Jaji Winfrida Korosso: Sheria zilizopitwa na wakati ni chanzo cha hasira kwa vijana

Jaji Winfrida Korosso: Sheria zilizopitwa na wakati ni chanzo cha hasira kwa vijana

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Jaji wa Mahakama ya Rufani Winifrida Korosso, amesema kuwa sheria nyingi zilizopo nchini hazilingani na mazingira ya sasa na baadhi yake zimekuwa chanzo cha migogoro katika jamii, ikiwemo kuongeza hasira na malalamiko miongoni mwa Vijana kutokana na kuona upendeleo na kutopewa fursa sawa.

Jaji Korosso ameeleza hayo jijini Dodoma wakati wa ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Zuberi Juma Homera, alipotembelea ofisi za Tume hiyo zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).



Amesema baadhi ya Sheria, hususani zinazohusu masuala ya jinai kama dhamana, zimekuwa zikisababisha kuwepo kwa kesi nyingi ambazo zinaathiri maisha ya watu moja kwa moja. Amebainisha kuwa changamoto hizo zimekuwa zikichangia ongezeko la hasira kwa Vijana

Aidha, amegusia changamoto katika umiliki wa ardhi kwa Vijana, akisema idadi kubwa ya Vijana wanakosa fursa ya kumiliki ardhi, jambo linaloongeza msongo na malalamiko, na kuongeza kuwa masuala ya mirathi yamekuwa yakiwaumiza Vijana na Watoto wengi kutokana na baadhi ya watu wachache kuwanyima haki zao.

Mbali na hayo, Jaji Winifrida amesema kuwa Sheria ya Ndoa ni miongoni mwa sheria zinazohitaji kufanyiwa marekebisho kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom