Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

Jamaa aliyeniibia kuku mwaka jana leo amefariki, mtaa unahisi nimemroga

Kwa maelezo yako haya huyo mzee wako ni kweli kuna dawa anayo ila wewe anakuficha ila utakuja kuujua ukweli mwaka atakaofariki utaitwa ili urithishwe hiyo dawa.
Haiwezekani matukio zaidi ya mara mbili itokee hapohapo kwenu.
Sina hakika na hilo aliwahi ugua sana namimi ndo nilikuwa karibu nae zaidi akitoka mama. Alikuwa ananimbia mambo kadhaa wa kadhaa tu lakini hili hata hana hakujaribu kuliongelea kamwe.

Wala mzee si mtu wa kwa waganga angekuwa mama ningesema kanunua au alipewa hii dawa maana yeye ndo kahusika kutupeleka kwa waganga sana udogo wetu wote hasa kwa kumtoroka mzee maana mzee alikuwa hapendi na hapendi hadi leo
 
Hali hii ilimkuta mzee wangu alikuwa yeye na rozari rozari na yeye. Mwaka 2001 tukaibwa ng'ombe mkubwa maksai wa kulimia alituuma sana kama familia hakuna aliyekula isipokuwa watoto wadogo. kipindi hicho tuna ng'ombe kama sabini na ushee hivi lakini huyo alituuma sana.

Baasa ya siku mbili tukimtafuta maporini kutwa nzima bila mafanikio siku3 mzee akaitwa ofisi ya kijiji.Kufika akaulizwa mzee wewe ndo makanya charo? akasema mimi ndiye. Wakamwambia ng'ombe wako kapatikana shilela watu wa huku watakuwa wanapaju hapo shilela karibu na lunguya barabara ya kwenda kahama ukiwa unatoka kakola na walio leta taarifa ni mgambo (sungusungu) wa huko baada ya kumtilia shaka mwizi na kumbana hatimae alikiri kaiba.

Mzee alienda kumchukua ng'ombe ni kweli ni yeye kumbuka alienda na sungusungu wa kijijn kwetu pia jamaa yule mwizi akapigwa viboko na kuogeshwa kwenye tope na faini ya ng'ombe wa kijiji wale. Ikawa hivyo.

Mzee akaulizwa kama ana hitaji kulipwa alipwe lakini aligoma akasema kwa sababu ng'ombe wangu kapatikana na kijiji kimefuata taratibu zake mimi yameisgha kabisa.

baada ya miezi kadhaa jama aliugua kafa...Mchawi akaambiwa ni mzee. unaambiwa siku anakata roho alikuwa anawaambia kamwiteni flani aje mzee hata hajafika kwa jamaa akakuta kashafariki.


wengine wizi wa sola panel nao walikufa wakisema hivyohivyo mwiteni mzee flani.

Baada ya hapo watu wakaanza miminika kuja kununua dawa kwa mzee wakimwambia akiwapa watampa ng'ombe au hadi ng'ombe watatu.....mzee kila akiwaambia hahusiki wala hawakuamini. tangu hapo hatujawahi ibwa tena.

Huwa nafuga kuku kule sifungii kuku na muda myingine wanalala nje lakini hutasikia wameiba lakini kuna watu wanibwa vibaya mno.


2012 Walikuja wezi pia japo hawakuiba na hatukujua walikuwa wanataka waibe nini ila walikuwa wameiba na miji mingine. walipofika home hatujui kiliwatokea nini baiskeli zao wakaziacha wakaanza kukimbia ovyo sisi tumelala...bahati mbaya wanakimbilia kule walikoiba huku wanalia walikamatwa wakapigwa na kuchomwa moto

kati ya hao3 mmoja alipewa muda kwanini walikuwa wanakimbia mbio huku wanalia akasema mzee fln na vijana wake ndo walikuwa wanatukimbiza.


Mimi nilimuibia mzee 100 zile za note nafikiri mwishoni mwa miaka 90 hivi......Alinipiga vibaya mno huku akisema unataka ufe? Sijui siri ya mzee kuhusu haya ila ni mtu wa dini na nusu hata hivyo angekuwa na dawa basi mimi angekuwa kashanipa au kunielekeza.(Nipo karibu nae mno)


Mara kdhaa huwa ansema kigoma huwa hawaibwi na yeye amewahi ishi kule miaka ya 60-70 kama .....
Mzee wako kuna Zindiko alifanya si bure
 
Amefariki kwenye mazingira gani?(kuumwa au ajali)..Ameiba vipi kuku wako?alivunja banda au ilikuaje?
 
