Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini


Kilichomfanya Magufuli apore uchaguzi badala ya kuiba ni baada ya kuona ameipotezea ccm mvuto, na akaogopa matokeo halali yakitangazwa hata kama ccm itakuwa imeshinda lakini itakuwa imepata kura chache kuliko ilivyotaka, na bado wapinzani wangekuwa wamepata kura nyingi sana. Sasa ili kulazimisha kuwa ccm ilikuwa imara chini yake, ikabidi apore uchaguzi ule. Lakini kimsingi alipoteza furaha yake yote, hasa ukizingatia kampeni alizoondesha Lisu, na support aliyopata ilimumiza sana. Toka wakati wa kampeni, uchaguzi hadi anakuja kufariki hakuwahi kurudisha furaha yake. Ni kama uchaguzi ule ulimuacha na msongo wa mawazo kwani alishuhudia ukweli uliomuumiza roho yake.
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Wengi wao wanatafuta cha kulamu baada ya kushindwa. Baadhi ya form zilizoenguliwa ziliwekwa hapa JF na walalamikaji, na kweli zilikuwa na makosa, ila wao walisema kuwa makosa hayo yalikuwa madogo. Normally ukishafanya kosa, lazima hukumu ifuatie. Usipokubaliana nayo, unakata rufaa. Wengi wao walikata rufaa na kuhurumiwa, lakini siyo kuwa walikuwa wameonewa bali ni kweli kulikuwa na makosa katika kujaza fomu zao. Mmoja aliandika kuwa chama chake ni ACT, lakini kisheria hakuna chama kinaitwa ACT bali kuna ACT-Wazalendo. Ni kosa dogo, lakini ni kosa.
 
Jina halina lugha

Mkoa wa Pwani utaitwa Pwani katila lugha zote utazotumia
Kujua kusoma na kuandika Kiswahili! Zinjathroupus ni kiswahili? Nina uhakika hata Jiwe asingeweza kulitamka hilo neno ipasavyo
 
Jina halina lugha

Mkoa wa Pwani utaitwa Pwani katila lugha zote utazotumia
Zinja ni common name kama Pwani? Ni waTZ wangapi wanaweza kulisoma hilo neno, au kuliandika ipasavyo?
 
Jina halina lugha haijalishi ni common au sio common
Mwanzo hukujua hilo ndio sababu ukasema walipaswa wajue kusoma na kuandika kiswahili ukidhan jina ni sehemu ya lugha

Tunajuana hata mimi huwa mbishi kukubali kukosolewa so tuendelee na mengine

Zinja ni common name kama Pwani? Ni waTZ wangapi wanaweza kulisoma hilo neno, au kuliandika ipasavyo?
 
Jina halina lugha haijalishi ni common au sio common
Mwanzo hukujua hilo ndio sababu ukasema walipaswa wajue kusoma na kuandika kiswahili ukidhan jina ni sehemu ya lugha

Tunajuana hata mimi huwa mbishi kukubali kukosolewa so tuendelee na mengine
Wangemuandikia "Pwani", siyo unamuandikia mtu asome neno "Schwarzenegger", then akishindwa kusoma unamcheka, ni ulimbukeni na utoto
 

Kama kweli hayo yalikuwa ni baadhi ya makosa ya kuwaengua wapinzani, basi hata ccm walifanya sana, na bado hawakuadhibiwa. Na ushahidi wa hizo fomu zilizokosewa na wanaccm uliwekwa hapa jukwaani, tena na baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani. Na hazikuchukuliwa hatua zozote.

Sheria za uchaguzi zinakataza mgombea kutumia kilugha kuombea kura, lakini Magufuli alipoona amezidiwa na Lisu huko kanda ya ziwa, alikuwa anatumia kisukuma tena wazi wazi akiwafokea wahudhiriaji wa kwenye kampeni, kwanini wanajazana kwenye mikutano ya msaliti yaani Lisu, japo hakumtaja Lisu kwa jina. Jambo lile lililalamikiwa kwa tume ya uchaguzi, na wakatoa utetezi wa kumuogopa Magufuli eti kuwa alikuwa anafafanua sera za ccm kwakuwa walitaka wazielewe zaidi. Kwahiyo kama unajaribu kutetea ushenzi ule jikite kwenye ukweli huo.
 
Ninavyoelewa ni kuwa wagombea huenguliwa kwa kuwekewa mapingamizi. Iwapo CCM hawakuwekewa mapingamizi, basi huenda makosa hayo yakapita. Tatizo ni kuwa wapinzania walikuwa hawakujiandaa vizuri, kwani walikubali kuwekewa mapingamizi, lakini wao hawakuweka. Kuhusu Magufuli kutumia snippets za lugha za Kienyeji kwenye kampeini zake kote alikopita; siyo kanda ya ziwa tu, huwezi kusema katumia lugha kupiga kampeini. Hotuba zote za za kuombea kura kwenye kampeini zilikuwa zinenedeshwa kwa kiswahili isipokuwa zile sehemu za kusalimia ambapo alikuwa na tabia ya kusalimia kwa kutumia lugha ya eneo hilo.
 
