Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
- Thread starter
- #121
Huyo huyo hahahaha, alikuwa anaungurumaSimba wa Yuda?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo huyo hahahaha, alikuwa anaungurumaSimba wa Yuda?
Kipindi Cha Kinana CCM waliiba kura ila kwa aligorithm yaani Gap iwe 60-40% kuanzia Kata hadi Urais. Ila kwa JPM aisee hakuna Cha formula yeye alizoa kila kitu kuanzia vijiji hadi Urais 90%+
Yaani mpaka Pemba eti CCM ilishinda majimbo karibu yote!! Seriously?
Then demokrasia haiishii tu kwenye uchaguzi, hata ushiriki wa wapinzani kwenye vyombo vya wawakilishi, free media, na uhuru wa maoni ikiwemo vyama vingi kufanya mikutano n.k, and more than other 11 principles of democracy walau hata 9 zilikuwepo. Ila kwa JPM hakukuwepo hata moja so unapo compare factor in Kila kitu sio chaguzi pekee.
Kujua kusoma na kuandika Kiswahili! Zinjathroupus ni kiswahili? Nina uhakika hata Jiwe asingeweza kulitamka hilo neno ipasavyoKuna Mgombea alibisha kuwa anajua kusoma na kuandika akaandikiwa Zinjathroupus akashindwa kusoma wakala kichwa
Wengi wao wanatafuta cha kulamu baada ya kushindwa. Baadhi ya form zilizoenguliwa ziliwekwa hapa JF na walalamikaji, na kweli zilikuwa na makosa, ila wao walisema kuwa makosa hayo yalikuwa madogo. Normally ukishafanya kosa, lazima hukumu ifuatie. Usipokubaliana nayo, unakata rufaa. Wengi wao walikata rufaa na kuhurumiwa, lakini siyo kuwa walikuwa wameonewa bali ni kweli kulikuwa na makosa katika kujaza fomu zao. Mmoja aliandika kuwa chama chake ni ACT, lakini kisheria hakuna chama kinaitwa ACT bali kuna ACT-Wazalendo. Ni kosa dogo, lakini ni kosa.Kwanini hawakuenda mahakamani?
Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Kujua kusoma na kuandika Kiswahili! Zinjathroupus ni kiswahili? Nina uhakika hata Jiwe asingeweza kulitamka hilo neno ipasavyo
Baadaye akamtumbua!! Jiwe alikuwa msanii sana
Zinja ni common name kama Pwani? Ni waTZ wangapi wanaweza kulisoma hilo neno, au kuliandika ipasavyo?Jina halina lugha
Mkoa wa Pwani utaitwa Pwani katila lugha zote utazotumia
Zinja ni common name kama Pwani? Ni waTZ wangapi wanaweza kulisoma hilo neno, au kuliandika ipasavyo?
Wangemuandikia "Pwani", siyo unamuandikia mtu asome neno "Schwarzenegger", then akishindwa kusoma unamcheka, ni ulimbukeni na utotoJina halina lugha haijalishi ni common au sio common
Mwanzo hukujua hilo ndio sababu ukasema walipaswa wajue kusoma na kuandika kiswahili ukidhan jina ni sehemu ya lugha
Tunajuana hata mimi huwa mbishi kukubali kukosolewa so tuendelee na mengine
Wengi wao wanatafuta cha kulamu baada ya kushindwa. Baadhi ya form zilizoenguliwa ziliwekwa hapa JF na walalamikaji, na kweli zilikuwa na makosa, ila wao walisema kuwa makosa hayo yalikuwa madogo. Normally ukishafanya kosa, lazima hukumu ifuatie. Usipokubaliana nayo, unakata rufaa. Wengi wao walikata rufaa na kuhurumiwa, lakini siyo kuwa walikuwa wameonewa bali ni kweli kulikuwa na makosa katika kujaza fomu zao. Mmoja aliandika kuwa chama chake ni ACT, lakini kisheria hakuna chama kinaitwa ACT bali kuna ACT-Wazalendo. Ni kosa dogo, lakini ni kosa.
Ninavyoelewa ni kuwa wagombea huenguliwa kwa kuwekewa mapingamizi. Iwapo CCM hawakuwekewa mapingamizi, basi huenda makosa hayo yakapita. Tatizo ni kuwa wapinzania walikuwa hawakujiandaa vizuri, kwani walikubali kuwekewa mapingamizi, lakini wao hawakuweka. Kuhusu Magufuli kutumia snippets za lugha za Kienyeji kwenye kampeini zake kote alikopita; siyo kanda ya ziwa tu, huwezi kusema katumia lugha kupiga kampeini. Hotuba zote za za kuombea kura kwenye kampeini zilikuwa zinenedeshwa kwa kiswahili isipokuwa zile sehemu za kusalimia ambapo alikuwa na tabia ya kusalimia kwa kutumia lugha ya eneo hilo.Kama kweli hayo yalikuwa ni baadhi ya makosa ya kuwaengua wapinzani, basi hata ccm walifanya sana, na bado hawakuadhibiwa. Na ushahidi wa hizo fomu zilizokosewa uliwekwa hapa jukwaani, tena na baada ya wagombea wa vyama vya upinzani. Na hazikuchukuliwa hatua zozote.
Shera za uchaguzi zinakataza mgombea kutumia kilugha kuombea kura, lakini Magufuli alipoona amezidiwa na Lisu huko kanda ya ziwa, alikuwa anatumia kisukuma tena wazi wazi akiwafokea wahudhiriaji wa kwenye kampeni, kwanini wanajazana kwenye mikutano ya msaliti yaani Lisu, japo hakumtaja Lisu kwa jina. Jambo lile lililalamikiwa kwa tume ya uchaguzi, na wakatoa utetezi wa kumuogopa Magufuli eti kuwa alikuwa anafafanua sera za ccm kwakuwa walitaka wazielewe zaidi. Kwahiyo kama unajaribu kutetea ushenzi ule jikite kwenye ukweli huo.
