Jaji Warioba: Viongozi na wanahabari acheni uchawa mnaumiza wananchi
Mkuu Jemima Mrembo , kitendo cha kunifananisha mimi na hawa machawa wa humu, sio kunitendea haki, ni kama kunitukana!, kumtukana mtu mwenye umri wa mzazi wako, ni kujitafutia balaa!, lakini kwa vile mimi japo umri umesonga lakini napenda warembo, nimekusamehe!, usirudie kunifananisha mimi na hawa machawa wa humu..
Kuna kusifia kwa sifa za ukweli, na kuna kusifia kwa uchawa, ili kujua namna ya kutofautisha, karibu pande hizi, Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza! mfano kuna machawa kibao wa Samia humu, mtu kama huyu, anayethubutu kumwambia Samia jambo kama sauti HII huwezi kumuita chawa!!.
P
 
Akizungumza mbele ya Media Council of Tanzania, waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba


View: https://m.youtube.com/watch?v=MvpysrliGgU



Ninatazama bunge la Dodoma, imekuwa fasheni kila mbunge kuanza mchango wake wa hoja kwa kutaja na kumsifia rais.

Vyombo vya habari kwa nyakati ya sasa hivi badala ya kutoa habari vimegeuka kuwa vyombo vya propaganda yaani uchawa ...

Woga umetamalaki kwa kisingizio cha self censorship/ nidhamu ya woga, hakuna habari za kiuchunguzi yaani zili zilizofayiwa research kwa kuogopa zinaweza kuwa kinzani na uchawa uliopo anasema Jaji Joseph Sinde Warioba ...

Waziri mkuu mstaafu anabainisha kuwa mwaka 1961 alifanya kazi na chombo cha media cha The Standard kabla ya kujiunga na masomo ya juu ya Chuo Kikuu. Hivyo anakumbuka viwango vya uandishi wa habari enzi hizo, na kulinganisha na hivi sasa ambapo yeye ni sehemu ya consumer society yaani walaji na anaona mapungufu makubwa ya viwango vya uandishi na utoaji habari ... kutokana na woga kuwakaba Media na hata viongozi..

Jaji Joseph Sinde Warioba anasema aliteuliwa katika Tume ya Haki Jinai kisha pia kuingizwa ktk Kamati ya Kutekekeza Mapendekezo ya Tume. Huko pia aliona woga wa wananchi ambao wengi hawataki kutoa ushirikiano kwa vyombo vya Haki Jinai kama Polisi, TAKUKURU n.k kwa kuhofia kupata matatizo ...

Wananchi wanahitaji habari za kila aina siyo hizi za uchawa / propaganda pekee zinazobebwa na media zote kusifia au kupamba kinamna habari zinazopendwa kusikika na viongozi....anasema Jaji Warioba.


Nafahamu kika chombo cha habari kina editorial policy / sera za mwegemeo, lakini vyombo hivyo visiwe kama kasuku kwa kutoa habari zenye chanzo / source kimoja bali vifanye research / uchunguzi ili habari katika vyombo vya habari ziaminike na kuwa habari zenye kuweza kufanyiwa rejea au kunukuliwa kwa uhakika.... ..

Jaji Joseph Warioba anawasa waandishi habari nguli na wahariri waliojitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na Jukwaa la Wanahabari wa Tanzania / Media Council of Tanzania, kuwa tabia ya kuendekeza uchawa / propaganda haiwasaidi wananchi wala viongozi ....

Nchi hii imejenga matabaka mawili yaani la juu ni viongozi, private sector na ninyi wasomi waandishi wa habari / wahariri na kujitambulisha kama tabaka 'muhimu' .....

Na tabaka hili la kwanza hufanya mikutano ya 'viongozi' bila kushirikisha tabaka la wananchi. Na item / point ya kwanza badala ya kuanza na ajenda, utambulisho ndiyo unaanza kwa urefu sana dakika hadi 15 kutaja kila kiongozi ... na kuhitimishwa itifaki / protokali imezingati.....

Jaji Warioba anasema masuala ya Itifaki imezingatiwa alianza kuona na kusikia Nigeria ambapo wenzetu kule hutaja viongozi wawili tu na wengine wote huingiza ktk kundi la itifaki imezingatiwa. Lakini hapa kwetu Tanzamia kutokana na uchawa huwa tunataja viongozi wote na itifaki inazingatiwa ni kwa kundi la wananchi wasio viongozi...


Hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha ilichukua ilikuwa ya masaa 2 na dakika 6 baada ya hapo utambulisho ikichukua dakika 40 kuwataja viongozi waliopo ukumbini, lakini wakasahau kuwa nje ya ukumbi kuna wananchi wanasikiliza hawa hawakutajwaa kabisa wakati hii ni bajeti ya nchi siyo wa viongozi .. .Jaji Wariiba anasimulia kasumba hii ilivyoota mizizi ...

