Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Update.....

Tulipanga leo saa Moja kamili tukutane nyumban kwangu na uyo binti pamoja na dogo. Tukampigia Ila akawa hapatikani.

Baadae Kwenye saa 1 na nusu,
Kaja kupatikana akasema anakuja sawa tumsubiri anakuja.

Sahivi tunampigia simu haipatikani.

Tumebadili mpaka namba, tunapiga ila bado hapatikani.

Tumejaribu kupigia shoga Ake wa karibu, mama P akamcheki kwake.

MDA si mrefu kasema kafika kwake hayupo,

Kasema anaelekea kwao kuona Kama atampata.

BADO TUNAMSUBIRI[emoji17]
 
Mpaka wamepanga na process zote za ndoa ni wamejipanga,ni bora ingekuwa kuchepuka tungesema kateleza,yaani hapo kikubwa ni kujitahidi kumrudisha mdogo wenu kwenye hali ya kawaida na wala sishauri urafiki wenu mlotengeneza miaka kumi ufe eti kisa mwanamke,
Kwangu mimi japo ni mwanamke ila kwa roho ngumu nilokuwa nayo yaani siku mbili naendelea na shughuli zangu kama hamna kilichotokea sijui nyie mnahandle vipi situation kama hizo
NOTE
Jamaa yangu umeumia lakini emu kuwa mwanaume ivi nyote mkiwa frustrated unadhani nani atamsaidia mhusika?wake up my dear!
Am cool now, najaribu kucope na Hali halisi mkuu[emoji17]
 
Usifanye hicho kitu unachotaka kukifanya,kama angekuwa anampenda asingefikia kote huko au we ulitaka ajiteteeje emu kuwa serious acheni mawazo ya kutorosha mtu mzima na akili zako,hivi umeanza kuyumba mapema hivi na huyo mdogo wako utamsaidiaje?
Nawaza TU mkuu, ukinipa USHAUR Bora zaidi ntashkuru Sana[emoji17]
 
Kosa analo huyo mnayemuita dogo.
Kwann kaleta malaya kwenye urafiki wenu ulioshibana?

Malaya katambulisha mtu nyumbani halafu anasema analazimishwa kuolewa naye[emoji23].

Ilikuaje mpaka akampeleka kwao?

Sikia, HUYO MALAYA ATAWAUA.
AMESHAUA URAFIKI WENU, SASA BADO ROHO ZENU.

NA NINAVYOKUONA NA AKILI ZAKO MGANDO ZA KUMTOROSHA KAMA HAMTOUANA BASI MTAPAKANA MAFUTA WE SUBIRI TU.
Maneno makali sana Ayo mkuu[emoji17]
 
Muongo kakubali kuolewa huyo anawachosha tuuu!!karne hii hamna hizooo!tena mkristo mwenziwe kabisaa!mzazi gani atakubali mwanawe abadili dini kirahisi hvyooo!!!wakati ana mchumba tayari na anataraji kumuoa ila huyo nae mpk ajenge ndo aoe!
Nmetafakari sana naona kama uko sahii kabisa mkuu[emoji848]
 
Update....
Ni kwamba mwanamke alinyang'anywa simu ya awali alokua anatumia na kapewa simu mpya yenye line mpya ya Airtel.

Nmefanikiwa kuipata hio namba na nmempigia na kuongea mwanamke mwenyewe.

Anasema,
"Shem mi sio kwamba simpendi rafiki ako, nampenda sana na nilitamani awe mme wangu. Sema rafiki ako hakua serious na Mimi. Miaka 4 yote tangu ameleta barua hamna kinachoendelea. Familia inanisumbua Sana afu nikimwambia hataki kunielewa anadai mpaka amalizie nyumba yake. Nyumba imeisha anadai finishing bado. Hivi kweli shemej nyumbA inaweza mzuia mtu wasifunge Ndoa? Hivi kweli anachonifanyia mwenzako unaona Ni sahii."

Nikamjibu,
"Kwaiyo meji ukaona Njia rahisi Ni kuolewa TU na rafki yake, hujui itamuumiza Kias gani?"

Akasema,
"Shemej nikwambie TU ukweli, uyu B tangu mwanzoni ashaonesha ananipenda Sana. Afu tangu zaman keshaonesha Nia ya kunioa MDA mrefu. Sema Mimi TU ndo nilikua kikwazo, afu kingine uyu B anakubalika Sana uku nyumban.

Shemej presha kwa familia yangu kuhusu B Ni kubwa Sana, Baba na mama na dada zangu wote wanataka niolewe na B. Imefkia mpaka mama ananambia uyu alonichumbia Ni mhuni TU miaka 4 Ni uchumba sugu huo. Imefkia mpaka baba haniongeleshi kisa sitak kuolewa na B. Na wote washanambia nisipoolewa B Mimi sitokua mwanao Tena na watanifuta kwenye ukoo.

