Jamal Bakhresa: TFF imeharibu mpira wa Tanganyika. Azam FC nitaihamishia Zanzibar

Jamal Bakhresa: TFF imeharibu mpira wa Tanganyika. Azam FC nitaihamishia Zanzibar

Ongezea, mwamuzi ndie aliepelekea mpaka yule mchezaji wa azam kujifunga

N.b: Ukitaka kujua yule mtu unaemheshimu kama ni mwendawazimu mkute kwenye mijadala ya Simba na Yanga utamkataa
Wewe ndio mfano wa huyo mtu, watu wanazungumzia mfumo kwa ujumla wake au mechi kwa ujumla wake, wewe unazungumzia tukio moja lililojitenga (isolated event) ya mchezaji kujifunga.
 
Sawa ila bodi ya ligi na tff wamejitahidi sana kutoa adhabu kwa marefa ila ndio hivyo rushwa imekita mizizi sana
Utakuta hata huyo mzee anaongea tu ili kupaka mafuta ila ukweli mwingine anaujua
Kauli ya Karia kuingilia maamuzi ya kanati ya masaa 72 kwenye adhabu ya Aragija inaonyesha hawako makini kuwashugulikia waamuzi.
 
Apunguze kujieleza. kama anataka atoke atoke tuu, ye naani alafu azam ni kitu gaani alafu hawa wanatuona sisi kama, eti kisa tupo kimya eeetiii!!!?
Mzee huyo sio kajamba nani, maoni yake yatasikilizwa na yatafanyiwa kazi.
 
Hiyo ligi ya matopeni itabidi asijili upya,hakuna mchezaji anayejielewa ataenda huko hata Ibenge hawezi.😁
 
Hivi huyu Jamal Bakhressa ni nani tena? Yawezekana ni mdogo wake, mi nilidhani hawa wengine ni wasimamizi tu ila mmiliki top kabisa wa Azam fc ni Mzee Said Salim Bakhresa
 
Huyu Mzee alifanya makubaliano batili na uongozi wa Yanga kwamba awaachie Yanga ubingwa wa ligi kuu wao watamuachia mechi ya nusu fainali ya kombe la FA.

Kakosa vyote sasa anapokuja kutishia kuondoa udhamini hizo huwa siasa za visingizio.

Anataka kusema Simba alibebwa!, Fei Toto kampiga ngumi ya hadharani kabisa Libasse Gueye alitaka Fei aachwe tu wakati ni faulo ya kadi nyekundu?.

Paschal Msindo kacheza rafu za kadi mwamuzi kapotezea, Simba wamefanyiwa sana uhuni msimu huu lakini timu ya waungwana haina muda wa kulialia nje ya viwanja.

Tangu GSM atoe mchango wa shilingi bilioni 10 za kampeni mwaka jana na Yanga ikatoa shilingi milioni 100 maana yake Yanga ni bingwa kwa namna yoyote ile, chafu au safi.

Hiyo milioni 100 ilipigiwa makelele na wanachama wakihoji kwanini itumike kwenye siasa pesa ya klabu.
Ila hata unapoandika haya unatumia akili kidogo hata kama hauna? Simba na yanga hao wote ni ccm kindakindaki hao wakina hersi walitoa kwa ajili ya kujijenga wao binafsi
 
Yuko sahihi kabisa, Azam jana walinyimwa penalti ya wazi kabisa na kwa kushangaza mchezeshaji wao aliyeangushwa kwenye eneo la adhabu eti ndiye akaonyeshwa kadi ya njano...!!!!
 
Tatzio siyo waamuzi wa mpira au TFF au bodi, tatizo ni mfumo mzima wa Tanzania uliojaa rushwa, dhuluma, na upendeleo.

Zamani sana nezi za TANU na FAT tulikuwa na marefa wasiokuwa na beji za FIFA, kama vile Manyoto Ndimbo, walikuwa wanachezesha mpira kwa haki bila malalamiko yoyote. Leo enzi za CCM na TFF mambo yamekuwa shaghla baghla.

Timu pendwa ya TFF ni Simba tu
Mkuu Hata zamani marefa walikua na upendeleo
Manyoto Ndimbo Alibeba sana Yanga.
Msafiri Mkelemi wa Tabora Alibeba sana Yanga.
Bakari Bendera wa Tanga aliibeba sana yanga.
Hafidhi Ali wa Zanzibar aliibeba sana Yanga.
Mussa Lyaunga wa Rukwa aliibeba sana Simba,
David Okoth wa Arusha alìbeba sana Simba'
Nasoro Hamduni wa Kigoma aliibeba sana Simba.
Abdulrasul Ismail wa Morogoro aliibeba sana Yanga.
Hawa watu ukimtoa Manyoto Ndipo wote niliwaona kwa macho yangu mwenyewe wakichezesha hivyo sitodanganywa na mtu kuhusu uchezeshaji wao.
 
Mkuu Hata zamani marefa walikua na upendeleo
Manyoto Ndimbo Alibeba sana Yanga.
Msafiri Mkelemi wa Tabora Alibeba sana Yanga.
Bakari Bendera wa Tanga aliibeba sana yanga.
Hafidhi Ali wa Zanzibar aliibeba sana Yanga.
Mussa Lyaunga wa Rukwa aliibeba sana Simba,
David Okoth wa Arusha alìbeba sana Simba'
Nasoro Hamduni wa Kigoma aliibeba sana Simba.
Abdulrasul Ismail wa Morogoro aliibeba sana Yanga.
Hawa watu ukimtoa Manyoto Ndipo wote niliwaona kwa macho yangu mwenyewe wakichezesha hivyo sitodanganywa na mtu kuhusu uchezeshaji wao.
Sijajua wewe unazungumza zamani gani, kwa sababu hata mwaka 2010 inaweza kuwa ni zamani kwa watu wengine. Wengi uliowataja ninafahamau walichezesha miaka ya themanini na tisini, mimi ninaongelea waliochezesha miaka ya sabini wakati wa TANU, nafikiri niliweka wazi jambo hilo. Kwa mfano aliyechezesha ile derby iliyokinukisha Nyamagana; pamoja na intensity yake, refa alitoka klini sana.
 
Back
Top Bottom