Jaman kuna sisi ambao tunarudi shule mnatuambiaje?

Jaman kuna sisi ambao tunarudi shule mnatuambiaje?

Point less

Senior Member
Joined
Jun 24, 2020
Posts
194
Reaction score
98
Kuna sisi ambao tunarudi mashuleni kuanzia leo hadi juma tatu, kama watu wenye busara na fikra endelevu tushaurini vyakuvifanya ambavyo sio vya kufanya kwa mafanikio kujenga taifa amina 🙂
 
Cha kufanya: ukasome kwa bidii
Cha kutokufanya: usichanganye mafaili dili na masomo kwanza.
Uwe na masomo mema kila la kheri Mungu awe salama na mafanikio yako kwa kila jema unalofanya.
 
Cha kufanya: ukasome kwa bidii
Cha kutokufanya: usichanganye mafaili dili na masomo kwanza.
Uwe na masomo mema kila la kheri Mungu awe salama na mafanikio yako kwa kila jema unalofanya.
Asante kwa ushauri mkuu ntajitahidi
 
Huu ni mwaka wa mwisho, ukiweza kuutumia vizuri unaweza kufanya vizuri.

Jibane, jinyime starehe kwa kipindi hiki kifupi.

Matumizi ya simu kwa namna yoyote ile ni kansa kwa mafanikio ya darasani.

Ukiweka nia inawezekana.

Kila la kheri mwanangu.
Asante mkuu simu nita ifungia sitatumia maana naenda bweni. Imefelisha wengi pia,ntayakumbuka maneno zako nikiwa shule
 
Asante mkuu simu nita ifungia sitatumia maana naenda bweni. Imefelisha wengi pia,ntayakumbuka maneno zako nikiwa shule

Vyema sana, usisahau pia swala la nidhamu.

Kuna sera ya ukitakiwa kupewa adhabu hata kama kosa siyo lako, kubali kwanza adhabu halafu baada ya adhabu ndiyo ugome. Sijui kama bado inatumika hii, sisi ilitusaidia kumaliza shule bila suspension wala kufukuzwa.
 
Duh!Iyo ina bidi niifanyie mazoezi maana wamefukuzwa wanne japo ngumu kidogo 🙁 kuhusu nidhan sita kuangusha
 
Duh!Iyo ina bidi niifanyie mazoezi maana wamefukuzwa wanne japo ngumu kidogo 🙁 kuhusu nidhan sita kuangusha

Mwaka wa mwisho una majaribu mengi sana, ile tu kujiita LY unaona kama mnalingana na waalimu.

Akili lazima itumike sana, ukikaa hovyo unashangaa umekula suspension ya mwezi, tayari inakutoa relini.

Bora uonekane bwege ila umalize kilichokupeleka.

Maliza topics zote kwa key subjects by May, then endelea kufanya reviews.

All the best.
 
Asanteee!Icho ndo kitu ambacho sitawahi fanya wakati wa shule asante sana
Wengi tunasemaga ivyo ila ukifika form 3 mambo yanabadilika. Hisia zinaposhindana na matamanio. Kaza buti elimu ndio kila kitu
 
Back
Top Bottom