Shemej yang mi mwenywe Niko Njia panda apa, moyoni mwangu B hayupo kabisa ila nalazimishwa TU na familia yangu. Uto rafiki yako hawamtaki kabisa ata kumskia uku nyumbani."

Nikamwambia,
"Kwaiyo shemej uko serious kabisa umelazimishwa Hii ndoa?"

Akasema
"Ndio Shem, yaan naomba TU uniombee msamaha TU kwa rafk yako. Mi bado nampenda Sana."

Nikamwambia,
"Bas Shem naomba ufanye jion tuonane ata kwa jamaa tujue tunaliwekaje hili"

Akasema,
"Sawa, ila Mimi kwa jamaa siwez kuja tena.italeta balaa. Labda yeye ata aje kwako niwakute apo kwako"

Nikasema,
"Sawa"

Ninachowaza Sasa,
Kama ni kweli uyu mwanamke kalazimishwa. Na kweli ANAMPENDA jamaa.

Nawaza kumshauri rafiki yangu, ashirikiane na uyu mwanamke.
Kisha binti atoroshwe akawekwe mafichoni kwa sikU kadhaa Hadi ile harusi ilopangwa itakapopita.

Uyu B atakapomtafuta akakosa Basi Iyo Ndoa ya kulazimisha itakua imeota manyoya.

Afu Sasa uyo B aje kwetu kulalamika kwetu katoroshewa MKE, na sisi tuje tumuoneshe kua upumbavu hatutaki.

SIJUI KAMA NIKO SAHII AU LAH[emoji848]

ushauri wenu tafadhali
Huyo mwanamke hana lolote,waacheni wafunge hiyo ndoa

Huyo dogo kaepushwa na balaa hilo,mwanamke hafai ni muongo.
 
Lakini huyo mwanamke mwenzetu hakutumia akili kwasababu mleta mada kasema bibie amesomeshwa , akatafutiwa kazi, akapangiwa nyumba nzima plus gari la kutembelea,.. hakuna mwanaume ambae Hana malengo na ww anaweza kukufanyia hayo yote ilikuwa ni uvumilivu ndo ulihitajika Kwa huyo mdada ..
Kabisa mkuu[emoji848]
Jamaa alimtunza binti utadhani malkia.

Kuna MDA tulkua mpk tunamlaumu kwa matumizi ya ovyo ya pesa na kumdekeza.

Maana nyumba alompangia alimuwekea housegal wakati hata kazi za maana pale hamna na nyumba nzima anakaa yeye na mdogo wake anaerisiti form six
 
Dah! Jamaa huwez Amin alkua anamgharamia Yule mwanamke utadhan mke wake wa Ndoa.

Jamaa yangu Ni form four, ila alipambana kumlipia Ada mpaka binti uyu kamaliza chuo kikuu.

Kibaya Zaid ata hapo sheli anakofanya kazi uyu binti, jamaa ndo kamuunganisha na ndo mdhamini wake.

Binti kapangiwa nyumba nzima, anaishi kwa Raha Sana.

Jamaa alkua analipa kila kitu khs mahitaj yake yote ya nyumbani mpaka dharula za familia yake.

Gari anayotembelea kamnunulia uyu jamaa,
(Tena nilishiriki ipasavyo kwenye mchakato mzima wa kuiagiza mpak kuitia mkononi)

mafuta juzi juzi TU tunatoka gym alipitia she'll kumuwekea ya 350,000 kwa ajili ya mizunguko yake.nikishuhudia mwenyewe.

Mshahara anaolipwa sidhan hata Kama uwa anaugusa kabisa.

Kwakweli,
alichomfanyia jamaa Ni zaidi ya unyama[emoji26]
Huyo mwanamke ni mbung'o
 
Karma lazima ije ifanye kazi yake kwa huto mwanamke na wazazi wake

Yaani hao wazazi wamesaidiwa mtoto wao kusomeshwa na kutafutiwa kazi kweli bado wakawa hawamkubali jamaa?

Yaani mtu asomeshe mtoto wenu halafu asimuoe yaani jamaa awe amefanya kazi bure...hao wazazi hawakujiuliza Hilo?

Hawakujiuliza hiyo miaka minne ya uchumba mtoto wao kafanyiwa nini na huyo jamaa?

Yaani Kama huyo mwanamke kafanyiwa kila kitu na jamaa Basi lazima angeolewa nae

Maswali hayo hapo juu wazazi hawakujiuliza huko ni kukosa shukran kabisa na watajuta aisee

We mwambie jamaa atulie tu asikilizie kama huyo mwanamke hajarudi huku analia..

