Jaji Warioba: Viongozi na wanahabari acheni uchawa mnaumiza wananchi
Una eneo la mkoa wa kodi huyo kiongozi wao kilaza anae tangaza migomo, alivyo mpuuzi anasema hilo eneo lina biashara 40,000 zilizosajiwa kwa VAT chini yake.

Anajusifia makusanyo ni billion 14 kwa mwezi, wakat kwa takwimu hizo minimum collection ye mwezi inatakiwa kuwa 120 billion, maximum ni karibu 420 bilion kwa mwezi.

Watu wanapiga kelele raisi anamtoa mtu anaefanya kazi. Na kuna washauri huko Ikulu wa maswala ya u humo (civil servant) ambao hawawezi mwambia unakosea.

Unadhani huko ulaya civil services zao au washauri wake zina watu wapumbavu karibu na raisi kama ilivyo kwetu.

Hakuna mtu anaehujumu Yanzanis, tupo hapo kwa uwezo wa kufikiria.
Juzi nipo mahala namsikiliza one of the most senior civil servant wa UK akiongelea kuhusu transfer of power baina ya new PM na yule Rishi, akasema kwa wao (civil servants) huakikisha hakuna changes zozote ambazo zitaathiri maslahi ya taifa zitazingatiwa, regardless ni chama gani chaingia madarakani.

Halafu akasema "issues of state-craft require great deliberation bila kufafanua zaidi.

Hawa watu kama huna nchi huyumba sana. Hukaa mafichoni sana lakini huongea kwa kalamu pekee yenye wino mwingi.

Ndo maana kuna mada nyingi nimechangia kuwa madam president ahitaji special advisers wenye ujuzi.
 
Akizungumza mbele ya Media Council of Tanzania, waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba

View: https://m.youtube.com/watch?v=MvpysrliGgU

Ninatazama bunge la Dodoma, imekuwa fasheni kila mbunge kuanza mchango wake wa hoja kwa kutaja na kumsifia rais.

Vyombo vya habari kwa nyakati ya sasa hivi badala ya kutoa habari vimegeuka kuwa vyombo vya propaganda yaani uchawa ...

Woga umetamalaki kwa kisingizio cha self censorship/ nidhamu ya woga, hakuna habari za kiuchunguzi yaani zili zilizofayiwa research kwa kuogopa zinaweza kuwa kinzani na uchawa uliopo anasema Jaji Joseph Sinde Warioba ...

Waziri mkuu mstaafu anabainisha kuwa mwaka 1961 alifanya kazi na chombo cha media cha The Standard kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Chuo Kikuu. Hivyo anakumbuka viwango vya uandishi wa habari enzi hizo, na kulinganisha na hivi sasa ambapo yeye ni sehemu ya consumer society yaani walaji na anaona mapungufu makubwa ya viwango vya uandishi na utoaji habari ... kutokana na woga kuwakaba Media na hata viongozi..

Jaji Joseph Sinde Warioba anasema aliteuliwa katika Tume ya Haki Jinai kisha pia kuingizwa ktk Kamati ya Kutekekeza Mapendekezo ya Tume. Huko pia aliona woga wa wananchi ambao wengi hawataki kutoa ushirikiano kwa vyombo vya Haki Jinai kama Polisi, TAKUKURU n.k kwa kuhofia kupata matatizo ...

Wananchi wanahitaji habari za kila aina siyo hizi za uchawa / propaganda pekee zinazobebwa na media zote kusifia au kupamba kinamna habari zinazopendwa kusikika na viongozi....anasema Jaji Warioba.

Nafahamu kika chombo cha habari kina editorial policy / sera za mwegemeo, lakini vyombo hivyo visiwe kama kasuku kwa kutoa habari zenye chanzo / source kimoja bali vifanye research / uchunguzi ili habari katika vyombo vya habari ziaminike na kuwa habari zenye kuweza kufanyiwa rejea au kunukuliwa kwa uhakika.... ..

Jaji Joseph Warioba anawasa waandishi habari nguli na wahariri waliojitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na Jukwaa la Wanahabari wa Tanzania / Media Council of Tanzania, kuwa tabia ya kuendekeza uchawa / propaganda haiwasaidi wananchi wala viongozi ....

Nchi hii imejenga matabaka mawili yaani la juu ni viongozi, private sector na ninyi wasomi waandishi wa habari / wahariri na kujitambulisha kama tabaka 'muhimu' .....