Wangemuandikia "Pwani", siyo unamuandikia mtu asome neno "Schwarzenegger", then akishindwa kusoma unamcheka, ni ulimbukeni na utoto
Mpuuzi kweli weye!Kwenda mahakamani,tena Tanzania ndiyo wangekufurahisha.Nyoko!Kwanini hawakuenda mahakamani?
Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Hahahaha, sawa ChiefNdio Siasa zipo hivyo Dunia nzima
Kasome Black American Movement uone weusi walivyokuwa wakipigwa dana dana kwy kupiga kura
Kuna Mwana Mama mweusi alipofika eneo la kupiga kura Wakala akamuandikia kwa lugha ya kichina asome…yule Mwana Mama akasoma 'Mzungu hataki mweusi apige kura' alipoulizwa akasema alisoma akili ya alieandika yale maandishi na sio maandishi yenyewe
Ninavyoelewa ni kuwa wagombea huenguliwa kwa kuwekewa mapingamizi. Iwapo CCM hawakuwekewa mapingamizi, basi huenda makosa hayo yakapita. Tatizo ni kuwa wapinzania walikuwa hawakujiandaa vizuri, kwani walikubali kuwekewa mapingamizi, lakini wao hawakuweka.
Ila wewe mtu nikikumbuka ulivyokuwa na posts za kuudhi enzi za JPM, na U-turn uliyoipiga ghafla huwa nawaza mbali sana. Umenifundisha kuwa siyo kila anayekupigia makofi anakuunga mkono. Nyie ni wanafiki, wahuni na waganga njaa tu.Kuna kuiba na kupora, hivi ni vitu viwili tofauti.
Kuiba kura hata Chadema na ACT wazalendo wanaiba.
Ila kupora lazima utumie nguvu zaidi ya Akili, ndivyo ilivyokuwa 2020!
Vazi limeuziwa dhambiNchi ilipitia kwenye mateso makubwa .
Pichani huyo alikua ni mgombea aliyekua akirejesha fomu ili kuepuka kutekwa na makuwadi wa dikteta ilibidi jamaa avae ushungi.
Udikteta ulitembea kwenye kivuli cha uzalendo uchwara.
View attachment 2176537View attachment 2176537View attachment 2176538
Tuweke kumbukumbu sawa. Siyo Magufuli peke yake. CCM kwa ujumla wake siyo waumini wa Demokrasia. Tangu tuurudishe mfumo wa vyama vingi ni uchaguzi upi ambao haujagubikwa na ghilba?Wameweka na ushahidi upo, kwa mfano kuna bwana mmoja anaitwa somebody Odero alikuwa mgombea wa udiwani kwenye baadhi ya kata huko mkoa wa Mara, alikwenda hadi kwenye kipindi cha Star Tv na kusema hayo mapungufu. Wakati anaendelea kusema hayo, ghafla matangazo yale yakakatishwa na mtangazaji wa kipindi kile aliomba msamaha kuwa hawezi kuendelea na kile kipindi. Lakini mtangazaji wa kipindi kile alionyesha kufedheheka sana. Huo ni mfano mmoja wa dhahiri wa hujuma kwenye uchaguzi ule. Acha waliotekwa wakirejesha fomu, na hayo yalifanywa na vijana wanaofahamika, na kibaya zaidi hayo yalifanyika mbele ya vyombo vyote vya dola. Na ukienda kushitaki ww mpinzani unageuziwa kibao.
Mfano mwingine wa dhahiri wa uhayawani wa Magufuli kwenye chaguzi chini yake, ni uchaguzi wa marudio hapa Dar wa jimbo la Mtolea hapa temeke. Wakati huo vituo vya televisheni na redio vilikuwa bado vinaruhusiwa kutangaza mubashara. Kwa macho yangu niliona mabox ya kura yakiletwa na vijana, chini ya uratibu wa polisi. Msimamizi wa uchaguzi alipoulizwa inakuwaje akasema yeye anaangalia wapiga kura na sio mabox ya kura. Baada ya muda matangazo yale yalikatwa na mtangazaji alikuwa Sam Mahela wa ITV, kisha katika hali ya kushangaza kabisa, taarifa ya habari ya saa 2 usiku ITV wakaomba msamaha kww kurusha tukio lile. Ule ndio ukawa mwisho wa vyombo vya habari kutangaza uchaguzi live. Nyuma ya pazia Sam Mahela alisumbuliwa sana na genge hatari la Magufuli la watu wasiojulikana na kituo cha ITV. Baadae Sam Mahela alihamia TBC!
Halafu iko hivi boss, usijifanye kutetea maovu yaliyokuwa wazi vile kama watu hatuna uelewa wowote wa tabia za magu. Fuatilia rekodi yote ya kwake toka akiwa mbunge kwa 20yrs, kama alishinda kihalali ni uchaguzi mmoja tu, tena wa mwanzo. Lakini chaguzi nyingine zote alikuwa anatangazwa mshindi kwa figisu maana hakuwa na ushawishi wa kisiasa. Kama aliweza kufanya hayo akiwa mbunge na waziri tu, je chini ya hii katiba ya rais Mungu ulitegemea angefanyaje? Ni kushauri tu, kwenye huu uzi kaa mbali, maana tuna ushahidi wote wa utawala wa kidhalimu wa Magufuli. Kama unamtetea kamtetee kwenye miundombinu kadhaa aliyosimamia, na sio jambo lolote linalohusu demokrasia.