Na huyo jamaa mpumbavu Sana mpunguzeni Kama vipi yaani inawezekana kabisa ndani ya hiyo miaka minne alikua na yeye anatembea nae kisiri Siri daah
Hakufikiria madhara ya yeye kumchukua na kumuoa mchumba wa rafiki yake Tena mke wa pili wakati rafiki yake Hana hata mmoja ndo huyo anaetegemea amuoe?
Aisee Hilo lijamaa mlipunguze tuu halina maana mkuu

Hata wewe mleta mada angalia asije kukuolewa mke wako awe mke wake wa 3

Anyway mkuu hebu tuambie na sisi ni bidhaa gani mnauza maana zinaonekana zina hela sanaaa na sisi tuanze kuuza
Kingine Cha kujiuliza,...
Mama Ake binti mwaka huu kalazwa pale Ocean road mwezi na nusu-jamaa kagharamia

Katolewa pale,
Kahamishiwa Agha khani, wiki 3 jamaaa katoboka bill zote.

Ila bado mama uyu baada ya kupona kabisa kashindwa kuthamini mchango wa dogo hata mwaka haujaisha anafanyia hivi[emoji26]

Duniani watu wema hulipwa vibaya, uyu dogo kalipwa vibaya Sana.[emoji26]

Naandika hivi Hadi machozi yananilenga.
 
Hao wazazi wake wanakauwezo?
 
Na je hao wazazi walikua wanajua dogo ndo analipa hizo bills?

Waliosemaga tenda wema nenda zako si wapumbavu aisee
 
Update....
Ni kwamba mwanamke alinyang'anywa simu ya awali alokua anatumia na kapewa simu mpya yenye line mpya ya Airtel.

Nmefanikiwa kuipata hio namba na nmempigia na kuongea mwanamke mwenyewe.

Anasema,
"Shem mi sio kwamba simpendi rafiki ako, nampenda sana na nilitamani awe mme wangu. Sema rafiki ako hakua serious na Mimi. Miaka 4 yote tangu ameleta barua hamna kinachoendelea. Familia inanisumbua Sana afu nikimwambia hataki kunielewa anadai mpaka amalizie nyumba yake. Nyumba imeisha anadai finishing bado. Hivi kweli shemej nyumbA inaweza mzuia mtu wasifunge Ndoa? Hivi kweli anachonifanyia mwenzako unaona Ni sahii."

Nikamjibu,
"Kwaiyo meji ukaona Njia rahisi Ni kuolewa TU na rafki yake, hujui itamuumiza Kias gani?"

Akasema,
"Shemej nikwambie TU ukweli, uyu B tangu mwanzoni ashaonesha ananipenda Sana. Afu tangu zaman keshaonesha Nia ya kunioa MDA mrefu. Sema Mimi TU ndo nilikua kikwazo, afu kingine uyu B anakubalika Sana uku nyumban.

Shemej presha kwa familia yangu kuhusu B Ni kubwa Sana, Baba na mama na dada zangu wote wanataka niolewe na B. Imefkia mpaka mama ananambia uyu alonichumbia Ni mhuni TU miaka 4 Ni uchumba sugu huo. Imefkia mpaka baba haniongeleshi kisa sitak kuolewa na B. Na wote washanambia nisipoolewa B Mimi sitokua mwanao Tena na watanifuta kwenye ukoo.

Shemej yang mi mwenywe Niko Njia panda apa, moyoni mwangu B hayupo kabisa ila nalazimishwa TU na familia yangu. Uto rafiki yako hawamtaki kabisa ata kumskia uku nyumbani."

Nikamwambia,
"Kwaiyo shemej uko serious kabisa umelazimishwa Hii ndoa?"

Akasema
"Ndio Shem, yaan naomba TU uniombee msamaha TU kwa rafk yako. Mi bado nampenda Sana."

Nikamwambia,
"Bas Shem naomba ufanye jion tuonane ata kwa jamaa tujue tunaliwekaje hili"

Akasema,
"Sawa, ila Mimi kwa jamaa siwez kuja tena.italeta balaa. Labda yeye ata aje kwako niwakute apo kwako"

Nikasema,
"Sawa"

Ninachowaza Sasa,
Kama ni kweli uyu mwanamke kalazimishwa. Na kweli ANAMPENDA jamaa.

Nawaza kumshauri rafiki yangu, ashirikiane na uyu mwanamke.
Kisha binti atoroshwe akawekwe mafichoni kwa sikU kadhaa Hadi ile harusi ilopangwa itakapopita.

Uyu B atakapomtafuta akakosa Basi Iyo Ndoa ya kulazimisha itakua imeota manyoya.

Afu Sasa uyo B aje kwetu kulalamika kwetu katoroshewa MKE, na sisi tuje tumuoneshe kua upumbavu hatutaki.

SIJUI KAMA NIKO SAHII AU LAH[emoji848]

ushauri wenu tafadhali

kama ni kweli basi huyo mwanamke ni mpumbavu.
 
Huku mbele sasa nahisi kuna chai.

Mafuta ya 350,000 kwa gari gani?

Semi tella?

Na kama ana gharamia hivyo, kwanini familia ya binti haimtaki na inamtaka huyo mwingine? Tena si wa dini yao? Na walianzaje kumtaka? Aliwatambulisha?
Mafuta ya 350k kwa SUV mbili mbona Ni ya kawaida Sana mkuu.
Hazifiki hata Lita 150
 
Back
Top Bottom