Jakaya Kikwete: Usirithi adui ya mtu... Tengeneza Adui yako Mwenyewe, lakini...

Ndikwega

R I P
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,979
Reaction score
5,527
Akiwa anatoa hotuba ya Kumsimika Makamu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam. Prof. William Lazaro Anangisye, ametoa Mfano akiwa mwenyekiti wa CCM huko Mtwara akotokea Jeshini.

Aliambiwa... “Ukitaka Mambo yako yafanikiwe, Haki ya Mungu, Fulani na fulani kaa Mbali nao!

Mwishowe kasema, “Tengeneza adui Wako Mwenyewe” na akakumbushia "Za Kupewa Changanya na za Kwako (za Mbayuwayu).”

Kasema ishi na Mtu kama alivyo, tuchukuliane na madhafui ya kila mmoja!

Fundisho: Kuna Ujumbe bila shaka Umemfikia bwana yule, Ametengenezewa maadui pia hawezi Kuchukuliana Kama ilivyo kwa wanadamu hakuna aliyekamilika.

Vyeo ni vya Muda tu na Kitambo kifupi tutaishi na Jamii hii hii tunayoitesa tukiwa na Vyeo.

Big up Prof. Jakaya Kikwete.

 
Una haraka sana ya kuandika, na pia unafanya conclusion vile uonavyo, na sivyo alivyomaanisha yeye.

Yeye kamwambia anangisye, wewe unahamishia kwa MTU mwingine.

Isitoshe JK hakuwa mkiti wa chama, alikuwa katibu.

Na pia hajasema "tengeneza madui zako mwenyewe", kasema usitengeneze maadui kabisa.
 
Ulisoma mchepuo gani sekondary mkuu?
 

Wewe ndo una haraka ya kumjibu kama umetumwa kufanya
damage control...

Kikwete anajua ujumbe wake hasa unamlenga nani...
watu wa pwani wanaweza kumtukana mtu kwa kumsifia
 
Unamlaumu vipi kusema aonavyo yeye wakati na wewe umeconclude uonavyo wewe..??

Mwenye kujua AMEMAANISHA NINI NI JK MWENYEWE. Wewe wala yeye hamjui JK alimaanisha nn, so usimlaumu..!!
 
Unamlaumu vipi kusema aonavyo yeye wakati na wewe umeconclude uonavyo wewe..??

Mwenye kujua AMEMAANISHA NINI NI JK MWENYEWE. Wewe wala yeye hamjui JK alimaanisha nn, so usimlaumu..!!
ulitaka aseme anamwambia nani? mbayuwayu zakupewa changanya na zako
 
Mkuu hii ni fasihi kila mtu ana tafsiri yake.
 


Hili Fundisho ni XXXXXX

Ushaanza kutunga negative thinking tupu..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…