Jakaya Kikwete: Usirithi adui ya mtu... Tengeneza Adui yako Mwenyewe, lakini...

Jakaya Kikwete: Usirithi adui ya mtu... Tengeneza Adui yako Mwenyewe, lakini...

Someni hapa nyie mabwana & mabibi mashaka!

Hata yeye mama samia aliwahi kiri mbele ya JPM kuwa yeye(samia na majaliwa) walipata taabu sana mwanzoni mwa utawala wa JPM,walikuwa wanashangazwa namna JP alivyotaka waenende, anaongezea kuwa baada ya muda mfupi walimuelewa sana JPM,then wakajikuta aina ya utendaji anaoutaka ndiyo utendaji mzuri kabisaa
 
Hivi huyu Lisu pamoja na kuonekana ni mjuzi wa mambo mengi kuliko wengine( maana huwa namsikia kila wafayalo wengine linaitwa la kijinga) lakini siyo kweli kwamba tuna mu overate sana???

Ndio hivyo anapewa sifa kiasi ambacho hakuna anayeza kuwaza kwamba Lissu kaiua cdm baada ya kupata nafasi ya kuwa mgombea Urais 2020.

Wakati wa DR Slaa tulisaidia cdm mawazo yaliyo kimarisha kiasi cha kutosha. Waliponunuliwa na EL na CCM kumleta JPM tukaamua kwenda na JPM mpaka kifo kitakapo tutenganisha.

Sasa wengine tuna angalia nani na nani wataingizwa uongozi CCM. Wakileta za kuleta na kuouuza maono ya JPM kwa vile katwaliwa basi jua upinzani ukiwa makini utaenda kuiondoa CCM madarakani. Marehemu JPM ni kama alikuwa mpinzani ndani ya CCM mafisadi. Hivyo CCM mafisadi ikirudi, ukae ukijua CCM JPM kukitokea watakaotupwa nje wenye uthubutu basi kuchukua nchi hii kwa njia mbadala kama kuhamia na kuimarisha upinzani itakuwa kama kusukuma mlevi wa changaa vile.

Unaweza amini kuwa jana geti la Airport lilikuwa limesheni Jewii na bado wakaona wawanchie walalahoi wamsindikize mtu wao mpaka kwenye ndege??! Yako mengi ya kujifunza ndugu, Tanzania ya JPM si ile ya 2015 ya mafisadi tena.
 
Back
Top Bottom