Na tabaka hili la kwanza hufanya mikutano ya 'viongozi' bila kushirikisha tabaka la wananchi. Na item / point ya kwanza badala ya kuanza na ajenda, utambulisho ndiyo unaanza kwa urefu sana dakika hadi 15 kutaja kila kiongozi ... na kuhitimishwa itifaki / protokali imezingati.....

Jaji Warioba anasema masuala ya Itifaki imezingatiwa alianza kuona na kusikia Nigeria ambapo wenzetu kule hutaja viongozi wawili tu na wengine wote huingiza ktk kundi la itifaki imezingatiwa. Lakini hapa kwetu Tanzamia kutokana na uchawa huwa tunataja viongozi wote na itifaki inazingatiwa ni kwa kundi la wananchi wasio viongozi...

Hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha ilichukua ilikuwa ya masaa 2 na dakika 6 baada ya hapo utambulisho ikichukua dakika 40 kuwataja viongozi waliopo ukumbini, lakini wakasahau kuwa nje ya ukumbi kuna wananchi wanasikiliza hawa hawakutajwaa kabisa wakati hii ni bajeti ya nchi siyo wa viongozi .. .Jaji Wariiba anasimulia kasumba hii ilivyoota mizizi ...

Hata hotuba zimekuwa watu wetu / wangu , zamani ilikuwa katika hotuba neno wananchi ndiyo limetamalaki anabainisha jaji Joseph Warioba kuonesha tabaka .... wananchi wamekuwa kama ni mali ya viongozi wakati wananchi ndiyo waliowaajiri viongoziv....

Kauli za wananchi waelimishwe baada ya kuanda sera au muswada inaukakasi asema Jaji Warioba. Ni kutokana na sisi tabaka la viongozi waanda sera kutowashirikisha wananchi toka mwanzo, kwa kuwa viongozi wanajiona wanahaki ya kuandaa muswada au sera bila kushirikisha umma, kisha wananchi waelimishwe..

Jaji Warioba anasema wanachofanya wananchi hakifahamiki, mfano angalia vichwa vya habari asubuhi ktk magazeti, radio, televisheni , online n.k zimesheheni matamko ya viongozi .... mgomo wa Kariakoo tuliona tu habari ya maduka kufungwa lakini habari ya maandalizi ya mgomo hayakuandikwa hii ina maana hawakusikilizwa na viongozi wala media hadi maduka yalipofungwa kwa mgomo, je hii ni bahati mbaya au ni tabaka la viongozi, wasomi wanahabari kutosikiliza kero za wafanyabishara wa Kariakoo ....

Tumeona kwa majirani zetu jinsi ndoa ya uchawa baina ya viongozi, wasomi waandishi habari, private sector walivyopuuza habari za kero za wananchi kisha kizazi cha 'Gen Z' kilivyolipuka kiaina na nchi hiyo kuingia ktk matatizo .....atoa mfano Jaji Warioba

Sera inakuwa rahisi kukubalika ikiwa viongozi, wasomi ikiwemo waandishi habari, private sector kuwauliza wananchi wanataka nini, vipaumbele vyao n.k badala ya tabaka lenu kujifungia kutunga sera halafu mkajidai mnaenda kuelimisha wananchi. Jaji Warioba anakiri alipokuwa kiongozi alijifunza mengi kutoka kwa wananchi, lakini sasa tabaka la juu la viongozi, wasomi wanadhani hawawezi kujifunza kutoka kwa wananchi .... jaji Joseph Warioba anawaasa tabaka hili la juu liliojitenga na wananchi....

Tanzania bila uchawa haiwezekani ipo damuni ......
 
Mwandishi kama mzee Mkumbwa Ally namfahamu tangia enzi ya hayati Mwalimu, wakti ule aliuliza masuali ya akili sana.

Labda amebaki Jenerali Ulimwengu tu

TAFAKURI YA NYAKATI ZETU

"A time is coming when men will go mad, and when they see someone who is not mad, they will attack him, saying, "You are mad; you are not like us."- St. Anthony the Great of Egypt

"Wakati unakuja ambapo watu watakuwa na wazimu, na wakimwona mtu asiye na wazimu, watamshambulia, wakisema, "Wewe ni wazimu; wewe si kama sisi."
- Mtakatifu Anthony Mkuu wa Misri
 
Juzi nipo mahala namsikiliza one of the most senior civil servant wa UK akiongelea kuhusu transfer of power baina ya new PM na yule Rishi, akasema kwa wao (civil servants) huakikisha hakuna changes zozote ambazo zitaathiri maslahi ya taifa zitazingatiwa, regardless ni chama gani chaingia madarakani.