Hata hotuba zimekuwa watu wetu / wangu , zamani ilikuwa katika hotuba neno wananchi ndiyo limetamalaki anabainisha jaji Joseph Warioba kuonesha tabaka .... wananchi wamekuwa kama ni mali ya viongozi wakati wananchi ndiyo waliowaajiri viongoziv....

Kauli za wananchi waelimishwe baada ya kuanda sera au muswada inaukakasi asema Jaji Warioba. Ni kutokana na sisi tabaka la viongozi waanda sera kutowashirikisha wananchi toka mwanzo, kwa kuwa viongozi wanajiona wanahaki ya kuandaa muswada au sera bila kushirikisha umma, kisha wananchi waelimishwe..

Jaji Warioba anasema wanachofanya wananchi hakifahamiki, mfano angalia vichwa vya habari asubuhi ktk magazeti, radio, televisheni , online n.k zimesheheni matamko ya viongozi .... mgomo wa Kariakoo tuliona tu habari ya maduka kufungwa lakini habari ya maandalizi ya mgomo hayakuandikwa hii ina maana hawakusikilizwa na viongozi wala media hadi maduka yalipofungwa kwa mgomo, je hii ni bahati mbaya au ni tabaka la viongozi, wasomi wanahabari kutosikiliza kero za wafanyabishara wa Kariakoo ....

Tumeona kwa majirani zetu jinsi ndoa ya uchawa baina ya viongozi, wasomi waandishi habari, private sector walivyopuuza habari za kero za wananchi kisha kizazi cha 'Gen Z' kilivyolipuka kiaina na nchi hiyo kuingia ktk matatizo .....atoa mfano Jaji Warioba

Sera inakuwa rahisi kukubalika ikiwa viongozi, wasomi ikiwemo waandishi habari, private sector kuwauliza wananchi wanataka nini, vipaumbele vyao n.k badala ya tabaka lenu kujifungia kutunga sera halafu mkajidai mnaenda kuelimisha wananchi. Jaji Warioba anakiri alipokuwa kiongozi alijifunza mengi kutoka kwa wananchi, lakini sasa tabaka la juu la viongozi, wasomi wanadhani hawawezi kujifunza kutoka kwa wananchi .... jaji Joseph Warioba anawaasa tabaka hili la juu liliojitenga na wananchi....

Tatizo liko kwa anayesifiwa huku amedungwa mrija ila hajui kama anaumizwa
 
Mungu tulindie huyu mzee maana naona amebaki pekee kusemea tabaka la chini sisi tusio na sauti
 
Asante mkubwa

Ila post zingine ni kwa ajili ya wanasiasa tu na wenye uelewa (sio lazima wa degree) but curious minds.

Ata huyo Plato kitabu chake akikumlenga kila mtu isipokuwa wenye madaraka miaka hiyo.

Republic original kina page zaidi ya 2000 na mambo kibao, leo kuna version kadhaa simplified (and the language is not easy). Thanks god to the internet.

Kitabu chenyewe ni dialogue (discussion) na kuna maneno magumu humo ya kizungu na philosophical explanations sio cha mtu wa kawaida kukielewa (including me I relied so much on google help).

Ndio maana nasisitiza wasomi wakisome na kukielewa sio kitabu cha kila mtu.

Basically Plato humo ndani anakumbushia discussion yake (na familia yake wakiwa na Socrates) sio kitabu chepesi kabisa kukidadavua kwa mtu asie na abc za siasa kwa mtazamo (wangu) aina maana hiyo kazi sio nyepesi kwa wengine.

Binafsi kuna concept kuzielewa kwa kina pamoja na kusoma kitabu imebidi niiingie you tube kuwasikiliza political philosophers. It’s not an easy book at least kwa uwezo wangu mdogo.

But personal naamini uwezi kushika nyazifa nyeti za siasa au civil services bila kusoma ‘Plato republic’, Machiavelli the prince’ and Aristotle Politics.
Mkuu umenifikirisha sana, unamaanisha kuwa hawa viongozi wetu mawaziri wamesoma Plato Republic yenye BOOK I -BOOK X? au umaanisha nini?
Napenda kusoma vitabu sana, nilipomaliza sekondari school kidato cha nne kitabu cha kwanza kusoma nikiwa nasubiri kwenda High school kilikuwa ni Rugged Constitution ikizungumzia jinsi Katiba ya Marekani ilivyoundwa miaka miaka hiyo 1789 kama sijakosea.
 
CCM chama hilo halina ubishi ila saa zingine lazima tuwape ukweli wao kwa faida ya jamiii.
Ccm kama Chama haina tatizo ila tatizo ni wale waliojipenyeza humo kwa nia zao za kujilimbikizia mali ndio shida !
Wale CCM Asili hawana tena chao humo kwa sababu hawana maokoto ya kumwaga 🙄😳😳
 
Mzee Warioba ndio Mzalendo pekee mwenye alikuwa na Wadhifa mkubwa katika Nchi hii ambaye huwa anazungumza vitu vya kweli kabisa bila kuwa na hofu
 
Mkuu umenifikirisha sana, unamaanisha kuwa hawa viongozi wetu mawaziri wamesoma Plato Republic yenye BOOK I -BOOK X? au umaanisha nini?
Napenda kusoma vitabu sana, nilipomaliza sekondari school kidato cha nne kitabu cha kwanza kusoma nikiwa nasubiri kwenda High school kilikuwa ni Rugged Constitution ikizungumzia jinsi Katiba ya Marekani ilivyoundwa miaka miaka hiyo 1789 kama sijakosea.
Don’t know the book you are talking about (though I have a read a couple of books on US political principal and keep them as reference). The building block.

