Jakaya Kikwete akiwa na Timu ya mpira wa kikapu Dar City nchini Afrika Kusini

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Nilishasema Sana Humu jukwaani na kula sehemu hapa Nchini kuwa Rais Samia ni Chaguo la Mungu Aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu na kuwekwa Hapo Alipo kwa kibali maalumu cha Mwenyezi Mungu Mwenyewe.

Rais Samia akikupatia Baraka na kukutakia Heri ni lazima ufanikiwe,ni lazima ubarikiwe ,ni lazima ushinde vita yako ,ni lazima usonge mbele kwa ushindi ,ni lazima uibuke kidedea ,ni lazima uibuke shujaa ,ni lazima. Rais Samia Ni Mama na kiongozi Ambaye ulimi wake na mikono yake imejaa baraka tupu.

Sijapata kuona Rais Mwenye kibali cha Mwenyezi Mungu kama alichonacho Rais Samia . Yaani sijui niseme nini juu ya Rais Samia ili Mpate kunielewa. Huyu Siyo kiongozi wa kawaida . Anaye Mungu ndani yake. Sasa Embu oneneni Dar city huko bondeni inavyofanya vizuri na kuwapa tabasamu na furaha mamilioni kwa mamilioni ya mashabiki wa mpira wa kikapu Ulimwengu kote.

Embu soma hapa👉“Mhe. Rais Mstaafu Kikwete na Dar City Afrika Kusini”

Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders - POE), na Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika katika juhudi za kutatua mgogoro wa Sudan Kusini, amekutana leo na Timu ya Mpira wa Kikapu ya Dar City inayoshiriki Michuano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (Basketball Africa League (BAL) 2026, inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Katika mazungumzo na Timu hiyo iliyoambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabit pamoja na Viongozi wengine kutoka Serikalini, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ameipongeza Timu ya Dar City kwa kufikia hatua hiyo muhimu ya Mashindano, akieleza kuwa mafanikio hayo ni ishara ya kukua kwa kiwango cha Mpira wa Kikapu nchini Tanzania.

Aidha, amewatia moyo na kuwapa ari Wachezaji wa Dar City kupambana katika Mchezo wao unaofuata mnamo tarehe 31 Machi, 2026 kabla ya kufika fainali, akisisitiza umuhimu wa nidhamu, kujituma na kujiamini wanapoingia Uwanjani. "Kwa hatua mliyofikia, nina imani kabisa mnaweza kutinga Fainali na hatimaye kubeba Kombe hili", alisema Dkt. Kikwete akizungumza na Wachezaji hao.

Rais Mstaafu Dkt. Kikwete, ambaye amewahi kuwa Mlezi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) huku akiwa mstari wa mbele katika kuendeleza Mchezo huo wakati wa Uongozi wake, ametumia fursa hiyo pia kutoa pongezi kwa dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Uwekezaji mkubwa unaofanyika katika Sekta ya Michezo nchini. Aidha, ameipongeza Wizara yenye dhamana ya kusimamia Michezo pamoja na Shirikisho la TBF kwa kusimamia vizuri maendeleo ya Mpira wa Kikapu, huku akibainisha kuwa mafanikio ya Timu ya Dar City ni ya Watanzania wote.

Mheshimiwa Dkt. Kikwete yupo nchini Afrika Kusini kwa Ziara ya Kikazi ambapo tarehe 29 Machi, 2026 alikutana na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, kama sehemu ya kutekeleza majukumu yake ya Kikanda akiwa kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la SADC, pamoja na jukumu lake jipya chini ya Umoja wa Afrika la kusaidia kutafuta suluhu ya Mgogoro wa Sudan Kusini.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Screenshot_20260330-205706_1.jpg
 
Hiyo timu haishindi tena mechi yoyote,hiyo jamaa akishatembelea timu lazima itolewe kwenye mashindano
 
Haya yote kayataka mello,eti tumewawekea sehemu ya report, jitu kama hili mawazo yako makalion* ukilitukana matusi mazito utakuwa unakosea kweli!!!??
 
Kulingana na aina ya mwili wa Msoga E0359 anaonekana kuwa na tatizo la Figo na maumivu upande mmoja hivyo analazimika kupindia upande mwingine ili kubalance maumivu

Ungana na Luluvi Godfather.
 
Madaktari wa Magonjwa ya akili mliopo hapa jf mkimuacha huyu mwehu namna hii iko siku atakuja kumwaga haja kubwa hapa jukwaani

Chukueni hatua haraka
Dogo hunaga akili kabisa . Embu rudi unyakyusani huko ukalage hata ndizi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nilishasema Sana Humu jukwaani na kula sehemu hapa Nchini kuwa Rais Samia ni Chaguo la Mungu Aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu na kuwekwa Hapo Alipo kwa kibali maalumu cha Mwenyezi Mungu Mwenyewe.

