Naomba uanzishe thread special kuhusu hili jambo. Tujadili humu watu waone tulivyo na dead Civil Service nchi hii ambayo inafanya future yetu kama Taifa kuwa hatarini sana
 
hawa wazee waache unafiki na kutaka waonekane kama walifanya mazuri enzi zao.

maisha ya wananchi yalikuwa magumu sana wkt wao wanatawala na kula keki ya nchi.

ajue tu uchawa haukuwezekana wkt wa utawala wao sio kwa sababu walifanya mazuri. ni big NO.

ni kwa sabab serikali ilikuwa ya kiimla/ kidikteta watu walinyamazishwa kuongeza.

usingeweza kuiongelea serikali kwa kuiokosoa na ukabaki salama kwa miaka iyo, kwanza hakukuwa na iyo platform ya kuongelea maana media zote zilikuwa za serikali au chama
 
Huyu mzee ni azina kwa Taifa, akitumiwa vizuri na viongozi wenye nia njema na hili taifa, lakini ndo hivovwanmpiga nakofi.
Pascal Mayalla , Tlaatlaah na Luka mna la kujifunza hapa wazee wangu wa hovyo.
 
Waandishi wa habari ni sehemu muhimu sana ya state-craft ni kwamba hawafahamu hilo na mzee Warioba kawakumbusha.

Hawajielewi kama wao ni mhimili wa nne ktk dola, wameamua kuwa sehemu ya watawala kwa sababu ya woga au uchawa.

Utakuta wanalaumu vyama vya upinzani kuwa havitoshi kwa kuandika makala au kujadili ktk radio/ televisheni wakitumia uchawa (propaganda) kuwa CCM ibaki milele ili nao waendelee kufaidi makombo wanayosaza watawala waliopo.

TOKA MAKTABA:

21 May 2024
LIVE: WAZIRI MKUU MAJALIWA AKISHIRIKI KONGAMANO LA WANAHABARI WA MITANDAO YA KIJAMII JUMUKITA


View: https://m.youtube.com/watch?v=gXavFSYiS5c&pp=ygU3S09OR0FNQU5PIExBIFdBTkFIQUJBUkkgV0EgTUlUQU5EQU8gWUEgS0lKQU1JSSBKVU1VS0lUQQ%3D%3D
 
Uchawa ni adui mkubwa wa ustawi kwa Taifa hili. Machawa wamekuwa mazezeta. Hawaongei kitu chochote cha maana zaidi ya kusifu.

Fikiria ungekuwa ndugu wa mtu kama Mwashambwa au Variable, si ungeona ni laana imeingia katika familia au ukoo? Nani angependa awe na ndugu wa namna Ile. Na hizi ni sampuli za waliopo mtaani. Kwa aina za watu kama hao, utasema kweli una Taifa?
 
Mzee kasema kweli kabisa,Haya mambo si ya kutafumbia macho kamwe!
 
Duuh Kali mno!
 
Ooh nashukuru sana mke wangu na watoto wangu kwa kunivumilia ninapokuwa kwenye majukumu!Si uache kama wanaona kazi ngumu hao wanao na mkea,Inaboa.
 
Pole mkuu,inawezekana uchawa ni kila mtu Sasa anayesifia!
 
Uchawa ni laana.
Lakini hili swala la "uchawa" sasa lina changanya.
Nikiangalia kwa karibu zaidi, "uchawa wa vyombo vya habari na waandishi" sioni tofauti yake na "RUSHWA"- Hawa uchawa wao ni kupewa rushwa toka serikalini.

Enzi za Magufuli, vyombo hivi hivi na waandishi wake walitekwa zaidi na "woga" na vitisho vya kunyimwa matangazo.
Waandishi wengi hadi leo wanaandika ili wapewe vyeo, kuteuliwa kuwa wakuu wa Wilaya na kwingineko

Kuandika habari za kuihoji serikali na viongozi hailipi.

Nchi nzima, tumegeuzwa hivyo hivyo, hata huku mitaani. Ukitaka mambo yako yakae sawa, inakubidi uwe chawa!
 
Pascal Mayala namtetea sio chawa
Nakumbuka ndo aliuliza swali lenye akili enzi za Magufuli aliyekuwa na viashiria vya udikteta
Baada ya hapo, taasisi ya Pascal Mayalla ya PRRR ilikosa kabisa kazi/ biashara, akakutana Na rejection ya hali ya juu, njaa ikampiga vibaya. Baada ya hapo akajiunga Na timu ya CHAWA wa Magu Na baadae akahamia timu ya chawa wa mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…