Jamaa kauliza swali la kufikirisha kuhusu Safina ya Nuhu.

Jamaa kauliza swali la kufikirisha kuhusu Safina ya Nuhu.

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Story ya Safina inasema Nuhu aliwaweka Wanyama wote duniani ndani ya Safina.

Swali?

Simba Na suala wanaweza kukaa sehemu moja hata kwa lsaa moja Tu achilia Mbali mwezi mzima?

Binadamu Na Simba? Binadamu Na nyoka? Kukaa sehemu moja ya wazi inawezekanaje jamani?

Vipi kuhusu Wanyama wadogo ambao life span yao ni wiki Moja au mwezi mmoja?

Vipi kuhusu Wanyama wa baharini kama nyangumi na papa?
 
Story ya Safina inasema Nuhu aliwaweka Wanyama wote duniani ndani ya Safina.

Swali?

Simba Na swala wanaweza kukaa sehemu moja hata Kwa lisaa limoja Tu achilia Mbali mwezi mzima?

Binadamu Na Simba? Binadamu Na nyoka? Kukaa sehemu moja ya wazi inawezekanaje jamani?

Vipi kuhusu Wanyama wadogo ambao life span yao ni wiki Moja au mwezi mmoja?

Vipi kuhusu Wanyama wa baharini kama nyangumi na papa?
sasa wee jamaaa papa na nyangumi wanaishi majini hivyo mvua ilipokuja walienjoy zaidi...
 
Story ya Safina inasema Nuhu aliwaweka Wanyama wote duniani ndani ya Safina.

Swali?

Simba Na suala wanaweza kukaa sehemu moja hata kwa lsaa moja Tu achilia Mbali mwezi mzima?

Binadamu Na Simba? Binadamu Na nyoka? Kukaa sehemu moja ya wazi inawezekanaje jamani?

Vipi kuhusu Wanyama wadogo ambao life span yao ni wiki Moja au mwezi mmoja?

Vipi kuhusu Wanyama wa baharini kama nyangumi na papa?
Wainjilist na wateule wa bwana njooni mjibu ila muache kutuambia Kila jambo linawezekana
 
Kama ingekuwa hivyo basi mvua ingeweza kuwaangamiza wahusika Tu huku ikiwaacha bila kuwadhuru Nuhu & company
Watakuambia kwa uwezo wa Mungu inawezekana
 
Hapo MWANZO: 1

3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru

21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.

Zingatia hizo Mungu akasema , yani Mungu akasema!!
 
Kama nyangumi analingana na Kisiwa ama ule mwamba wa Bismarck Rock, Je Safina Ya Ndugu Nuhu ililingana na nini?
 
Safina ulikua na vyumba vingi pia na vyumba vya watani vilikua mhim la sivyo wangeuana
 
Hapo MWANZO: 1

3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru

21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.

Zingatia hizo Mungu akasema , yani Mungu akasema!!
Inaposemwa kwamba Mungu AKASEMA usifikiri alikuwa anatamka halafu vitu vinatokea kama mazingaombwe.

Alikuwa anatoa amri kitu Fulani kitengenezwe Na kinatengenezwa.

So tunaposema Kwa mfano Mungu alimuumba mtu hatumaanishi kwamba Mungu mwenyewe alichukua udongo aka mfinyanga MTU isipokuwa tunaamanisha kwamba Mungu alitoa amri au maelekezo atengenezwe kiumbe binadamu and then Malaika wake special ambao aliwapa maarifa ya kutengeneza viumbe kupitia elimu ya genetical engineering wakafanya Kazi ya kumtengeneza binadamu Kwa amri Na maelekezo ya Mungu.

Yani ni Sawa tunavyo SEMA uwanja umetengenezwa Na Mkapa au Stendi ya Magufuli, Mkapa & Magufuli hawakusogeza hata tofali Moja isipokuwa walitoa fund Na amri.

Point yangu Ni kwamba Mungu alitoa amri lakini utekelezaji wa amri lazima uendane Na kanuni ZA asili ambazo Mungu mwenyewe ndio kaziweka. Ndio maana hata hiyo Safina yenyewe Nuhu alielekezwa mpaka vipimo ili kusurvive Kwa Safina hiyo kuendane Na kanuni ZA asili ZA Mungu mwenyewe.

Kwa hiyo swali bado linabaki pale pale.
 
Story zingine zinadai Nuhu hakuwa muokoaji,ila mleta janga
Eti alipoona watu awafuati mafundisho,akaomba kwa Mungu alete mafuriko kuwaangamiza
 
Kama adamu aliishi na hao wanyama wote bila kuliwa kwa nuhu inashindikana vp?

Kama daniel aliweza kupona kuliwa na simba wenye njaa kali kwa nuhu inashindika vp?

Kama nyoka aliweza kuongea na eva pia na yesu kule jangwani kwa nuhu inashindikana nini?

Kama yona aliweza kutapikwa na samaki mla watu kwa nuhu chashindikana nini?

Kama hata jua lilimtii musa likaganda mpaka izrael na joshua waliposhinda vita, ni nini kitakachoshindikana kwa nuhu?

Hebu tafakari kwanza hayo kama bado unamaswali niambie nikujibu
 
Back
Top Bottom