moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 159,165
- 777,891
Msafiri Mkelemi alichezsha kuanzia miaka ya 70 na mechi ya mwisho ya derby alichezezesha mwaka 1988.Sijajua wewe unazungumza zamani gani, kwa sababu hata mwaka 2010 inaweza kuwa ni zamani kwa watu wengine. Wengi uliowataja ninafahamau walichezesha miaka ya themanini na tisini, mimi ninaongelea waliochezesha miaka ya sabini wakati wa TANU, nafikiri niliweka wazi jambo hilo. Kwa mfano aliyechezesha ile derby iliyokinukisha Nyamagana; pamoja na intensity yake, refa alitoka klini sana.
Mussa Lyaunga alichezesha miaka ya 80 mpaka 90.
David Okoth alichezesha kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 80 alimaliza mwanzoni mwa miaka ya 90.
Abdulrasul Ismail alihujumu Simba kwenye derby ya mwaka 1986 pale Salum Kabunda alipomrukia miguu yote kifuani Edward Chumila ( Chumila alizimia, akakimbizwa hospitali) na hakutoa hata kadi.
Unasemaje hiyo ni miaka 10 iliyopita?
Mechi ya mwisho Simba ambayo amechezesha David Okoth mjini Dar es salaam ilikuwa ni dhidi ya Biashara Shinyanga mwaka 1992.
Mkuu Kichuguu zamani inaanzia miaka mingapi nyuma?