Rais Samia akikupatia Baraka na kukutakia Heri ni lazima ufanikiwe,ni lazima ubarikiwe ,ni lazima ushinde vita yako ,ni lazima usonge mbele kwa ushindi ,ni lazima uibuke kidedea ,ni lazima uibuke shujaa ,ni lazima. Rais Samia Ni Mama na kiongozi Ambaye ulimi wake na mikono yake imejaa baraka tupu.

Sijapata kuona Rais Mwenye kibali cha Mwenyezi Mungu kama alichonacho Rais Samia . Yaani sijui niseme nini juu ya Rais Samia ili Mpate kunielewa. Huyu Siyo kiongozi wa kawaida . Anaye Mungu ndani yake. Sasa Embu oneneni Dar city huko bondeni inavyofanya vizuri na kuwapa tabasamu na furaha mamilioni kwa mamilioni ya mashabiki wa mpira wa kikapu Ulimwengu kote.

Embu soma hapa👉“Mhe. Rais Mstaafu Kikwete na Dar City Afrika Kusini”

Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders - POE), na Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika katika juhudi za kutatua mgogoro wa Sudan Kusini, amekutana leo na Timu ya Mpira wa Kikapu ya Dar City inayoshiriki Michuano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (Basketball Africa League (BAL) 2026, inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Katika mazungumzo na Timu hiyo iliyoambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabit pamoja na Viongozi wengine kutoka Serikalini, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ameipongeza Timu ya Dar City kwa kufikia hatua hiyo muhimu ya Mashindano, akieleza kuwa mafanikio hayo ni ishara ya kukua kwa kiwango cha Mpira wa Kikapu nchini Tanzania.

Aidha, amewatia moyo na kuwapa ari Wachezaji wa Dar City kupambana katika Mchezo wao unaofuata mnamo tarehe 31 Machi, 2026 kabla ya kufika fainali, akisisitiza umuhimu wa nidhamu, kujituma na kujiamini wanapoingia Uwanjani. "Kwa hatua mliyofikia, nina imani kabisa mnaweza kutinga Fainali na hatimaye kubeba Kombe hili", alisema Dkt. Kikwete akizungumza na Wachezaji hao.

Rais Mstaafu Dkt. Kikwete, ambaye amewahi kuwa Mlezi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) huku akiwa mstari wa mbele katika kuendeleza Mchezo huo wakati wa Uongozi wake, ametumia fursa hiyo pia kutoa pongezi kwa dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Uwekezaji mkubwa unaofanyika katika Sekta ya Michezo nchini. Aidha, ameipongeza Wizara yenye dhamana ya kusimamia Michezo pamoja na Shirikisho la TBF kwa kusimamia vizuri maendeleo ya Mpira wa Kikapu, huku akibainisha kuwa mafanikio ya Timu ya Dar City ni ya Watanzania wote.

Mheshimiwa Dkt. Kikwete yupo nchini Afrika Kusini kwa Ziara ya Kikazi ambapo tarehe 29 Machi, 2026 alikutana na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, kama sehemu ya kutekeleza majukumu yake ya Kikanda akiwa kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la SADC, pamoja na jukumu lake jipya chini ya Umoja wa Afrika la kusaidia kutafuta suluhu ya Mgogoro wa Sudan Kusini.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.View attachment 3564742
Kwahiyo wanaofikiria tofauti wana kasoro? Anyway, tujidanganye wenyewe tu, ila ukweli una tabia ya kukataa kufunikwa chini ya kapeti...unakataa kabisa mambo ya funika kombe mwanaharamu apite
 
Haya yote kayataka mello,eti tumewawekea sehemu ya report jitu kama hili mawazo yako makalion* ukilitukana matusi mazito utakuwa unakosea kweli!!!??
Mungu akusamehe sana na kukuba Neema ya kubadilika.
Acha kumuhusisha Mungu kwenye upumbavu wako,hata Mungu anasema mwana mpumbavu ni mzigo kwa babaye.Mwanangu huwa una upumbavu mwingi sana ni basi tu wanasema hili ni jukwaa huru sisi wenye akili pamoja na matahira kama wewe wote tuna haki sawa humu ndani
 
raisi kikwete kama mwenzake raisi samia wote ma dr's, tanzagiza tumebahatika kutoa maraisi wenye Phds, ingawaje bado sijajua field walizofanyia Phd research zao lkn haijalishi, kudos kwao ...
 
Haya sasa ndio mambo yetu, yale mambo ya kusimamia masharika kusiwe na wizi wa kodi zetu kama CAG alivyosema sio vitu vyetu kabisa,

Mambo ya mifumo kusomana huu mwaka wa tano hamna kitu kinafanyika, hasara juu ya hasara watu wanapiga hela,

Sometimes ni aibu kuzaliwa Africa
 
Back
Top Bottom