Jaji Werema: Tumepitia magumu awamu ya 5, Katiba Mpya ni muhimu

Jaji Werema: Tumepitia magumu awamu ya 5, Katiba Mpya ni muhimu

Usomi wa Tanzania ni bure kabisa, mtu kama huyu na elimu yake alikuwa anaogopa kuzungumza mpaka mzee afe? Msomi hana ujassili Namna hii?
 
Nimeangalia kwenye hii picha kama kuna Werema simuoni??

IMG-20141224-WA0001.jpg
 
Ccm na serikali wanajifanya kuwa wao ni Wananchi wasio ona umuhimu wa katiba kwamba wao Wanataka maendeleo, na kwamba eti wao (ccm na serikali) hawajaitaka katiba mpya.

Huu ni ujanja wa kutufanya sisi Wananchi halisi kuwa ni wajinga,

Hivi ni kweli kuwa wamesahau tulivyopigwa na jua mchanga kuitwa kutoa maoni yetu kupitia kwa mh jaji Warioba.

Hao Wananchi wanaotaka wawaonyeshe kwamba wanatoa maoni ya hitaji wa katiba Wanataka watumie njia gani?

Au mpaka waandamane kwa vurugu kama nchi zingine ndipo muone wingi wake?

Basi kama ni hivyo ruhusuni makongamano au maandamano muwaone vizuri.
Mkuu hawa watu wako kama manyani. Manyani ndiyo kila inyeshapo mvua utasikia yanagugua ..''mh kesho lazima tujenge nyumba, kesho lazima tujenge nyumba''. Mvua inapoacha nayo yanasahau. Sasa hivi waliokuwa wanalia kipindi cha Magufuli (kina Makamba, Zitto, Kinana, Kikwete); wameshasahau tayari kilichowapata na hawaoni umuhimu wa katiba. Wale waliokuwa wanatamba wakati wa Magufuli (kina Polepole etc,) ndiyo zamu yao, wanalialia sasa hivi.
 
Nafikiri mjadala wa katiba mpya unaelekea pazuri na labda kuchelewa kwetu kutatupa katiba iliyo bora zaidi.
 
Nyerere ndio wakulaumiwa kwa kutanguliza ubinafsi wake kwa kutuletea katiba hii. Na yeye alikiri kbs kuwa katiba tuliyo nayo endapo akaja rais kichaa anaweza kufanya anavyotaka yeye. Ya awamu ya Tano tumejionea.
 
Kwani aliyezoea vya kunyonga huhitaji vya kuchinja? Unataka waruhusu mwisho wao wa madaraka
 
JK na Mzee Mizengwe Bend hawakuamini kwamba mzaha wao juu ya katiba mpya uliwatesa hata wao pia
 
Ukweli ni ukweli tu bila kujali unasema wakati gani. Ukweli unaishi
 
Back
Top Bottom