Hakuna sababu ya kununua chakula kwa ajili ya WW3. Sisi hatuna interest yoyote na vita vya tatu. Labda ungeshauri serikali inunue madawa, vifaa tiba, mafuta, gesi na mahitaji mengineyo ambayo tuyaagiza nje. Sisi tutakuwa tunalima huku mabosi zetu wakipigana kivyao huko majuu. Tutalima hadi wa kula wakosekane maana soko letu la bidhaa za kilimo lipo kwao na wao watakuwa busy na vita. Na vita vitapiganiwa hukohuko wala sio huku kwetu. Na mabaki ya silaha zitakazobaki baada ya vita tutauziwa sisi tusiojua hata kuzitengeneza. Narudia tena usije ukajaribu kununua mahindi eti yatapanda bei au yataadimika. Nunua bidhaa amabazo nchi yetu na Afrika kwa ujumla hawazalishi.