuapishwa hata Wenyeviti wa Bodi.

Mahakama iliyosema Wakurugenzi wakiapa basi ni waadilifu kwasababu ya kiapo
Hii ndiyo unapeleka kesi ya kushindwa tena wakati wa mwendazake utegemee haki

Mkumbo bado ana kumbu kumbu za akina Nyalali, Kisanga, Samatta!
Sijui ni kuvimbiwa asali au ni kitu gani.
 
Jaji Warioba ametoa valid observation,wanaopinga wapinge tu,lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.
-Uongozi wa CCM ulitaka Mgombea wao apate ushindi wa kimbunga,ili kumtia moyo kuwa anafaa kuongoza nchi.
-Mamlaka ya uteuzi iliwahi kuchimba mkwara Kwa wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji ikiwaonya kuwa "wameteuliwa kuwa wakurugenzi na wamepewa magari na nyumba, halafu wasikie CCM imeshindwa uchaguzi".
-Ujumbe huo ulichangia haki kutofanyika wilaya zote.
-wasimamizi wa uchaguzi walitumia hila kuchakachua matokeo mpaka wamejikuta ,wapinzani wana viti viwili tu
-Na matakwa ya Sheria ,kamati ya PAC na LAAC bungeni ni lazima ziongozwe na wapinzani,
-Ndipo walipowachukua Covid-19, baada ya Chadema kutishia kutotambua matokeo na kutopendekeza wabunge wa vitie maalum ni aibu,
-wenye Chama ( CCM ) wanakiri
kuwa kulikuwa na mapungufu,yanayohitajika kurekebishwa.
-Jaji Warioba ndiyo waanzilishi wa CCM na amebaki kuwa mwanaccm lakini siyo mnafiki.


Ushauri
-Ushindi Ni ushindi,hata ukipata asilimia 51 ya wapiga kura bado ni ushindi.
-Viongozi wetu wawe wanasutwa na nafsi zao,waache unafiki, wasipende kusema Yale ambayo mkuu anaipenda kuyasikia,wakiwa pembeni,na wao wanalilia.
-Mwenyekiti wa CCM awe na forum ya kuonana na hawa wazee wetu ( Makada wa CCM ) na kupata ushauri huru , kabla ya kufanya vikao vya kamati kuu au Halmashauri kuu,hii itaondoa tabia ya Makada wa CCM kutoa maoni na ushauri kwenye makongano.
 
Tatizo ni hapo kuna kundi ambalo halitaki na haliwezi kuvumilia kuona huyo jamaa anazungumziwa kinyume na mabaya ya huyo mtu, kuna wengine wanakwenda mbali zaidi hawataki hata kukubali kwamba huyo mtu ana mema, ndio maana kila pale anapozungumziwa huyo mtu si kwa mabaya wao huona kama anasifiwa shetani hivyo huchefukwa na kuja kueleza mabaya hata yale ambayo hayahusiani na mada husika.
 
Wewe ndio zwazwa sadist ambaye unawahusudu madikteta na watu makatili
Mkuu wale sio tu kuwahusudu bali wamesaidia kwa upande flani kupunguza wapumbavu nchini
 
Magufuri alikuwa mshamba tu, aliyetokea kijijini huko.kwani Nape unafikiri alikosea aliposema tuna rais mshamba, alikuwa sahihi huoni mamlaka imemrudisha tens
 
Unafahamu hats Adolf Hitler na Makaburu kuna mema walifanya?
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Aliyemteua Mahera si ndio huyo huyo alimteua mkuu wa mahakama? Kwa akili yako ulitegemea Mahera anaweza kupokea maelekezo na kuyatekeleza lakini mkuu wa mahakama asitekeleze? Aibu ndogo ndogo kama hizi unaweza kuziepuka mkuu
 
Unafahamu hats Adolf Hitler na Makaburu kuna mema walifanya?
Ndio nafahamu si ndio tumesema kila binaadamu ana mema na mabaya yake na hao pia ni binaadamu, kwahiyo inategemea unapomzungumzia mtu unamzungumzia kwa lipi. Kuna mengi ya kumzungumzia binaadamu hasa akiwa kiongozi hata huyo Hitler au iwe Osama bin laden kabisa.
 
Madini ya mzee Warioba haya, halafu kuna Mkulya kule space anadai huyu mzee sio CREDIBLE wa kushiriki kongamano hili sababu ni CCM. Alijaribu kumu dharirisha kuhalalisha kugomea ushiriki wao. Ati Hana ufahamu wa madhira waliyowapata vidole juu. Nashukuru MM alimukanya asimudharau mzee huyu. Ndiye aliyetuletea rasimu ya katiba tunayoipigania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…