Jakaya Kikwete na Ridhiwani, wageni rasmi kwenye sherehe za Jando na Unyago huko Msoga

Jakaya Kikwete na Ridhiwani, wageni rasmi kwenye sherehe za Jando na Unyago huko Msoga

sawa, swali je ridhwani alipelekwa unyago na raisi kikwete? au yeye ridhwani kama ana mtoto kampeleka kwenye huo unyago? jibu lake wewe mwenyewe unalijua kwamba ni no, sasa kwa nini huo unyago kama ni mzuri uwe kwa watoto wa wengine tu?
Hakuna mzazi anaelazimishwa kupeleka mtoto wake huko, na wala haukatazwi.

Ambae anataka kupeleka apeleke asiona kama kuna manufaa asipeleke

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Kutumia umaarufu wa Rais mstaafu katika hii jando, ni kurudisha nyuma fikra na maendeleo ya kisasa.. Kwanini, asitumie umaarufu kuleta kitu cha kisasa cha kimaendeleo kwa watu wao.... Ukiona mtu anajikita katika mila, kuna kitu analenga au anataka kukwepa... Hiyo ni kuwateka mawazo watu wa maeneo hayo... Hawa watoto ambao wanaonekana karibu miaka 10 , wangepewa ujuzi unaowasaidia katika maisha ya sasa, sio kuwaweka kwenye kambi ya jando kama hizo..
 
Inasikitisha sana, ndio maana kupata maendeleo Africa ni vigumu sana.
Mbona wazungu wana Mila zao mpaka leo na Bado wana maendeleo yaani uwa natamani kuwapiga makofi nyie wenye mawazo ya kijinga..
Mnaona bora kukumbatia Mila za wazungu na Sio mila zetu..

Mbona wao wana mila zao na hawazioni kama ni mbaya
 
ukitaka kujua kwa nini wanazima umeme na kutesa watu au kwa nini watoto albino hawakuwa protected na walitekwa kuuliwa na kukatwa viungo angalia tu matendo ya watawala wetu, hata umeme upo na na wanakata makusudi sababu ya matambiko, nina uhakika kwa 100% raisi mstaafu kikwete hakumpeleka ridhwani unyago kama alitairiwa alimpeleka hospitalini na nina uhakika kama ridhwani ana mtoto hakumpeleka unyago bali hospitalini and the question is kama unyago ni mzuri kwa nini wao wasipeleke watoto wao kwa nini utamaduni uenziwe na wengine tu?

nchi hii adui mkuu wa maendeleo ni uislamu wa tanzania ambao aidha haueleweki na wajiitao waislamu au wenyewe ni tatizo lkn mara nyingi uislamu hauwezi kuwa na tatizo kwani umetumika jamii nyingine kuleta maendeleo na ustaarabu hivyo tatizo ni waislamu wa tanzania na watu aina hii tunategemea watuvushe 20th century kweli?


Jitahidi kuondoa chuki zinazoleta giza katika fikra zako, umeziacha mpaka zinakutawala kiasi hueleweki unataka kusema nini.

You sound like you’re about to get a seizure. Pole.
 
21st century mnapromote unyago? what about kuwasha umeme watu wafanye kazi wajiari na kupata kipato?


Uko sahihi, umeme uwashwe saa 24 bila kukatika Kama hakuna national emergency.

Kuhusu kupromote Unyago karne ya 21 naona Kama hata watu wanachelewa sana, Unyago ulipaswa uwe lazima kwa kila kabila kuendana na mila na desturi zao.


KTY; Mila, Desturi na Tamaduni ndivyo vinavyotufafanua na kutukamilisha as individuals and societies in general. Ni zaidi ya muhimu.
 
Ila haka kamkoa ka pwani kana Mambo ya hovyo sana. Nmeshuhudia maeneo ya chalinze, msoga, mbonga, lugoba, mindu tulieni, makombe, kinzagu ni Mambo ya jando kutoa mwari na ushenzi wa shuguli za ovyo kila siku. Mkwere Yuko tayari afanye shughuri ya kutoa mwanae ambaye ashatolewa bikra kitambo wakati huo yeye analala kwa nyumba ya miti paa nyasi na analala kwa bed ya kamba.


Sio dhambi kuwa tofauti. Jamii ulimwenguni kote ni mkusanyiko wa watu/koo tofauti tofauti.

Tofauti zetu ndizo zinazotufanya binaadam/viumbe hai kufanana.

Hakuna mila, desturi ama Tamaduni bora wala dhaifu katika jamii husika kwa maana hizo kwao ni Sawa na miongozo ya maisha iliyorithiwa kizazi kwa kizazi na kudumu kutokana na Imani yao kwa kuleta ufanisi wanaouhitaji/wanaoutarajia.

Ndiyo misingi ya ujenzi wa jamii zao, ni muhimu kwao. Zinawahusu zaidi wao.
 
Unyago sio kukeketwa. Wanafundishwa mambo ya kawaida tuu ingawa mengine ni ya kikubwa zaidi. Mfano jinsi mtoto anavyopatikana, binti atajua kumbe hanunuliwi atamtoa mwilini mwake muda ukifika, usipekue pekue godoro la wazazi wako, usiingie chumbani kwa wazazi wako bila ruhusa, kuwaheshimu wakubwa wako na mengine mengi tuu
Binti gani saizi ambaye hajui mtoto anapatikana vip
 
Alifanyiwa, kumbuka kwenye unyago na jando jamii zote za kuanzia Mtwara, Lindi, Pwani n.k, suala la kupeleka mtoto kwenye jando (mtoto wa kiume) na unyago (mtoto wa kike ) ni "LAZIMA"

Kinachotofautisha kati ya masikini na tajiri ni maeneo ya kufanyia hayo matukio ya jando na unyago.

Huyu atafanyia porini huko na huyu atatafuta eneo lililojitenga na jamii ila kuna miundombinu ya kuishi, atafungiwa humo mtoto/watoto kwa kipindi kisichozidi mwezi huku akila elimu ya jadi, jamii, ndoa na kufanya ushirikina(matambiko).

Hilo tukio unaloliona ni sherehe ya kuhitimisha zoezi hilo baada ya kukaa kambini kwa takribani mwezi mzima bila kuonana na wazazi wao tofauti na yule anayewafunda na wale wanaowaandalia chakula.
Ila nimeona madogo wa 3 wana vitambi na viduku. Ina maana huko ni buffee na saloon kwa sana.
 
Ila nimeona madogo wa 3 wana vitambi na viduku. Ina maana huko ni buffee na saloon kwa sana.
Kwa tajiri ni kujiachia, huku pangu pakavu tia mchuzi unafurahia lishe siku ukitoka jandoni, ila ukiwa huko jandoni ni mwendo wa ugali dagaa wa kuchemshwa
 
Back
Top Bottom