Halafu akasema "issues of state-craft require great deliberation bila kufafanua zaidi.

Hawa watu kama huna nchi huyumba sana. Hukaa mafichoni sana lakini huongea kwa kalamu pekee yenye wino mwingi.

Ndo maana kuna mada nyingi nimechangia kuwa madam president ahitaji special advisers wenye ujuzi.
Katibu mkuu mwenyewe anaitwa (Permanent Secretary) hiyo title sio ya kujifurahisha tu ni kweli ukifika nafasi hiyo uwezi tolewa na mtu mpaka umri wa kustaafu au uachie mwenyewe.

Na kufikia nafasi hiyo succession planning yake na performance appraisal sio ndogo.

Kwa kifupi senior civil servants wana hold strategic position za nchi to explain how they operate in line with the republic thinking and how western government structure their civil services hiyo sasa ni political degree au kusoma vitabu kadhaa.

But the ukishaelewq unakuwa na expectations za government behaviour kama kuna hao wataalamu waliotengenezwq kwa misingi ya hiyo philosophies, awawezi fanana wa kila nchi kutokana na mataifa kupishana vipaumbele, but there is a standard of decision making.

Ukimsikiliza raisi Samia hana hao wataalamu.
 
Labda amebaki Jenerali Ulimwengu tu

TAFAKURI YA NYAKATI ZETU

"A time is coming when men will go mad, and when they see someone who is not mad, they will attack him, saying, "You are mad; you are not like us."- St. Anthony the Great of Egypt

"Wakati unakuja ambapo watu watakuwa na wazimu, na wakimwona mtu asiye na wazimu, watamshambulia, wakisema, "Wewe ni wazimu; wewe si kama sisi."
- Mtakatifu Anthony Mkuu wa Misri
Mkuu, kipo kitabu cha The Prince ameandika Nicollo Machiavelli aongelea namna ya kutwaa madaraka na kuyamudu kuhakikisha hayachomoki kama samaki kambare.
 
Katibu mkuu mwenyewe anaitwa (Permanent Secretary) hiyo title sio ya kujifurahisha tu ni kweli ukifika nafasi hiyo uwezi tolewa na mtu mpaka umri wa kustaafu au uachie mwenyewe.

Na kufika hiyo nafasi succession planning yake na performance appraisal sio ndogo.

Kwa kifupi senior civil servants wana hold strategic position za nchi to explain how they operate in line with the republic thinking and how western government structure their civil services hiyo sasa ni political degree au kusoma vitabu kadhaa.

But the ukishaelewq unakuwa na expectations za government behaviour kama kuna hao wataalamu waliotengenezwq kwa misingi ya hiyo philosophies, awawezi fanana wa kila nchi kutokana na mataifa kupishana vipaumbele, but there is a standard of decision making.

Ukimsikiliza raisi Samia hana hao wataalamu.
Uko sawa kabisa.

Na ndo maana nimetumia neno state-craft mtu aweza sema nini hii.

State-Craft ni utengenezaji wa taifa kimkakati kwa kutumia diplomasia na wakati mwingine jeshi.

Sasa watu washanaa kuona kwa mfano nchi kama Russia yawezaje kukabiliana na nchi zipatazo 50 peke yake kwenye mgogoro pale Ukraine. India, China, Brazil kote watumia hii state-craft.

Hiyo ndo state-craft unakuwa na kiongozi ambae asimamia uundwaji upya wa taifa, uimara wake na mwelekeo wake kijiografia.

Waandishi wa habari ni sehemu muhimu sana ya state-craft ni kwamba hawafahamu hilo na mzee Warioba kawakumbusha.
 
Mkuu, kipo kitabu cha The Prince ameandika Nicollo Machiavelli aongelea namna ya kutwaa madaraka na kuyamudu kuhakikisha hayachomoki kama samaki kambare.
Sio book readers hawa

Ni watu wa kusikia na kusimulia engineer kasema SGR itachukua muda huu.

But themselves can’t deduce the merit of the argument nor have the time to analyse and evaluate the engineering factors nor the finance factors.

Uanze kuongelea the prince na changamoto za Machiavelli hadi kuwa power broker wa Europę.