Ha
Mkuu umeongea kitu kikubwa sana ambacho nami kinaniumiza kichwa, je baada ya msiba ndugu zake watakubali tu yaishe hali ya kuwa wanahisi me ndio nimemroga ndugu yao? Je wakisema walipe kisasi wanidhuru si itakuwa dakika 0 tu maana sijui mambo ya kishirikina kabisa. Akili nyingine inaniambia nitafute wataalam wanikinge sasa si ndio itakuwa najiingiza kwenye maagano ya kichawi?
Hama hiyo sehemu, Fanya sana maombi ya ulinzi. Nenda katoe sadaka na mshirikishe mtu Mungu muwe mnaomba pamoja
 
Mzee wako kuna Zindiko alifanya si bure
Kwasababu mleta uzi kanikumbusha basi nitaenda tena kwa mzee shida hanywi pombe muda wote yupo active hivyo ni ngumu sana kunambia. Hlafu kwanini anifiche kitu cha faida na tuna share nae vitu vingi? Ila awamu hii namuuliza ikiwa kweli anayo nitafurahi mno
 
Wakuu habari zenu,
Mwaka jana mwezi March kuna jamaa mtaani hapa aliniibia kuku mchana kweupe kabisa watu wanaona, nilipopata taarifa nikamtafuta mtaani nikamkosa, nikaamua kwenda nyumbani kwako nikamkuta dada zake nikawaeleza jamani fulani kaniibia kuku wangu naomba akija mwambieni arudishe. Hawakutilia sana maanani wakasema wamechoka na habari zake za wizi ila watamwambia arudishe.

Niliporudi mtaani nikapata taarifa kutoka kwa wambea wa mtaa ya sehemu alipouza hao kuku ikabidi nifunge safari mpaka kwa huyo mama aliyeuziwa kuku lakini nae akakataa kabisa kuwa hajauziwa. Basi me nikaondoka, kesho yake mchana nikapewa taarifa kuwa mwizi wangu ameonekana mtaani huko eti ananitafuta ajue kwa nini namchafulia jina lake mtaani, ikabidi sasa nianze kumtafuta hali ya kuwa kichwani tayari nimechafukwa kwa hasira. Muda si mrefu nikakutana nae kabla sijaongea nae akaanza kunipandishia sauti kwa nini nimeenda kwao nimemuita mwizi wa kuku, hapo uzalendo ukanishinda kwa hasira nikavaana nae nikampiga kidogo then nikamchukua nikampeleka mpaka ofisi ya mtaa kushtaki kuwa mwizi wangu huyu naomba anirudishie kuku wangu.

Alipoulizwa kuhusu kuiba kuku akakataa kabisa tena akaniruka kuwa nimempiga sana hali ya kuwa kuku hajaiba, me kuulizwa ushahidi sina zaidi ya kutaka kwenda alipouza kuku, tukaongozana mimi, mwizi wangu pamoja na mtendaji wa mtaa mpaka alipouza kuku, kufika hapo aliyenunua kuku akakataa kabisa kuwa hajauziwa kuku. Hapo nikakosa ushahidi wa kumtia hatiani ikabidi niwe mpole tu ila nikatamka kuwa basi namuachia Mungu kama kweli hajaiba kuku na iwe hivyo lakini kama ameiba basi Mungu atalipa kwa wote waliohusika, nikaondoka zangu.

Sasa ikapita miezi kama sita tukio limeanza kusahaulika, akaja jirani mmoja kunipa habari kuwa yule mwizi wangu anaumwa sana na anaropoka huko usiku wa manane kuwa kuku wamemponza, sikutilia maanani sana habari hizo maana najua umbea wa mtaani labda walitaka kunichimba wajue kama nikisamehe kweli au kuna kitu nilifanya. Baada ya kama wiki mbili hivi habari zikaenea zaidi kuwa jamaa anaumwa sana na amewaambia ndugu zake kuwa anakufa kwa sababu ya kuku. Baada ya siku kadhaa akaja mzee mmoja ni sheikh wa msikiti ninaosali hapo mtaani akaniambia kuwa amefuatwa na familia ya mwizi wangu kuwa yeye sheikh ameitwa kumuombea dua mgonjwa ambaye ndio huyo mwizi wangu, baada ya dua familia imemtuma aje kwangu kuomba msamaha kwa niaba yako maana hali imekuwa ngumu sana. Me nikamjibu sheikh "mzee wangu mimi sihusiki kabisa na ugonjwa wa huyo mtu, tangu nilipokosa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu kuku wangu aliowaiba basi nikasamehe kwa maana kwanza kuku wenyewe hawakuwa wengi lakini pia nikiendelea kufuatilia hii issue nitapoteza muda lakini pia nitajijengea ubaya na ndugu zake kwa hiyo nimesamehe kwa roho moja"
Mzee anaondoka.

