Update....
Ni kwamba mwanamke alinyang'anywa simu ya awali alokua anatumia na kapewa simu mpya yenye line mpya ya Airtel.
Nmefanikiwa kuipata hio namba na nmempigia na kuongea mwanamke mwenyewe.
Anasema,
"Shem mi sio kwamba simpendi rafiki ako, nampenda sana na nilitamani awe mme wangu. Sema rafiki ako hakua serious na Mimi. Miaka 4 yote tangu ameleta barua hamna kinachoendelea. Familia inanisumbua Sana afu nikimwambia hataki kunielewa anadai mpaka amalizie nyumba yake. Nyumba imeisha anadai finishing bado. Hivi kweli shemej nyumbA inaweza mzuia mtu wasifunge Ndoa? Hivi kweli anachonifanyia mwenzako unaona Ni sahii."
Nikamjibu,
"Kwaiyo meji ukaona Njia rahisi Ni kuolewa TU na rafki yake, hujui itamuumiza Kias gani?"
Akasema,
"Shemej nikwambie TU ukweli, uyu B tangu mwanzoni ashaonesha ananipenda Sana. Afu tangu zaman keshaonesha Nia ya kunioa MDA mrefu. Sema Mimi TU ndo nilikua kikwazo, afu kingine uyu B anakubalika Sana uku nyumban.
Shemej presha kwa familia yangu kuhusu B Ni kubwa Sana, Baba na mama na dada zangu wote wanataka niolewe na B. Imefkia mpaka mama ananambia uyu alonichumbia Ni mhuni TU miaka 4 Ni uchumba sugu huo. Imefkia mpaka baba haniongeleshi kisa sitak kuolewa na B. Na wote washanambia nisipoolewa B Mimi sitokua mwanao Tena na watanifuta kwenye ukoo.
Shemej yang mi mwenywe Niko Njia panda apa, moyoni mwangu B hayupo kabisa ila nalazimishwa TU na familia yangu. Uto rafiki yako hawamtaki kabisa ata kumskia uku nyumbani."
Nikamwambia,
"Kwaiyo shemej uko serious kabisa umelazimishwa Hii ndoa?"
Akasema
"Ndio Shem, yaan naomba TU uniombee msamaha TU kwa rafk yako. Mi bado nampenda Sana."
Nikamwambia,
"Bas Shem naomba ufanye jion tuonane ata kwa jamaa tujue tunaliwekaje hili"
Akasema,
"Sawa, ila Mimi kwa jamaa siwez kuja tena.italeta balaa. Labda yeye ata aje kwako niwakute apo kwako"
Nikasema,
"Sawa"
Ninachowaza Sasa,
Kama ni kweli uyu mwanamke kalazimishwa. Na kweli ANAMPENDA jamaa.
Nawaza kumshauri rafiki yangu, ashirikiane na uyu mwanamke.
Kisha binti atoroshwe akawekwe mafichoni kwa sikU kadhaa Hadi ile harusi ilopangwa itakapopita.
Uyu B atakapomtafuta akakosa Basi Iyo Ndoa ya kulazimisha itakua imeota manyoya.
SIJUI KAMA NIKO SAHII AU LAH
ushauri wenu tafadhali