Kwa hawa watu hata watu ivyo vitabu vya siasa at foundation level ukiwasikiliza unaona kabisa hawaja soma na hapa (namzungumzia Dr. Bashiru) though I love him kwa sababu zingine.

Kuna vitabu luluki vya siasa at foundation level, hawa watu hata hizo concept kuzielewa shida kwao (nazungumzia a majority of senior politicians) huo ndio uhalisia.

Ukija huko kwa Plato ni maswala ya strategies wana olewa political philosophy na uelewa huo nafasi zake ni strategic pia.

Kwa siasa zetu hakuna hao watu, kwa sababu wanatakiwa kutengenzwa ni story ndefu.

Tunafanya hayo mambo kwa kufundishwa ila bila ya kuelewa walimu wetu, wame copy kwa Plato na msingi wake ni nini.
 
Ccm kama Chama haina tatizo ila tatizo ni wale waliojipenyeza humo kwa nia zao za kujilimbikizia mali ndio shida !
Wale CCM Asili hawana tena chao humo kwa sababu hawana maokoto ya kumwaga 🙄😳😳
Ndugu CCM chama ambacho hakina mpinzani.

Na hakuna chama kisicho na wahuni wachache wenye kusaka mali.

Ni vipi CCM inalea hao wahuni Ndio shida.

Iła CCM chama kulinganisha na upupu uliopo vyamq vya upinzani.
 
Kwa miaka zaidi ya 30 Warioba alikuwa anakula nchi, kwa kutumia katiba hii hii, hakuwahi kumwambia lolote Nyerere kwamba katiba ni mbaya. Alikuwa "chawa" mtiifu. Ni yeye ndiye alikuwa mwanasheria mkuu aliyekuwa akipeleka bungeni sheria kandamizi, ikiwemo ya kuweka watu kizuizini bila kupelekwa mahakamani.
Anayoyasema ni ya kweli au uongo? kama alikosea huko nyuma asiseme ukweli?
 
Siku hizi twaona cheo cha katibu mkuu wa wizara chachezewa hovyo bila ridhaa yake.

Katibu mkuu wa wizara ni mtu ambae ni wa kudumu kwa maana kwamba hungalia transfer ya viongozi mbalimbali na kuwafundisha kazi wanapokuja kwenye wizara.

Ndo maana siku hizi twaona baadhi ya mawaziri wachukua hatua za ajabu na kuamua masuala mengine yalo juu ya uwezo wao wakisahau kuwa yupo katibu mkuu wa wizara ambae utaomba ushauri wake kama "senior civil servant" wako.

Ndo maana ya kuwa na permanent secretary wa wizara yoyote ile.
Hao Makatibu Wakuu wenyewe wanateuliwa vilaza wasio wa mbele wala nyuma. Unategemea tutakuwa na Civil Service imara?
 
Katibu mkuu mwenyewe anaitwa (Permanent Secretary) hiyo title sio ya kujifurahisha tu ni kweli ukifika nafasi hiyo uwezi tolewa na mtu mpaka umri wa kustaafu au uachie mwenyewe.

Na kufikia nafasi hiyo succession planning yake na performance appraisal sio ndogo.

Kwa kifupi senior civil servants wana hold strategic position za nchi to explain how they operate in line with the republic thinking and how western government structure their civil services hiyo sasa ni political degree au kusoma vitabu kadhaa.

But the ukishaelewq unakuwa na expectations za government behaviour kama kuna hao wataalamu waliotengenezwq kwa misingi ya hiyo philosophies, awawezi fanana wa kila nchi kutokana na mataifa kupishana vipaumbele, but there is a standard of decision making.

Ukimsikiliza raisi Samia hana hao wataalamu.
Uko sahihi kabisa. Nimependa mchango wako.

Huku tuna makatibu wakuu naskia wanakimbizana kwenye matukio ya kuzionesha Wizara zao kwenye vyombo vya habari ili tu waonekane na Rais wanafanya kazi.

Wameacha kabisa mambo ya msingi kwenye Wizara zao ikiwemo kusimamia sera na kutengeneza sera zinazohakikisha nchi inakuwa na maendeleo ya uhakika siku za mbeleni.

Tuna Makatibu Wakuu ambao hawajui hata vision ya nchi ikoje. Imefika wakati huoni tofauti kati ya Permanent Secretary na Mwanasiasa

Tuna safari ndefu sana Tanzania.
 
Back
Top Bottom