Jamani fuatilieni Halmashauri mbalimbali, sasa zinamwaga ajira

Jamani fuatilieni Halmashauri mbalimbali, sasa zinamwaga ajira

Clark boots

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
6,770
Reaction score
6,202
Kweli Mama Samia anaupiga mwingi, Ajira zinazomwagwa Sasa hv na Halmashauri mbalimbali nchini ni kufuru yaan Kila Halmashauri Ajira kibao Watendaji wa mitaa, mabwana Shamba na mifugo, madereva, maafisa manunuzi. Tembeleeni tovuti za halmashauri mbalimbali ili mufahamu namna ya kuomba kazi hzi.

Kila la kheri JobSeekers.
Hadi Sasa Halmashauri zilizotangazwa Ajira ni kama ifuatavyo na bado Halmashauri zingine zinaendelea kutangaza.

Halmashauri ya Masasi mji.
Halmashauri ya Newala mji.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Halmashauri wilaya ya Kondoa.
Ilemela Mwanza.
Tandahimba.
 
Nimeingia tovuti za wilaya mbili Kati ya ulizotaja hakuna kitu Mkuu,tuwekee hapa links
 
Hizo halmashauri nimezicheki ni afisa mtendaji na madereva ndio wanahitajika


Mabwana shamba na afisa mifugo hakuna


We umeona tangazo lipi mkuu ?
 
Halmashauri nyingi Sana, matangazo ninayo halmashauri zote, Ni zaidi ya hizo ulizoorodhesha,mwenye kuhitaji anipe namba yake ya WhatsApp inbox ili nimtumie, nashindwa jinsi ya kuyaweka hapa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Katika hayo matangazo umewaona mabwana shamba mkuu ?
Matangazo mengi Sana Ni watendaji wa mtaa, wa kijiji, kila halmashauri Ni nafasi 12,14 na Nyasa nafasi 6, Makatibu mukhtasi, madereva, hamashari nyingi Sana mkuu, mabwana shamba wanaweza wakawepo maana sijayasoma yote, Ila watendaji wa mtaa na vijiji ndio wengi Sana, ngoja nikuangalizie halafu nakujulisha inbox au Kama una haraka nitext WhatsApp nikutumie ya halmashauri zote, nayaweka naona yanakataa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Weka mkuu, unashindwa nini au unataka uwape connect nawe wakupe opportunity vijna .?
Halmashauri nyingi Sana, matangazo ninayo halmashauri zote, Ni zaidi ya hizo ulizoorodhesha,mwenye kuhitaji anipe namba yake ya WhatsApp inbox ili nimtumie, nashindwa jinsi ya kuyaweka hapa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tujiandae kuonjo Asali maana bajeti ya mwaka huu imeconsinder katika Kilimo
Nilikuwa nazungumzia Ajira za Mifugo na karimo zilizotangazwa mwez wa 4, sio za kwenye bajeti ijayo hapana ni bajeti ya 2021/2022.
Hizo walitangaza Ila bado hawajatoa muongozo wa maombi..
Nawe una taaluma ya kilimo kama Kunguru wa Manzese...?
 
Back
Top Bottom