Sasa leo alfajir nikiwa msikitini ndio nikasikia tangazo la kifo cha jamaa aliyeniibia kuku wangu, kibinadamu niliingia huzuni lakini nikahisi sasa watu wamepata cha kusema kuhusu Mimi na huyu jamaa, wakuu tangu muda huo story mtaani ni mimi kuhusika na kifo cha jamaa, wengine wanasema sawa tu jamaa alizidi, wengine wanasema Nina roho mbaya yaani kuku tu ndio natoka roho ya mtu. Basi sina amani na hata msibani kuzika nafikiria nisihudhurie maana hata wasionijua watatambulishwa leo kuwa mimi ndio muhusika.

Cha kushangaza yule mama niliyeambiwa kuwa ndio alinunua kuku niliobiwa, asubuhi kanifuata nyumbani eti kuniomba msamaha, kakiri ni kweli aliuziwa kuku wangu na yule jamaa na sio kuku wangu tu hata kuku wa watu wengine pia huwa anamuuzia na mbuzi alishawahi kununua kwa jamaa. Nikamjibu kuku wangu mimi ni wale weupe akasema ndio aliwanunua ila anaomba msamaha yuko tayari kulipa pesa ya hap kuku ila nisifanye kitu kibaya katika familia yake au yeye maana anajua tego la mwizi huwa linaanza na mwizi, aliyenunua mpaka aliyekula hivyo ana hofu familia yake itaangamia. Nikamjibu mama we kuwa na amani mimi sihusiki na hilo. Ameondoka lakini hana raha kabisa.

Wakuu nakiri mbele yenu nyinyi sijawahi hata kuusogelea ushirikina na sihusiki kabisa na hili lakini ndio hivyo nimeshapata sifa mbaya mtaani, naombeni ushauri wenu katika hali hii nifanye nini angalau niwe na amani.

Shukran.
eeeh[emoji17] pole sana mkuu, but relax, najua ndio wataongea sanaa kwa muda kiasi, ila baada ya muda watasahau , mi nikushauri ujipe likizo fupi uende ubadirishe mazingira then urudi, utarefresh mind sana, but pole, ndo binadamu walivo, wanaamini upumbavu.
 
🤓 🤓 🤓, Kabisa mkuu, kuna jamaa alienda kuiba kuku usiku, Sasa baadala ya kuwanyonga shingo ili asipige kelele, yeye akakosea akanyonga mguu 😂😂. Wacha kuku apige makelele ya kiwango cha lami.

Mpaka leo ni R. I. P
Nimeshuhudia matukio mawili ya watu kufa, sababu ya kuku,...mmoja aliiba kuku vizuri kabisa,sasa wakati anakimbia akaingia kwenye shimo lililochimbwa kwa ajili ya kupanda mgomba, akavunjika mgongo, akakutwa asubuhi akiwa mzima, ila watu wakagoma kumsaidia mpaka akafa , maana walisema alikuwa msumbufu sana, na huwezi amini alikuwa na wake wawili,.....

wengine ilikuwa pale mbeya karibu na shule ya iyunga boys, walienda kuiba kuku, jirani wa mwenye kuku alikuwa katoka kupiga masanga akawaona wakiwa wanatoboa ukuta, akawashtua wengine kwa simu, wezi wakajaa kwenye kumi na nane... wawili wakala kiberiti,..mmoja tu ndo alipokonyoka,......

Kuku..🙌🙌🙌
 
Umemroga live bila chenga.. Hapa unatupa tu taarifa tukuogope😂
 
Ingawa sijasoma content ila ushauri wa hao wapuuzi unaoishi nao kitaa anzisha biashara ya uganga nadhani utawapata (Kama na wewe ni walewale wa Imani hizo za kale... )
 
Maana halisi ya "wanaokwenda jela sio wote wenye hatia....!" Mtafute huyo sheikh, mama aliyenunua kuku, ndugu wa marehem na baadhi ya watu wenye ushawishi mkae muyajenge! ndugu wa marehemu tu ndio wanaweza kukuondolea hizo hisia au kufanya zidumu!
 
Back
Top Bottom