RAYMANU254
SPIRITUAL HUSBANDS AN WIVES.
Nataka kuzungumzia somo linalohusu MAJINI MAHABA, kuhusu majini Mahaba kwa Sasa limekuwa tatizo katika jamii yetu.
Kwanza Kabisa tambua kuwa hizi roho zimegawanyika katika makundi matatu.
1-Zinazokuwa kama wanaume
2-Zinazokuwa kama wanawake
3-Zinazokuwa kama watoto.
-Zinazokuwa kama mwanaume hupenda kukaa wa binadamu wanawake,
-Zinazokuwa kama wanawake hupenda kukaa kwa wanadamu Wanaume.
-Watoto huwa ni matokeo ya hizo zote mbili baada ya kukaa kwa mwanadamu, Hivyo zinazokuwa kama watoto hukaa kote yaani kwa WANAWAKE na WANAUME.
Kuna Sababu kadhaa zinazopelekea Mtu kuvamiwa na hizi Roho.
Kuna Sababu kadhaa zinazopelekea Mtu kuvamiwa na hizi Roho.
Kwanza kabisa unapaswa kuelewa kuwa hizi Roho hulenga mahusiano katika maisha ya mwanadamu..
Haya nifuatilia sasa 👇👇👇
SABABU YA HIZI ROHO KUVAMIA MAISHA YA MWANADAMU.
1- Kupenda- Hizi Roho huwa na hisia za kupenda kama ilivyo kwa Mwanadamu, Zinaweza kumpenda mtu na kuamua kuanzia Mahusiano na mtu bila ridhaa ya mtu au bila hata mtu mwenyewe kujua.
Zinaanzisha mahusiano, Kama ni mwanaume zinataka ziwr MKE na kama ni mwanamke huja MUME.
Hii huweza kumtoke mtu hata akiwa anatembea tu hata amekaa akahisi kama kitu kimemvaa. Au Mtu huyu akaota kama anafunga ndoa.
2- Kupitia Ushirikina/Kurogwa- Yaani mtu anaweza kutaka kuharibu mahusiano au Ndoa ya mtu, Anaenda kwa mganga kisha mganga hutuma jina mahaba la kike kwa Mwanaume kama mke au la kiume kwa mwanamke kama mume. Yaani unaozesha bila wewe kujua ili tu mahusiano yako ya kimwili yaharibike.
3- Kwa Njia ya KURITHI.
Kwanza nataka ujue kuwa kibiblia WAZAZI ndo walikuwa Makuhani wa familia zao. Mfano; Ibrahimu muwe wa Isaka, Ayubu, Labani baba yao kina Rachel na Rebecca.
Sasa wazazi na wazee wa ukoo husikilizwa katika wanapoenda kwa Mungu au miungu kw ajili ya Ukoo au familia zao.
Sasa kwa Mila zetu kuna wakati wazee huenda katika mito na milima kuzungumza na hizi ili kukabidha uzao wao mfano; Wanaweza kusema "watoto wote wa kike watakao zaliwa watakuwa WAKE WENU". Sasa hata kama hayo maneno yatasema ukiwa hujazaliwa basi ujue hizo zitafuatilia kizazi hadi kizazi na zitakufikia na kukumiliki tu. Na zitakufuata kwa kuwa tu umezaliwa katika huo ukoo...
4- Kwa njia ya mtu kufanya mapenzi na mtu Pepo mahaba.
Biblia inasema "Aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja nae" 1Kor 16
Ndio maana kuna watu baada ya kushiriki kimwili na watu fulani Mambo yakiharibika sana, Wengine baada tu kushiki mapenzi na watu fulani hadi leo hawezi kudumu katika mahusiano ina maana hizi Roho huwa zinahama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.