Ndio Siasa zipo hivyo Dunia nzima

Kasome Black American Movement uone weusi walivyokuwa wakipigwa dana dana kwy kupiga kura


Kuna Mwana Mama mweusi alipofika eneo la kupiga kura Wakala akamuandikia kwa lugha ya kichina asome…yule Mwana Mama akasoma 'Mzungu hataki mweusi apige kura' alipoulizwa akasema alisoma akili ya alieandika yale maandishi na sio maandishi yenyewe
Wangemuandikia "Pwani", siyo unamuandikia mtu asome neno "Schwarzenegger", then akishindwa kusoma unamcheka, ni ulimbukeni na utoto
 
Hahahaha, sawa Chief
 

Wameweka na ushahidi upo, kwa mfano kuna bwana mmoja anaitwa somebody Odero alikuwa mgombea wa udiwani kwenye baadhi ya kata huko mkoa wa Mara, alikwenda hadi kwenye kipindi cha Star Tv na kusema hayo mapungufu. Wakati anaendelea kusema hayo, ghafla matangazo yale yakakatishwa na mtangazaji wa kipindi kile aliomba msamaha kuwa hawezi kuendelea na kile kipindi. Lakini mtangazaji wa kipindi kile alionyesha kufedheheka sana. Huo ni mfano mmoja wa dhahiri wa hujuma kwenye uchaguzi ule. Acha waliotekwa wakirejesha fomu, na hayo yalifanywa na vijana wanaofahamika, na kibaya zaidi hayo yalifanyika mbele ya vyombo vyote vya dola. Na ukienda kushitaki ww mpinzani unageuziwa kibao.

Mfano mwingine wa dhahiri wa uhayawani wa Magufuli kwenye chaguzi chini yake, ni uchaguzi wa marudio hapa Dar wa jimbo la Mtolea hapa temeke. Wakati huo vituo vya televisheni na redio vilikuwa bado vinaruhusiwa kutangaza mubashara. Kwa macho yangu niliona mabox ya kura yakiletwa na vijana, chini ya uratibu wa polisi. Msimamizi wa uchaguzi alipoulizwa inakuwaje akasema yeye anaangalia wapiga kura na sio mabox ya kura. Baada ya muda matangazo yale yalikatwa na mtangazaji alikuwa Sam Mahela wa ITV, kisha katika hali ya kushangaza kabisa, taarifa ya habari ya saa 2 usiku ITV wakaomba msamaha kww kurusha tukio lile. Ule ndio ukawa mwisho wa vyombo vya habari kutangaza uchaguzi live. Nyuma ya pazia Sam Mahela alisumbuliwa sana na genge hatari la Magufuli la watu wasiojulikana na kituo cha ITV. Baadae Sam Mahela alihamia TBC!

Halafu iko hivi boss, usijifanye kutetea maovu yaliyokuwa wazi vile kama watu hatuna uelewa wowote wa tabia za magu. Fuatilia rekodi yote ya kwake toka akiwa mbunge kwa 20yrs, kama alishinda kihalali ni uchaguzi mmoja tu, tena wa mwanzo. Lakini chaguzi nyingine zote alikuwa anatangazwa mshindi kwa figisu maana hakuwa na ushawishi wa kisiasa. Kama aliweza kufanya hayo akiwa mbunge na waziri tu, je chini ya hii katiba ya rais Mungu ulitegemea angefanyaje? Ni kushauri tu, kwenye huu uzi kaa mbali, maana tuna ushahidi wote wa utawala wa kidhalimu wa Magufuli. Kama unamtetea kamtetee kwenye miundombinu kadhaa aliyosimamia, na sio jambo lolote linalohusu demokrasia.
 
Kuna kuiba na kupora, hivi ni vitu viwili tofauti.

Kuiba kura hata Chadema na ACT wazalendo wanaiba.

Ila kupora lazima utumie nguvu zaidi ya Akili, ndivyo ilivyokuwa 2020!
Ila wewe mtu nikikumbuka ulivyokuwa na posts za kuudhi enzi za JPM, na U-turn uliyoipiga ghafla huwa nawaza mbali sana. Umenifundisha kuwa siyo kila anayekupigia makofi anakuunga mkono. Nyie ni wanafiki, wahuni na waganga njaa tu.
Afadhali mwenzenu Polepole ameendelea kuwa consistent kwa alichokiamini na kukisimamia
 
Tuweke kumbukumbu sawa. Siyo Magufuli peke yake. CCM kwa ujumla wake siyo waumini wa Demokrasia. Tangu tuurudishe mfumo wa vyama vingi ni uchaguzi upi ambao haujagubikwa na ghilba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…