Jamaa yangu ameomba mchango wa kufanya birthday party

Jamaa yangu ameomba mchango wa kufanya birthday party

Katuma na Emoji ya Kulia kabisa [emoji23][emoji23][emoji23] hakuna kitu hapo
 
Aisee huyo hafai hata kuwa au kuitwa jamaa. Usiwe na ujamaa na watu wa hovyo kiasi hicho.
 
Birthday inachangiwa tangu lini? Kwanza hayo ni mambo ya wanawake, mwanaume kujishughurisha na mambo ya birthday ni lazima utakuwa na walakini kichwani.
Watu tunatofautiana kweli yaani na ndevu zote hizi eti unaimbiwa na makofi sijui keki, kwa kweli hapana hata wanawake wazima huwa nawatizama na jicho la dharau kuona jitu kubwa linasheherekea Happy birthday sasa basi bora ata awe mkweli na miaka yake kuitaja hataki sasa wewe kama hutaki watu wajue miaka yako sherehe ya nini unashangilia nini kikubwa?
 
Mimi mwezi uliopita mtu wa aina hiyo amenitumia text kwamba anatarajia kufanya birthday yake mwezi wa nane mwaka huu [emoji38][emoji38], imagine vichwa vya watu wengine vinavyowaza na huyo ni kijana ambaye umri wake ni wa mtu mwenye majukumu kabisa.Sikuijibu Ile meseji baada ya siku tatu akatuma tena ktk WhatsApp yangu nikaisoma na blue tick akaziona ila nikapiga kimya.Yani mtu seriously kijana wa kiume anakwambia zipo kadi za single elfu 10 na double elfu 20 aiseee nilijawa na hasira kwanini watu wasiwekeze ktk vitu vinavyowaletea maendeleo,nadhani kwa kutojibu text zake ilikua jibu ila akipiga simu kukumbushia ntaamini ana shida ktk kichwa chake.
 
😂😂😂nimecheka kwanza ila kimtazamo wangu yani mbavu kabisa mbaba unafanya birthday? Kuna jamaa yangu mbav moja hivi ilienda mpaka studio kupiga picha kisha ikapost fb na whatsap nilichoka kabisa
 
Back
Top Bottom