Jakaya Kikwete: Wazee tulikataa kubadili Katiba muhula wa Urais kutoka miaka 5 kuwa miaka 7

Jakaya Kikwete: Wazee tulikataa kubadili Katiba muhula wa Urais kutoka miaka 5 kuwa miaka 7

Akiwa kwenye mahojiano na kipindi maalum cha Clouds leo aliyekuwa Rais wa awamu ya Nne Jakaya Kikwete amesema kuwa mchakato uliokuwa mgumu zaidi kwake ni kuzuia uhuni wa kubadili muhula wa uongozi ndani ya CCM kutoka miaka mitano kuwa saba.

Jakaya anasema mjadala ulipoletwa ulikuwa ni moto ila tayarI CCM kulikuwa na utaratibu wa miaka mitano na uamuzi huo uheshimiwe.

======

KUONGEZA MIAKA YA URAIS
Kikwete:
Kuna kipindi walianza sana mjadala wa kubadili katiba sijui iwe miaka 7, pale wazee tulishauriana tukasema hapana, huku wanapotaka kutupeleka hawa sipo.

Nchi yetu ina viwango, hapa ilipofikia heshma yake kubwa ni kuheshimu vipindi viwili vya miaka mitano, wakianza hawa na miaka 7 huko tunakokwenda siko.

Nakumbuka tulikutana wazee na siku hizi hamna haja kukutana hata kwa simu mnaunganisha, tukakubaliana hawa lazima tuwaambie vijana hawa.

Walewale!alipaswa kuyasema kabla
 
Kuna watu wanatafuta heshima ya kwa nguvu ingawaje nobody respects them, Heshima hailazimishwi, u-stateman unakuja tu, watu wanakuona wewe ni State man na wanakuheshimu hahuhitaji kulazimisha, pure evil!
Ushirikina pia ulitumika ili kuogopwa na kila mtu.
Kuna mtu mmoja tu huo ushirikina ulishindwa kufanya kazi dhidi yake, ndio maana alipokamatwa aliagiza apimwe mkojo kwasababu hakuamini kama ni ujasiri wake bali aliamini ni madawa ya kulevya ndio yanampa ujasiri.
 
Wala hakikumtisha, ndio maana alikigomea kuongeza muda.
 
Sijui kwanini hakuliona Hilo. Ukatili wake kwa wapinzani ndio ulipunguza ushawishi wake. Kama angeruhusu democrasia na kuondoa mambo ya wasiojulikana Leo angekuwa bado yupo hai.
Maisha ya yule mwamba ni controversial, he was an enigma both in life and in death, wengine wanasema aliwahishwa na kijani wenzie kwamba ile covid iliyomchukua alipelekewa makusudi
 
Back
Top Bottom