Simply hayo mambo wengi wetu Tanzania atuelewi what shaped siasa za wenzetu kwa sababu hata vitabu muhimu vilivyo shape siasa za dunia atusomi.

Yes I know not ideal talking, but sometimes you got to be unapologetic rather than entertain shallow thinking.
 
Sio book readers hawa

Ni watu wa kusikia na kusimulia engineer kasema SGR itachukua muda huu.

But themselves can’t deduce the merit of the argument nor have the time to analyse and evaluate the engineering factors nor the finance factors.
Yupo mzungu mmoja aliekuwa akitoa mhadhara mara baada ya JPM kuchaguliwa.

Akasema " We will monitor and evaluate the new government mechanism (how the government works) in doing things and will respond accordingly.

Umetumia analyze and evaluate, ni maneno muhimu sana kila unapoteta kuhusu leadership.
 
Huyu mzee kaongea vizuri sana, katika vitu vinanikera ni utambulisho wa kutaja kila mtu, unachukua nusu ya muda wa hotuba. Uanze na mh, raisi, utaje jina, makamu wa raisi, utaje jina, waziri mkuu, utaje jina, viongozi wote na unawataja kwa majina. Ni kero kubwa na inapoteza muda sana.

Fikiria kusoma budget ya wizara ya fedha ilichukua masaa mawili na ushee ila dakika 40 nzima ilikuwa utambulisho. Yaani theluthi koja ya muda yako unaitumia kutambulisha, sio sawa na hii ni kwa viongozi wote.

Kujipendekeza kunatumaliza kama taifa.
 
Uko sawa kabisa.

Na ndo maana nimetumia neno state-craft mtu aweza sema nini hii.

State-Craft ni utengenezaji wa taifa kimkakati kwa kutumia diplomasia na wakati mwingine jeshi.

Sasa watu washanaa kuona kwa mfano nchi kama Russia yawezaje kukabiliana na nchi zipatazo 50 peke yake kwenye mgogoro pale Ukraine.

Hiyo ndo state-craft unakuwa na kiongozi ambae asimamia uundwaji upya wa taifa, uimara wake na mwelekeo wake kijiografia.

Waandishi wa habari ni sehemu muhimu sana ya state-craft ni kwamba hawafahamu hilo na mzee Warioba kawakumbusha.
Hao watu wana long term vision za nchi zao (a lot of thinking goes into comparative advantages and disadvantages) that includes production capabilities, technology, economy, security and so forth..

In attaining those goals wanaangalia global challenges zao how best to mitigate those risks.

Sasa kama ku-achieve hizo goals wanahitaji allies, they have to do so; kila kitu kinafikiriwa kwa muda mrefu. Uwezi kumtegemea Donald Trump, Putin, Biden au sijui nani kwa mipango ya nchi ya miaka 20 mpaka 50 mbele. Unahitaji kutengeneza civil services itakayo isimamia hata kije chama gani.

Ndio msingi wa civil servants wengi kuwa sehemu ya usalama wa taifa kwa maslahi ya nchi.

Usingizi tena, hatuko hapo kwa bahati mbaya; ila ni kutokana na watu wasio weza endesha nchi.

Mfano mdogo tu kama watu wanaweza chepusha mafuta kutoka bandarini; halafu unasema unaulinzi ni kwa sababu auko vitani; vinginevyo ungejua umuhimu wa kulinda njia za mafuta na usalama wake ndio tungejua ni kiasi gani hilo swala ni security risk nchi nyingine.

Hakuna security services hapo kuna wambea tu.

Usalama wa taifa unaitwa ‘intellligence services’ kwa sababu ni mchezo wa watu wenye akili kwenye mipango.

Sasa Uwezi kuwa na afisa na usalama anaewaza kukaita katoto ka miaka 21 akakafungia kwenye gari na kukafanyia mambo ya ajabu halafu ukatumia nguvu kumlinda.

Hatuko hapo kwa sababu ye wazungu, ni kwamba hatuna uwezo tu ndio maana tupo hapo.
 
Mzee katoa hotuba iliyoshiba busara, wanaosema wananchi waelimishwe,unakuta anayeelimisha,
elimu yake juu ya analotolea elimu,ujuzi wake haujai hata kwenye kijiko.
Anajivunia polisi waliosimamia shoo. Kwa kweli tumefika pahali hata elimu inakosa thamani mtaani.
 
Tuna ideas za kuendesha nchi zulizopewa wakoloni na system za kukopi (kwa kukariri) bila ya kuelewa foundation zake na namna ya kuzi-implent kwa mazingira yetu.

Kazi ya kuongoza nchi sio nyepesi inataka serious technocrats wa watu walio elewa kitabu cha Plato Republic not the ‘allegory of the cave’ that was not political.

But the ‘metaphor’ of population decision; leading to the appointment of philosophers king and their role in running a country.

Kupitia hiyo metaphor ndio msingi wa nchi zilizoendelea leo kukubali kuwa na wanasiasa darasa, Iła sio services especially at senior posts inayopwaya.

Senior civil posts are serious nchi za wenzetu uwezi pata mkuu wa mkoa analawiti watoto; kama kuna scandal ya uongozi kwa ngazi ya juu hasa ya hivyo
basi inamuhusu nwanasiasa, sio senior servants.

Kuelewa kwanini soma Plato republic.

Kwa nchi yetu hata kwa speech na maamuzi ya raisi Hakuna walinzi wa nchi kwa mujibu wa Plato.
Wewe ni mmoja wa aliyezunguziwa na Warioba, humu kuna wananchi wa aina mbalimbali ila bado unatumia maneno yanayochanganya lugha mbalimbali bila kujua kama unamfikishia nani taarifa au unawafikishia wasomi vs wasomi!! Warioba yeye amesema Viongozi wanawasiliana wao kwa wao na kuwachukulia mawazo ya wananchi kama kero.
Ebu jaribu kufikisha taarifa yako kwa lugha rahisi ili kila mtu apate kukuelewa, usifanye kama usomi wako wa kitabu cha Plato hakijakuwezesha kuitafsiri kwa lugha rahisi.
 
View: https://m.youtube.com/watch?v=oLU-Evdlt-A&pp=ygUaeWVzIG1pbmlzdGVyIGZ1bGwgZXBpc29kZXM%3D

Not sure kama kuangalia hizo series YouTube zinataka VPN.

Ila hiko kipindi cha ‘Yes Minister’ series zote hadi kufikia ‘Yes Prime minister’ ni kama 60% ya uhalisia wa namna U.K. government inavyoendeshwa.

Sio kipindi cha watu wasiojua siasa za nchi zinavyo takiwa, but very educational kwa siasa za uingereza.

Binafsi post hii naichukulia kama zingine za kutwanga maji kwenye kinu. Kwa sabsbu kuelewa inataka uelewa wa role ya civil services na politicians.
 
Wewe ni mmoja wa aliyezunguziwa na Warioba, humu kuna wananchi wa aina mbalimbali ila bado unatumia maneno yanayochanganya lugha mbalimbali bila kujua kama unamfikishia nani taarifa au unawafikishia wasomi vs wasomi!! Warioba yeye amesema Viongozi wanawasiliana wao kwa wao na kuwachukulia mawazo ya wananchi kama kero.
Ebu jaribu kufikisha taarifa yako kwa lugha rahisi ili kila mtu apate kukuelewa, usifanye kama usomi wako wa kitabu cha Plato hakijakuwezesha kuitafsiri kwa lugha rahisi.
Asante mkubwa

Ila post zingine ni kwa ajili ya wanasiasa tu na wenye uelewa (sio lazima wa degree) but curious minds.

Ata huyo Plato kitabu chake akikumlenga kila mtu isipokuwa wenye madaraka miaka hiyo.

Republic original kina page zaidi ya 2000 na mambo kibao, leo kuna version kadhaa simplified (and the language is not easy). Thanks god to the internet.

Kitabu chenyewe ni dialogue (discussion) na kuna maneno magumu humo ya kizungu na philosophical explanations sio cha mtu wa kawaida kukielewa (including me I relied so much on google help).

Ndio maana nasisitiza wasomi wakisome na kukielewa sio kitabu cha kila mtu.

Basically Plato humo ndani anakumbushia discussion yake (na familia yake wakiwa na Socrates) sio kitabu chepesi kabisa kukidadavua kwa mtu asie na abc za siasa kwa mtazamo (wangu) aina maana hiyo kazi sio nyepesi kwa wengine.

Binafsi kuna concept kuzielewa kwa kina pamoja na kusoma kitabu imebidi niiingie you tube kuwasikiliza political philosophers. It’s not an easy book at least kwa uwezo wangu mdogo.

But personal naamini uwezi kushika nyazifa nyeti za siasa au civil services bila kusoma ‘Plato republic’, Machiavelli the prince’ and Aristotle Politics.
 
Back
Top Bottom